Trump hatashinda japo na Kamala Harris hatauweza urais wa Marekani kipindi ambapo taifa hilo linadidimia

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Baada ya kufuatilia kwa makini mkutano mkuu wa Democratic na kampeni za Donald Trump nimegundua kwamba Trump hatoweza tena kamwe kuupata uraisi wa Marekani anaoutamani.

Historia ya maisha yake ya kihuni na kupenda ubaguzi pamoja na uadui kwa waislamu hautamuwezesha Donald Trump kurudia kwenye kiti cha uraisi. Wamarekani wanaompinga wakiwemo wa rangi mbali mbali na wahamiajia hawatampigia kura kabisa.

Trump atabaki na kundi la wabaguzi wa rangi ambao hawatotosha kumpatia kura za uraisi.

Kwa maana hiyo Kamalla Harris ndiye atakayekuwa mshindi wa kiti hicho,kwanza kwa vile ni mwanamke na enzi hizi wanawake ni wengi sana kwenye chaguzi za mataifa mengi na ni rahisi kushawishika na vitu ambavyo si rahisi kuwapata wanaume.

Vile vile Kamalla ni Mmarekani mwenye asili ya nje ambapo katika Marekani idadi ya watu hao ni wengi sana. Waliotokea Afrika, America kusini, China na bara hindi. Wote hao ni wapiga kura wake.

Wapiga kura Waislamu japo sio wengi lakini wote pamoja na matatizo ya viongozi wa Democratic akiwemo raisi wa sasa Biden kujipendekeza kwa mayahudi,pamoja na hivyo Trump anaonekana ni hatari zaidi kwao kuliko Kamalla.

Tukija upande wa Kamalla ambaye ana asilimia kubwa za kushinda.Jee atauweza uraisi huo wakati taifa hilo liko kwenye hali mbaya za kiuchumi na liko mbioni kuzama.

Uadui na mataifa makubwa kama Urusi na China pamoja na vita vya Gaza ni majukumu ambayo huwa ni mazito kwa raisi mwanamke.

Kwa namna yoyote ile kinachoendelea kwa Marekani kwa sasa ni tope ambalo hatimaye litaizamisha na kuwa nafuu kwa dunia nzima baada ya taifa hilo kufanya jeuri na kufuru kwa muda mrefu duniani.
 
Trump kama atakosa urais haitakuwa kwa sababu ya kuuchukia uislam kwa sababu kura ya Marekani haiamuliwi na waislam ambao huko Marekani dini yao haitambuliki kama dini bali wanaiona kama Cult tu kwani hakuna hata sikukuu ya kiislamu inayosherehekewa katika nchi hiyo.

Uchumi wa Marekani kwa sasa hauko vibaya kama unavyojaribu kudanganya ila wa Russia ndio unaelekea pabaya.

Kwa ukuaji wa uchumi unavyoonyesha hakuna taifa lolote ambalo uchumi wake utaweza kuupita wa Marekani kwa karne hii tuliyopo.
 
Kamala huenda historia ikaja kumuandika kama ndie rahisi alofiwa na Americant mikononimwe

Ila usilolijua ama umelisahau nikwamba kura za marekani hazichaguliwi na raia wamarekani kama ulivyoandika hapo

Wamarekani zaidi ya 200M+ sijui 300M+ wanachaguliwa ama wanateuliwa rais wao na kakikundi chawatu tu hawazidi hata mia nne(400) sijui mia tano (500)

Moja ya nchi inayotakiwa kufunzwa kuhisiana na demokrasia basi marekani inatakiwa iende ikajifunze demokrasia hata kwa Zimbabwe au Venezuela
 
Trump kama atakosa urais haitakuwa kwa sababu ya kuuchukia uislam kwa sababu kura ya Marekani haiamuliwi na waislam ambao huko Marekani dini yao haitambuliki kama dini bali wanaiona kama Cult tu kwani hakuna hata sherehe ya kiislamu inayosherehekewa katika nchi hiyo.

