Trump atia saini amri ya kujiondoa kwa Marekani kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa

Nadhani kunaenda kutengenezwa aina mpya ya ukoloni mamboleo ukiondoa huu wa mtandao wa umoja wa mataifa ambapo mfadhili mkuu kaamua kujitoa. Mlengwa mkuu ni Afrika ila naona bado yuko usingizini kama kawaida yake. Miaka ya 1940s tutajitetea kuwa hatukuwa huru, huu unaokuja sijui tutajiteteaje.
... sasa tutasaini mikataba kama ambayo Zelensky anaambiwa asaini, yaani 'MSAADA KWA MADINI BURE'! HATUNA NAMNA ZAIDI YA KUJISALIMISHA, NA UKICHELEWA INAKULA KWAKO!
Mliokuwa mnasubiri 'NEW WORLD ORDER' ndiyo hii INAKUJA!
 
Trump kashtukia kuwa wao ndo sababu ya mbo mengi ya kipuuzi kupata kibali duniani kwa sababu ya pesa wanazotoa.

Kumbuka ni rais aliekaa madarakani miaka minne kuna mambo alijifunza kuwa ndo sababu kubwa inayoifelisha Marekani kusimama katika ubora wake vile inavotakiwa.

Haiwezekani wewe mashirika yote muhimu duniani unatoa michango mikubwa alafu kuna watu wanajiita wao ndo super power.

Naonq vile issue ya BRICS inavoenda kuvunjika maana mpaka sasa inakosa mvuto.

Marekani nae anataka kuja kuwekeza Tanzania kama wachina wanavokuja na sio kupitia mashirika ambayo kiuhalisia yamekaa kimakakati mno kwa wanufaika wachache.
... bado kuna cha kuwekeza hapa? ... labda Congo!
 
Trump alisisitiza "uwezo mkubwa" wa Umoja wa Mataifa lakini akasema hauendeshwi ipasavyo.
Trump analipa kisasi kwa nani yaani kwa mfano? Maana sasa hatumuelewi ni km ana bifu na dunia nzima kwani dunia nzima ndio iliyotaka kumuua basi wale waliotaka kumuua waliona mbali sana huyu mwehu akiendelea hivi hafiki mbali lazima wamdedishe maana usenge anaoufanya ni mwingi sana anatibua tibua kila kitu kila alichokikuta ofisini kwa Biden hakitaki

Mfalme Charles wa Uingereza pamoja na ukuu wake wa kifalme hafanyi km anavyofanya Mfalme Trump wa Marekani
 
Trump analipa kisasi kwa nani yaani kwa mfano? Maana sasa hatumuelewi ni km ana bifu na dunia nzima kwani dunia nzima ndio iliyotaka kumuua basi wale waliotaka kumuua waliona mbali sana huyu mwehu akiendelea hivi hafiki mbali lazima wamdedishe maana usenge anaoufanya ni mwingi sana anatibua tibua kila kitu kila alichokikuta ofisini kwa Biden hakitaki
Wapi alipokwambia kuwa analipa kisasi? Hiyo si ni donation tu. Akiona ipo kinyume na matarajio ya nchi yake kwanini mseme ana bifu na dunia?
Kama hamkutosheka na kumkosakosa kumuua si muende mkamuue tena? Kwani mmekatazwa?
 
Huyo jamaa aongeze ulinzi maana anafanya ujinga ujinga mwingi kwa muda mfupi sana yaan ujinga ujinga mwingi mpaka mwingine unashangaa huyu mwamba ana bifu na nani? Maana Trump kwa mabifu tu hajambo sasa aendelee na mabifu mimi nasubiria breaking news tu hapa Trump is Dead
 
Wala hana bifu na mtu, US wenyewe wanamkubali kichizi. Amewafungua macho, sasa hivi watu hawaangalii Netflix, bali waafuatilia series za White house, Congress na Senate.
Vumilia tu, jipe muda mkuu, utakuja kumkbali mwenyewe
 
Bado Mkuu tuna madini mengi muhimu kwa mfano uranium iko huko Ruvumq na hizo rare minerals ziko Huko Songwe ndo kwanza wako stage za mwanzo kuzichimba. (kumbuka hizi ndo zinatafutwa mno)
Hizo simuliza za tuna nani kawafundisha? Tuna wewe na nani? Inakuhusu nini wewe hio Uranium ya wale waliopo kule kwenye meza kuu? Wewe komaa tu na kuendesha bodaboda uingize bukubuku kesho ukawapigie magoti Chama cha Vegetables
 
Wala hana bifu na mtu, US wenyewe wanamkubali kichizi. Amewafungua macho, sasa hivi watu hawaangalii Netflix, bali waafuatilia series za White house, Congress na Senate.
Vumilia tu, jipe muda mkuu, utakuja kumkbali mwenyewe
Hakuna kitu km hicho huyo Mzee wa kutibuatibua opportunist Trump ni Mfanya biashara usilisahau hilo anaangalia maslahi ya biashara zake yeye km yeye sio maslahi ya watu wengine, sasa huku kampandishia China huku UN anaanza kufolokonyoa kule BRICS anawapiga biti hili jamaa vipi kwani?
 
