Bulamba
JF-Expert Member
- Sep 17, 2011
- 13,741
- 13,049
Dakika chache tu zilizopita, Rais wa Marekani Bw. Donald J. Trump, katangaza kuwa shirika la madawa la Marekani, FDA, limeruhusu dawa ya malaria, ambayo wengi wetu tumeitumia sana, kuanza kutumika katika kutibu virusi vya Corona.
Chloroquin, ndo dawa yenyewe. Matumizi yatakuwa kwenye hatua ya clinical trial.
Idadi ya vidonge vya chloroquin nilivyovimeza maishani mwangu haihesabiki. Achilia mbali sindano zake. Dozi ya sindano ilikuwa ni 1x3.
Hats off kwa “mabeberu”.
Sisi tuna wachawi wengi sana na waganga wengi tu wa kienyeji.
Kama kweli hawa wataalamu wetu wana huo ujuzi ambao hudaiwa wanao, kwa nini washindwe kwenye hili la kutibu Corona?
Heko Marekani. Mchango wake kwenye advancement of humanity hauelezeki kwa maneno.
bado haijafanyiwa utafiti