Uchumi wa marekani hauwezi kua mzuri au imara kwakudanganya watu kua uchumi wa russia ndio mbaya kijana

Badala yake ilitakiwa utoe takwimu za uzuri za uchumi wa Americants na ubaya wa uchumi wa Russia tulinganishe
 
Kamala huenda historia ikaja kumuandika kama ndie rahisi alofiwa na Americant mikononimwe

Ila usilolijua ama umelisahau nikwamba kura za marekani hazichaguliwi na raia wamarekani kama ulivyoandika hapo

Wamarekani zaidi ya 200M+ sijui 300M+ wanachaguliwa ama wanateuliwa rais wao na kakikundi chawatu tu hawazidi hata mia nne(400) sijui mia tano (500)

Moja ya nchi inayotakiwa kufunzwa kuhisiana na demokrasia basi marekani inatakiwa iende ikajifunze demokrasia hata kwa Zimbabwe au Venezuela
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Umeua sana.
 
Baada ya kufuatilia kwa makini mkutano mkuu wa Democratic na kampeni za Donald Trump nimegundua kwamba Trump hatoweza tena kamwe kuupata uraisi wa Marekani anaoutamani.
Historia ya maisha yake ya kihuni na kupenda ubaguzi pamoja na uadui kwa waislamu hautamuwezesha Donald Trump kurudia kwenye kiti cha uraisi.Wamarekani wanaompinga wakiwemo wa rangi mbali mbali na wahamiajia hawatampigia kura kabisa.
Trump atabaki na kundi la wabaguzi wa rangi ambao hawatotosha kumpatia kura za uraisi.
Kwa maana hiyo Kamalla Harris ndiye atakayekuwa mshindi wa kiti hicho,kwanza kwa vile ni mwanamke na enzi hizi wanawake ni wengi sana kwenye chaguzi za mataifa mengi na ni rahisi kushawishika na vitu ambavyo si rahisi kuwapata wanaume.
Vile vile Kamalla ni Mmarekani mwenye asili ya nje ambapo katika Marekani idadi ya watu hao ni wengi sana.Waliotokea Afrika,America kusini,China na bara hindi.Wote hao ni wapiga kura wake.
Wapiga kura waislamu japo sio wengi lakini wote pamoja na matatizo ya viongozi wa Democratic akiwemo raisi wa sasa Biden kujipendekeza kwa mayahudi,pamoja na hivyo Trump anaonekana ni hatari zaidi kwao kuliko Kamalla.
Tukija upande wa Kamalla ambaye ana asilimia kubwa za kushinda.Jee atauweza uraisi huo wakati taifa hilo liko kwenye hali mbaya za kiuchumi na liko mbioni kuzama .Uadui na mataifa makubwa kama Urusi na China pamoja na vita vya Gaza ni majukumu ambayo huwa ni mazito kwa raisi mwanamke.
Kwa namna yoyote ile kinachoendelea kwa Marekani kwa sasa ni tope ambalo hatimaye litaizamisha na kuwa nafuu kwa dunia nzima baada ya taifa hilo kufanya jeuri na kufuru kwa muda mrefu duniani.
Kuanguka kwa Marekani itakua ni ahueni kubwa kwa Dunia na uhai wa Mwanadamu..Ni Jambo jema sana yeyote atakaetusaidia iwe Kamala au mtu mwingine yeyote itakuja Jambo jema..

Maelfu ya Watu mamilioni ya vizazi vimeteketea achilia mbali mali zilizoharibiwa kwa ajili tu Nchi hiyo ya marekani inavyotumia vibaya maguvu yake ya kijeshi kuua na kuharibu hii Dunia.

