Habari za mida,
Watu wengi duniani hutumia pombe kwa sababu mbalimbali zikiwemo kulewa, burudani, kuongeza uwezo wa kujichanganya na watu, kusahau matatizo na hisia hasi, kusherehekea, kuburudika na wapendwa wao, n.k.
Watu maarufu, wanasiasa, wafanya biashara wakubwa ni dhahiri kwamba pombe huwa ni sehemu kubwa ya maisha yao kwa sababu wao huingiliana na watu wengi zaidi, hushinikizwa sana yaani kwa kifupi ni kwamba wanashughulika na watu sana kuliko mtu wa kawaida na yote hayo yanahitaji kujiliwaza ili kuongeza uwezo.
Donald Trump rais wa 45 wa Marekani alishawai kusikika katika moja ya hotuba zake akisema hajawai kugusa pombe wala sigara maishani mwake! Wengi walishangazwa na hili kwa kuwa nafasi ya aliyokuwanayo Trump bila kumwagilia moyo aliwezaje?
Trump alienda mbali na kueleza kuwa alijifunza kutoka kwa kaka yake Fred Trump Jr ambaye alikuwa na tatizo la uraibu wa pombe. Anasema kaka yake alikuwa akimwambia kwa msisitizo mkali "Don't drink" yaani usinywe na akiogeza "Don't smoke" yaani usivute sigara.
Trump anasema kupitia kaka yake alijifunza na hajawai kuwa na nia wala tamaa ya kunywa pombe wala kuvuta sigara. Trump anakili kwamba Fred ndiyo alikuwa na muonekano, akili na utu kuliko yeye lakini pombe ilimuharibia.
Fred Trump Jr ndiye alikuwa mtoto mkubwa wa kiume wa tajiri Fred Trump na ndiye alikuwa anategemewa kuja kuwa mrithi wake, lakini mipango ya baba yake kumfanya mrithi iliisha baada Trump Jr kuamua kuachana na biadhara ya familia na kwenda kusomea na kuwa rubani, aliingia kwenye shida ya ulevi sugu aliishia kupoteza kazi ya urubani na kuishi maisha magumu.