Kwani huyo Mchina na BRICS hawailengi US?
Hiyo UN ina msaada gani kwa US na EURO?

Na hawa nao ni Trump?

Baada ya miaka 4 raisi ajaye wa Marekani atairudisha tena Marekani kwenye hayo mashirikia

Hizi ni drama tu za miaka 4 na kisha zitaishia hapo

Trump ni mwendawazimu
 
Saa100 asome ulichoandika
... nawaonea huruma sana watembeza bakuli wa Dunia, lakini, vilivile, nawaonea huruma sana jamaa waliokuwa wanazunguka Marekani na Maulaya kulalamikia matokeo ya chaguzi nchini kwao, maana sasa hivi watarudishwa kama wahamiaji haramu!
🤣
 
Rais wa Marekani, Donald Trump, Jumanne alitia saini amri ya kujiondoa kwa Washington kutoka mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa, yakiwemo Baraza lake la Haki za Binadamu (UNHRC), huku akianzisha mapitio mapana ya ufadhili wa Marekani kwa taasisi hiyo ya kimataifa

Amri hiyo ilitangaza kujiondoa kwa Washington kutoka Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UNHRC) na shirika kuu la misaada kwa Wapalestina la Umoja wa Mataifa (UNRWA), huku ikipanga kupitia upya ushiriki wake katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).

Soma pia: Miongoni mwa Amri alizosign Trump Januari 20, 2025

Hatua hizo zilichukuliwa kama njia ya kupinga kile ambacho katibu wa Ikulu ya white house, Will Scharf, alikiita "upendeleo wa kupinga Marekani" katika mashirika hayo ya Umoja wa Mataifa.

Wanachama 47 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa huchaguliwa na Baraza Kuu kwa vipindi vya miaka mitatu, huku kipindi cha hivi karibuni cha Marekani kikimalizika tarehe 31 Desemba. Kwa sasa, Marekani ina hadhi ya mwangalizi katika baraza hilo.

Amri hiyo ya Jumanne inaonekana kumaliza kabisa ushiriki wa Marekani katika shughuli za baraza hilo, ambazo zinajumuisha mapitio ya rekodi za haki za binadamu za nchi mbalimbali na madai maalum ya ukiukwaji wa haki.

"Kwa ujumla, amri ya kiutendaji inataka mapitio ya ushiriki na ufadhili wa Marekani katika Umoja wa Mataifa kwa kuzingatia tofauti kubwa za viwango vya ufadhili kati ya nchi mbalimbali," alisema Scharf.

Trump alisisitiza "uwezo mkubwa" wa Umoja wa Mataifa lakini akasema hauendeshwi ipasavyo.

"Unapaswa kufadhiliwa na kila mtu, lakini sisi tunachangia kwa kiasi kikubwa zaidi, kama ilivyo kawaida kwetu," alisema.

Trump kwa muda mrefu amekuwa akilalamikia kiwango cha ufadhili wa Washington kwa mashirika ya kimataifa, akitaka mataifa mengine yaongeze michango yao, hasa katika muungano wa kijeshi wa NATO.

UNRWA ndicho chombo kikuu cha misaada kwa Wapalestina, ambapo wengi wa watu milioni 1.9 waliokoseshwa makazi kutokana na vita vya Gaza wanategemea misaada yake ili kuishi.

Chini ya Trump, Washington imeunga mkono hatua ya Israel kupiga marufuku shirika hilo, baada ya mshirika wake huyo wa Marekani kulishutumu UNRWA kwa kusambaza nyenzo za chuki.

Ufadhili wa Marekani kwa UNRWA ulisitishwa Januari 2024 na utawala wa rais wa wakati huo Joe Biden baada ya Israel kuwatuhumu wafanyakazi 12 wa shirika hilo kushiriki katika shambulio la Hamas la Oktoba 7, 2023.

Mfululizo wa uchunguzi ulibaini baadhi ya "masuala yanayohusiana na kutokuwa na upendeleo" ndani ya UNRWA, lakini haukupata ushahidi wa kuthibitisha madai makuu ya Israel, na wafadhili wengi wengine waliokuwa wamesitisha ufadhili wao wakarejesha msaada wao wa kifedha.

Katika kipindi chake cha hivi karibuni madarakani, Trump pia alijiondoa kutoka kwenye makubaliano ya hali ya hewa ya Paris na akaanza mchakato wa kujiondoa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), ambalo Marekani ni mfadhili wake mkuu.

Kila mojawapo ya hatua hizi ni marudio ya kile alichofanya katika muhula wake wa kwanza wa urais, ambao ulikamilika mwaka 2021.
a lake la Haki za Binadamu (UNHRC), huku akianzisha mapitio mapana ya ufadhili wa Marekani kwa taasisi hiyo ya kimataifa

Muacheni Donald Trump aendelee kujitoa kwenye kila kitu duniani kwa vile anafikiri USA ni kama peponi. Iko siku atasaini order ya kujitoa kwenye dunia yetu hii.
 
Back
Top Bottom