Kile kinachoitwa UN hata sioni sababu ya kuwepo Kwanini bado tuna kitu kinaitwa UN????? Inafanya nn kwa ajili ya nani?? Marekani ni lini waliona Mgogoro unafukuta sehemu kati ya nchi na nchi wakasaidia kwa haki??? Wao wanaua watu wanafadhili mauaji wanatesa na kuiba .
 
marekani kulingana na systeam yao ilivyo jengeka katika nyanja ya uongozi hasa uraisi hata ukiweka sahani au jiwe kuwa raisi nchi hiyo itaongozeka kama kawaida yule sio mama wa wakuupiga mwingi shule iko pale mkuu na viongozi wa staafu pia wako pamoja na kamala so nchi itasonga vizuri we tafuta visa ukaishuhudie marekani ya kamala
 
Trump kama atakosa urais haitakuwa kwa sababu ya kuuchukia uislam kwa sababu kura ya Marekani haiamuliwi na waislam ambao huko Marekani dini yao haitambuliki kama dini bali wanaiona kama Cult tu kwani hakuna hata sherehe ya kiislamu inayosherehekewa katika nchi hiyo.

Uchumi wa Marekani kwa sasa hauko vibaya kama unavyojaribu kudanganya ila wa Russia ndio unaelekea pabaya.

Kwa ukuaji wa uchumi unavyoonyesha hakuna taifa lolote ambalo uchumi wake utaweza kuupita wa Marekani kwa karne hii tuliyopo.
Hata kama ni marhaba, basi uganye na utafiti mdogo uweze kusema walau chenga chenga na sio pumba zote. Unasema uchumi wake hatuwezi... Kwa Karne hii? Uchumi wake unafanya vizuri kuliko.... Urusi upo vibaya?

God have Mercy
 
Hujapenda maelezo yake?
 
Kamala huenda historia ikaja kumuandika kama ndie rahisi alofiwa na Americant mikononimwe

Ila usilolijua ama umelisahau nikwamba kura za marekani hazichaguliwi na raia wamarekani kama ulivyoandika hapo

Wamarekani zaidi ya 200M+ sijui 300M+ wanachaguliwa ama wanateuliwa rais wao na kakikundi chawatu tu hawazidi hata mia nne(400) sijui mia tano (500)

Moja ya nchi inayotakiwa kufunzwa kuhisiana na demokrasia basi marekani inatakiwa iende ikajifunze demokrasia hata kwa Zimbabwe au Venezuela
Hii uliyoandika hapana. Ni kamba kwa 100%. Umedanganya pakubwa mnoo.

USA kwa sasa ni miongoni mwa nchi tano duniani zenye uchumi mkubwa na imara zaidi wenye kuweza kuhimili misuko suko na kuendelea kuitawala dunia kwa karne nyingine. Uwekezaji wao wa nje, hifadhi ya kutosha ya nishati, nguvu kubwa za kijeshi, mifumo imara ya kiungozi ya taifa lao na Sarafu yao imara hakuna nchi inayoweza kuwakaribia au kuwachokoza. Hivyo, haijarishi Kamala Harris atakuwa rais ama USA ikakosa rais kwa miaka minne ijayo, bado USA itabakia kuwa superpower. Hii ni Facts.

Kuhusu Demokrasia ya USA ni kama hujui chochote. Rais wa USA anachaguliwa na mamilioni ya wamerekani, wajumbe wachache wanaohitimisha kupiga kura ni kuhitimisha maamuzi ya mamilioni ya wamerekani wanaotangulia kupiga kura.
 
Sijui nianze kukujibu wapi kuelekea wapi kijana ila acha nianze juu kwenda chini

Huenda wewe ndio ukawa huelewi kitu chochote wao wanathibitisha kama nani?

Kwamba watu 400+ ndio wanaweza ama wana haki ya kuthibitisha maamuzi ya watu zaidi ya 300M+ wao kama nani kuwazidi hao wengine Million walopiga kura?

