Trump asimamisha misaada kwa nchi nyingine kwa siku 90 ili kupitiwa upya. Tanzania nayo kuathirika

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Utawala mpya wa Rais wa Marekani Donald Trump umesitisha na kuzuia misaada ya kimarekani kwa nchi za kigeni.

Marco Rubio ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ameripotiwa kutuma barua kwenye balozi zote duniani kusitisha miradi ya maendeleo ambayo inafadhiliwa na Marekani ndani ya siku 90.

Barua ya Marco Rubio imedokeza kuwa ndani ya siku hizo 90, uongozi mpya wa Trump utafanya uchambuzi kuhusu namna ambavyo Marekani itakuwa inatoa misaada yake kwa nchi nyingine ambapo Rais Trump alidokeza kuwa misaada yote inayotolewa nchi za nje lazima ijibu maswali matatu rahisi:
  1. Je, misaada hiyo inachangia kuifanya Marekani kuwa salama?
  2. Je, inaiimarisha Marekani kama taifa lenye nguvu?
  3. Je, inachangia ustawi wa kiuchumi wa Marekani?

Kwa hiyo ndni ya siku 90 iwapo kuna mradi wowote kutoka Marekani ambao hautajibu hayo maswali matatu muhimu kuna uwezekano mkubwa mradi huo ukafutwa kabisa

Marco.png

Uamuzi wa Trump utakavyoiathiri Tanzania

Kwa nchi za Kiafrika na dunia ya 3 kwa ujumla, uamuzi wa Trump ni pigo kubwa kwa taasisi na miradi ya maendeleo inayotegemea msaada kutoka Marekani.

Ukweli mchungu ni kwamba hata baada ya mapitio hayo, hakuna uhakika kuwa mambo yatarejea kama kawaida.

Hatua hiyo imeshaanza kuleta athari na kusababisha wasiwasi miongoni mwa wafanyakazi wa miradi inayofadhiliwa na Marekani, wengi wao wakiwa hawana uhakika wa ajira zao.

Gazeti la Mwananchi lilipata wasaa wa kuzungumza na baadhi ya wafanyakazi ambao baadhi ya miradi yao inafadhiliwa na Marekani wakieleza wasiwasi yao juu ya uamuzi huo wa Rais Trump.

Esther Jackson (sio jina lake halisi), meneja wa mradi wa elimu ya afya ya uzazi jijini Dar es Salaam, amesema kuwa tangazo hilo limeathiri miradi yao moja kwa moja.

"Baada ya maagizo yale, tulitangaziwa ofisini kuwa miradi tuliyokuwa tunaitekeleza itasimama kwa muda. Kwa sasa tumeambiwa hatuna haja ya kwenda kazini mpaka pale tutakapofahamishwa vinginevyo," amesema Jackson.

================================================================

Secretary of State Marco Rubio ordered an immediate stop to the flow of almost all U.S. foreign assistance Friday pending a review, according to an internal State Department cable obtained by NBC News.

The directive sent to all consular and diplomatic posts follows President Donald Trump’s executive order Monday pausing new obligations and disbursements of foreign aid pending reviews "for programmatic efficiency and consistency" with U.S. foreign policy, within 90 days of the order.

The memo stipulates that U.S. departments, agencies and entities “shall not provide foreign assistance funded by or through the Department and USAID without the Secretary of State’s authorization or the authorization of his designee."

Source: Financial Times, Mwananchi
 
Wakuu,

Utawala mpya wa Rais wa Marekani Donald Trump umesitisha na kuzuia misaada ya kimarekani kwa nchi za kigeni.

Marco Rubio ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ameripotiwa kutuma barua kwenye balozi zote duniani kusitisha miradi ya maendeleo ambayo inafadhiliwa na Marekani ndani ya siku 90.

Barua ya Marco Rubio imedokeza kuwa ndani ya siku hizo 90, uongozi mpya wa Trump utafanya uchambuzi kuhusu namna ambavyo Marekani itakuwa inatoa misaada yake kwa nchi nyingine.

Uamuzi wa Trump utakavyoiathiri Tanzania
Gazeti la Mwananchi linaripoti kwamba uamuzi wa Rais Donald Trump wa kusitisha karibu misaada yote ya kigeni ya Marekani kwa muda, umeshaanza kuleta changamoto kubwa kwa Watanzania.

Hatua hiyo imesababisha wasiwasi miongoni mwa wafanyakazi wa miradi inayofadhiliwa na Marekani, wengi wao wakiwa hawana uhakika wa ajira zao.

