Trump: "Iran msiache kuandamana, msaada utafika hivi karibuni, Hifadhini majina ya wauaji watalipa gharama kubwa, "

Trump: "Iran msiache kuandamana, msaada utafika hivi karibuni, Hifadhini majina ya wauaji watalipa gharama kubwa, "

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
3,253
Reaction score
9,736
Ameandika hivyo Rais wa Marekani Donald Trump kwenye mtandao wake wa Truth

1768325547670.png
 
Daaah huyu jamaa angetoa tamko kama hilo kuhusu Tz ingerudisha matumaini kwa wengi waliokata tamaa.

Hata kama angetania ila hiyo post peke yake ingetosha sana kuweka mambo sawa.
Ingebidi apewe kitalu Cha GESI huko ntwara kwa akina the big show ikienda sambamba na pande zote mbili kunufaika
 
Kuna watu wanadanganya kuwa nchi inaonewa wivu kwa Sababu ya rare earth minerals mara wanasema uranium na blah blah nyinginezo. Wakati kipaumbele Cha USA Wala sio hicho.

Hizo blah blah wanapiga kwa Sababu hawataki mizozi ya kifisadi waliyojiwekea kwenye nchi na serikali ikatwe
Hao ni wehu

Watawala ndio wanawatuma waseme hivyo ili wazidi kujimilikisha madaraka wao na vizazi vyao.

Unaweza kujiuliza hivi mwananchi wa chini ananufaika vipi na uranium?

At least kungekuwa na fursa ambazo zinamnufaisha mwananchi wa chini kupitia hayo madini. Lakini haipo hivyo.

Hayo madini hayatunafaishi mimi na wewe wa huku chini.

Kama tu hadi madaraja wanayojenga hawaruhusu hata watu kupiga picha ndio waje wakuachie madini unufaike nayo?

Panton za kuvuka kigamboni to Magogoni zote zinapiga marufuku watu kupiga picha. Can you imagine mtu anakubania hadi picha halafu mtu huyu aje akupe mwanya wa kupiga michongo ya maana kupitia rasilimali za nchi?

Watu wa kwanza kunufaika na hizo rasilimali ni watawala then sisi wa low class ndio tutaambulia makapi yaliyodondoka wakati matajiri wakila.

Kwa hiyo wakisema wanatuonea wivu maana yake ni hao matajiri wanufaika na hizo rasilimali ndio wapo kwenye hiyo hofu.

Kwa hali ambayo tunapitia saizi kama nchi ni bora tutawaliwe na mzungu ambaye atajimilikisha hivyo vitu as long as hatutatekwa na kuuliwa hovyo.
 
Umefafanua kwa upana ambao binafsi nisingeweza kufafanua. Umeongea Yale niliyokuwa natamani kuandika siku zote. Umeongea ukweli mtupu
 
Umefafanua kwa upana ambao binafsi nisingeweza kufafanua. Umeongea Yale niliyokuwa natamani kuandika siku zote. Umeongea ukweli mtupu

Mimi naamini kwamba kipindi cha Mwalimu Julius Nyerere na wapigania haki wenzake hakikuwa na mazingira magumu kama tunavyoshuhudia sasa.

Wakati ule, adui alikuwa ni mkoloni mzungu, mtu ambaye hakuwa na DNA ya Kiafrika.

Ilikuwa ni rahisi kuona akiminya uhuru wa watu weusi kwasababu yeye si miongoni mwetu na ukiongeza n ile chuki ya ubaguzi vyote vinampa sababu kubwa ya kufanya ukatili.

Kikawaida, ilitegemewa kuona mzungu ambaye hana DNA ya Uafrika ndiye akiongoza katika ukandamizaji na mateso.

Lakini hali ya sasa imegeuka kuwa ya kusikitisha zaidi. Sio mzungu tena, bali Watanzania wenzetu wale tuliowapa mamlaka na imani ndio wanaotuteka, kutunyanyasa, na kutuua.

Ni kama vile Simba aliyepewa jukumu la kulinda kundi, akageuka na kuanza kushambulia wenzake na kuwala nyama.

Unajua katika jamii wananchi wengi hawajali kuhusu ufisadi wa wanasiasa? Kwa hiyo kuna wananchi hata wakisikia kiongozi fulani kaiba mabilioni wao hata hawajali na bado wakakupigia kura vilevile.

Lakini wananchi hao ukianza tu kuwaua au kuua ndugu zao basi hapo umeingiza chuki na nio kosa ambalo watawala wa sasa wanafanya wakidhani damu ya mtu inaweza kufutwa kwa propaganda.

Sioni umuhimu wowote wa vitabu vya historia kusimulia mapito ya wapigania haki kipindi cha ukoloni na struggles waiizokiwa wanapitia bila kuangalia uhalisia wa sasa.

Kwa sababu mateso tunayoyashuhudia leo ni makubwa kuliko yale ya jana, na cha kusikitisha zaidi ni kwamba wenye mamlaka hawataki kuruhusu yaandikwe kama mabaya.

Wanataka historia iandikwe kwa kalamu ya unafiki, kana kwamba ukatili wa ndani si jambo la kutajwa.

Ndio maana binafsi naamini kama Wakoloni wangekaza kama hivi, sidhani kama hata Nyerere na wenzake wangeweza kupata uhuru katika mazingira haya ya sasa.

Wakati ule, mshikamano wa wananchi ulikuwa silaha kubwa dhidi ya mkoloni. Lakini leo mshikamano huo umevunjwa, na wapo wana jamii wenzetu ambao wamegeuka wasiliti kwa maslahi madogo wanayopata kwa watawala.

Ndiyo maana natamani watu wote wamuone Tundu Lissu kwa jicho la tafakuri pana sana. Si kwa sababu ni mtu mmoja tu, bali kwa sababu anawakilisha ule ujasiri wa kupaza sauti katika giza la hofu.
 
Back
Top Bottom