Hilo linaonesha wazi kama kura za marekani sio zakidemokrasia kama watu 400+ wanaweza kuthibitisha urais wa mtu maana yake wanaangalia vigezo vyao ila sio wingi wa watu kama wanavyohubiri kua demokrasia ni nguvu ya umma nandio maana Hillary alishinda kura za wananchi kidemokrasia ila akashindwa kuwa rahisi kutokana na kura za kupanga za watu 400+

Mie mbona hakuna sehemu nimeongelea kuhusiana na marekani na kua super power mzee au umechanganya mambo nisome tena vyema hemu kufa kwa nchi sio lazima isiwe super power ila inaweza ikaporomoka kwenye angle nyingi kisiasa kiuchumi kijeshi kimoja wapo ila ikiporomoka kwa vyote ndio inakua imekufa

Kama uingereza ile ndio imekufa kabisa kila angle Americant haijafika huko ila itafika nanatamani iwe chini ya kamala kama atashinda kura zao zamchongoma

Nilichomwambia mleta koment nikwamba alete takwimu za uchumi wa russia na marekani tuone upi unaofanya vyema au msaidie wewe kuleta takwimu tuone maana yeye kachemka sababu aliuongelea uchumi wa russia kana kwamba unaporomoka

Mwisho Americant hakuna demokrasia hata kama mtataka muwatetee kwakiasi gani
 
Baada ya kufuatilia kwa makini mkutano mkuu wa Democratic na kampeni za Donald Trump nimegundua kwamba Trump hatoweza tena kamwe kuupata uraisi wa Marekani anaoutamani.
Historia ya maisha yake ya kihuni na kupenda ubaguzi pamoja na uadui kwa waislamu hautamuwezesha Donald Trump kurudia kwenye kiti cha uraisi.Wamarekani wanaompinga wakiwemo wa rangi mbali mbali na wahamiajia hawatampigia kura kabisa.
Trump atabaki na kundi la wabaguzi wa rangi ambao hawatotosha kumpatia kura za uraisi.
Kwa maana hiyo Kamalla Harris ndiye atakayekuwa mshindi wa kiti hicho,kwanza kwa vile ni mwanamke na enzi hizi wanawake ni wengi sana kwenye chaguzi za mataifa mengi na ni rahisi kushawishika na vitu ambavyo si rahisi kuwapata wanaume.
Vile vile Kamalla ni Mmarekani mwenye asili ya nje ambapo katika Marekani idadi ya watu hao ni wengi sana.Waliotokea Afrika,America kusini,China na bara hindi.Wote hao ni wapiga kura wake.
Wapiga kura waislamu japo sio wengi lakini wote pamoja na matatizo ya viongozi wa Democratic akiwemo raisi wa sasa Biden kujipendekeza kwa mayahudi,pamoja na hivyo Trump anaonekana ni hatari zaidi kwao kuliko Kamalla.
Tukija upande wa Kamalla ambaye ana asilimia kubwa za kushinda.Jee atauweza uraisi huo wakati taifa hilo liko kwenye hali mbaya za kiuchumi na liko mbioni kuzama .Uadui na mataifa makubwa kama Urusi na China pamoja na vita vya Gaza ni majukumu ambayo huwa ni mazito kwa raisi mwanamke.
Kwa namna yoyote ile kinachoendelea kwa Marekani kwa sasa ni tope ambalo hatimaye litaizamisha na kuwa nafuu kwa dunia nzima baada ya taifa hilo kufanya jeuri na kufuru kwa muda mrefu duniani.
shehe naona unaota ndoto baada ya kushiba viazi,
 
Trump kama atakosa urais haitakuwa kwa sababu ya kuuchukia uislam kwa sababu kura ya Marekani haiamuliwi na waislam ambao huko Marekani dini yao haitambuliki kama dini bali wanaiona kama Cult tu kwani hakuna hata sherehe ya kiislamu inayosherehekewa katika nchi hiyo.

Uchumi wa Marekani kwa sasa hauko vibaya kama unavyojaribu kudanganya ila wa Russia ndio unaelekea pabaya.

Kwa ukuaji wa uchumi unavyoonyesha hakuna taifa lolote ambalo uchumi wake utaweza kuupita wa Marekani kwa karne hii tuliyopo.
Umeanza na uislamu wakati mimi katika mambo yatakayomuweka Kamalla kwenye kiti cha uraisi nimeutaja mwisho kabisa.Pamoja na hivyo kura za waislamu nazo katika hesabu kila mgombea atazihitaji na kuzipuuza ndio kushindwa katika mbinu za kupata ushindi.
 
Back
Top Bottom