Mambo ya vita vita visivyo vya lazima huleta ufukara.
 
Hii imekaa vyema.
Niwakati wa Rusia kutupa misaada sasa.
Nyinyi ni vilema mpaka mtegemee misaada?
Yaani naomba ikiwezekana waikate jumla ili akili zitukae sawa.

Yaani hela za kuhudumia raia hazipo mpaka mnategemea nchi nyingine ziwasaidie,lakini hela za kununu mashangingi mapya kila mwaka na mafuta ya kuyaendesha,kununua wapinzani ili waamie ccm,kunua magoli, kutoa zawadi kwa mashehe na maasikofu, za kiiba na kwenda kuficha uswizi ,za kupeleka wasanii korea hizo zipo za kutosha.
Pumbavu kabisa.
 
Wakuu,

Utawala mpya wa Rais wa Marekani Donald Trump umesitisha na kuzuia misaada ya kimarekani kwa nchi za kigeni.

Marco Rubio ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ameripotiwa kutuma barua kwenye balozi zote duniani kusitisha miradi ya maendeleo ambayo inafadhiliwa na Marekani ndani ya siku 90.

Barua ya Marco Rubio imedokeza kuwa ndani ya siku hizo 90, uongozi mpya wa Trump utafanya uchambuzi kuhusu namna ambavyo Marekani itakuwa inatoa misaada yake kwa nchi nyingine.

Uamuzi wa Trump utakavyoiathiri Tanzania
Gazeti la Mwananchi linaripoti kwamba uamuzi wa Rais Donald Trump wa kusitisha karibu misaada yote ya kigeni ya Marekani kwa muda, umeshaanza kuleta changamoto kubwa kwa Watanzania.

Hatua hiyo imesababisha wasiwasi miongoni mwa wafanyakazi wa miradi inayofadhiliwa na Marekani, wengi wao wakiwa hawana uhakika wa ajira zao.

Esther Jackson (sio jina lake halisi), meneja wa mradi wa elimu ya afya ya uzazi jijini Dar es Salaam, amesema kuwa tangazo hilo limeathiri miradi yao moja kwa moja.

"Baada ya maagizo yale, tulitangaziwa ofisini kuwa miradi tuliyokuwa tunaitekeleza itasimama kwa muda. Kwa sasa tumeambiwa hatuna haja ya kwenda kazini mpaka pale tutakapofahamishwa vinginevyo," amesema Jackson.

================================================================

Secretary of State Marco Rubio ordered an immediate stop to the flow of almost all U.S. foreign assistance Friday pending a review, according to an internal State Department cable obtained by NBC News.

The directive sent to all consular and diplomatic posts follows President Donald Trump’s executive order Monday pausing new obligations and disbursements of foreign aid pending reviews "for programmatic efficiency and consistency" with U.S. foreign policy, within 90 days of the order.

The memo stipulates that U.S. departments, agencies and entities “shall not provide foreign assistance funded by or through the Department and USAID without the Secretary of State’s authorization or the authorization of his designee."

Source: Financial Times, Mwananchi

Trump yupo sahihi, kila nchi ianze kujitambua na kuanza kujitegemea wao wenyewe Sasa, wasiendelee kuitegemea Marekani. Safi Sana hii, hii itawalazimisha Watu wengine waliopo duniani kote hususani Watu weusi kuanza kujitambua na kupata akili nzuri ya kuweza kujitegemea. Hatua hizi za Utawala wa Trump ni Kama 'Black Consciousness Campaign' kwa Watu weusi wote kabisa hapa duniani ili waache kutegemea Misaada kutoka Marekani. Ni mwanzo mzuri.

Kwanza Watawala wengi sana wa kutoka katika nchi za Afrika pamoja na Vibaraka wao daima wamekuwa wakiwasema vibaya sana Wazungu hususani Watu wa Marekani kuwa ni Mabeberu na Wapenda Ushoga, Sasa kwa hatua hizi za Utawala wa Trump zitasaidia Sana kukomeshwa kwa hiyo Misaada inayodaiwa kuwa eti 'imetoka na Mabeberu na Wapenda Ushoga.'
Watu wa Afrika (Watu weusi) hususani waTanzania sasa wanatakiwa waelekeze maombi yao ya Misaada kwenda kwa Marafiki zao wa nchi za Mashariki ambao wanawaona kuwa siyo Mabeberu na Wasiopenda Ushoga, nchi za China, Urusi, Korea ya Kaskazini, Belarus, n.k ili waweze kupatiwa Misaada kutoka huko.
 
Mfano Tanzania tunapenda misaada kivipi wakati rasilimali nyingi za mpaka kula bata tunazo?

Trump yupo sahihi tujitafakari bana tutasaidiwa mpaka lini sisi!
Very good observation! Tuna fedha za kununua magoli, tuna fedha za kusafirisha machawa wa Samia kwenda Korea, tuna fedha za kununua ndege ya raia brand new na nyingine ya watu mashuhuri.... yaani tuna uwezo mkubwa.
 
Trump amefikiria akaona kuna nchi zinamchezea.. Yaani kutinga tu AFCON watu wamelamba milioni 700, bado kuna mamilioni yanatolewa kwenye goli la mama na ngumi ya mama halafu bado hiyo nchi ipo kwenye orodha inasubiria msaada huo ni upumbavu.
 
Pia misaada ya wenzetu wanaotumia ARV imeondolewa?
 
Wakuu,

Utawala mpya wa Rais wa Marekani Donald Trump umesitisha na kuzuia misaada ya kimarekani kwa nchi za kigeni.

Marco Rubio ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ameripotiwa kutuma barua kwenye balozi zote duniani kusitisha miradi ya maendeleo ambayo inafadhiliwa na Marekani ndani ya siku 90.

Barua ya Marco Rubio imedokeza kuwa ndani ya siku hizo 90, uongozi mpya wa Trump utafanya uchambuzi kuhusu namna ambavyo Marekani itakuwa inatoa misaada yake kwa nchi nyingine ambapo Rais Trump alidokeza kuwa misaada yote inayotolewa nchi za nje lazima ijibu maswali matatu rahisi:
  1. Je, misaada hiyo inachangia kuifanya Marekani kuwa salama?
  2. Je, inaiimarisha Marekani kama taifa lenye nguvu?
  3. Je, inachangia ustawi wa kiuchumi wa Marekani?

Kwa hiyo ndni ya siku 90 iwapo kuna mradi wowote kutoka Marekani ambao hautajibu hayo maswali matatu muhimu kuna uwezekano mkubwa mradi huo ukafutwa kabisa

Uamuzi wa Trump utakavyoiathiri Tanzania

Kwa nchi za Kiafrika na dunia ya 3 kwa ujumla, uamuzi wa Trump ni pigo kubwa kwa taasisi na miradi ya maendeleo inayotegemea msaada kutoka Marekani.

Ukweli mchungu ni kwamba hata baada ya mapitio hayo, hakuna uhakika kuwa mambo yatarejea kama kawaida.

Gazeti la Mwananchi linaripoti kwamba uamuzi wa Rais Donald Trump wa kusitisha karibu misaada yote ya kigeni ya Marekani kwa muda, umeshaanza kuleta changamoto kubwa kwa Watanzania.

Hatua hiyo imesababisha wasiwasi miongoni mwa wafanyakazi wa miradi inayofadhiliwa na Marekani, wengi wao wakiwa hawana uhakika wa ajira zao.

Esther Jackson (sio jina lake halisi), meneja wa mradi wa elimu ya afya ya uzazi jijini Dar es Salaam, amesema kuwa tangazo hilo limeathiri miradi yao moja kwa moja.

"Baada ya maagizo yale, tulitangaziwa ofisini kuwa miradi tuliyokuwa tunaitekeleza itasimama kwa muda. Kwa sasa tumeambiwa hatuna haja ya kwenda kazini mpaka pale tutakapofahamishwa vinginevyo," amesema Jackson.

================================================================

Secretary of State Marco Rubio ordered an immediate stop to the flow of almost all U.S. foreign assistance Friday pending a review, according to an internal State Department cable obtained by NBC News.

The directive sent to all consular and diplomatic posts follows President Donald Trump’s executive order Monday pausing new obligations and disbursements of foreign aid pending reviews "for programmatic efficiency and consistency" with U.S. foreign policy, within 90 days of the order.

The memo stipulates that U.S. departments, agencies and entities “shall not provide foreign assistance funded by or through the Department and USAID without the Secretary of State’s authorization or the authorization of his designee."

Source: Financial Times, Mwananchi
Trump hana akili, hii maana yake ndio kusema anavunja mahusiano na mataifa mengine duniani, China na Russia wa wakisikia habari hizi watafurahi sana na kucheza msondo, watalitumia hilo gape kuongeza marafiki na ushawishi na kupanua wigo wao wa kuwekeza kiuchumi kwenye hayo mataifa yatakayotengwa na Marekani.
US ndio inaenda kutengwa na dunia,
 
Back
Top Bottom