Trump kuendelea kuisapoti Ukraine katika mapambano yake dhidi ya urusi

Trump kuendelea kuisapoti Ukraine katika mapambano yake dhidi ya urusi

kp kipanya44

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2022
Posts
12,971
Reaction score
15,248
Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, anatarajiwa kuendeleza msaada wa kijeshi wa Marekani kwa Ukraine baada ya kuapishwa tarehe 20 Januari, kwa mujibu wa gazeti la Financial Times


Kwa mujibu wa vyanzo vitatu vilivyoarifiwa kuhusu mazungumzo na maafisa wa Magharibi, Trump anapanga kuendelea kusambaza msaada wa kijeshi wa Marekani kwa Ukraine baada ya uapisho wake.

Vyanzo hivyo vimeeleza kuwa ingawa Trump bado anaamini kuwa Ukraine haipaswi kuwa mwanachama wa NATO na anatamani kumalizika mara moja kwa vita, anaona usambazaji wa silaha kwa Kyiv kama njia ya kufanikisha "amani kupitia nguvu" baada ya kusitishwa kwa mapigano.

Aidha, vyanzo hivyo vimefichua kuwa Trump anatarajiwa kushinikiza nchi wanachama wa NATO kuongeza lengo la matumizi yao ya ulinzi kufikia asilimia 5 ya Pato la Taifa (GDP), kutoka kiwango cha sasa cha asilimia 2. Kwa sasa, ni wanachama 23 pekee kati ya 32 wa NATO wanaotimiza lengo la asilimia 2.

=========================================================


U.S. President-elect Donald Trump intends to maintain U.S. military support for Ukraine after his inauguration on January 20.

That's according to the Financial Times, Ukrinform reports.

According to three sources who were briefed on discussions with Western officials, Trump plans to continue supplying Ukraine with U.S. military aid following his inauguration.

The sources added that while Trump still believes that Ukraine should never become a NATO member and wants an immediate end to the war, he views continued arms supplies to Kyiv as a means to achieve "peace through strength" following a ceasefire.

The sources also revealed that Trump is expected to push NATO member states to increase their defense spending target to 5% of GDP, up from the current benchmark of 2%. Currently, only 23 of NATO's 32 members meet the 2% target.

Source: Ukrinform
 
Habari ndio hiyo wakuu.., Putin bado ana safari ndefu sana katika vita yake huko Ukraine.., na Trump akiamua kuisapoti Ukraine itakuwa mbaya sana kwa urusi maana huyu jamaa ana nguvu kotekote.., kuanzia congles,senate,na kwenye supreme court,hivo Yuko fit haswa na hakuna Cha kumzuia kama Biden alivyokuwa akipata changamoto kubwa kupitisha agenda zake🏃🏃🏃


Lee Van free
 
Habari ndio hiyo wakuu.., Putin bado ana safari ndefu sana katika vita yake huko Ukraine.., na Trump akiamua kuisapoti Ukraine itakuwa mbaya sana kwa urusi maana huyu jamaa ana nguvu kotekote.., kuanzia congles,senate,na kwenye supreme court,hivo Yuko fit haswa na hakuna Cha kumzuia kama Biden alivyokuwa akipata changamoto kubwa kupitisha agenda zake🏃🏃🏃


Mrusi anapambana na mataifa 30 ya NATO.
 
embu tufafanulie Urusi anapambanaje na hayo mataifa 30 ya NATO maana sisi tunaiona Ukraine tu inashambuliwa mbona haya mataifa ya NATO hayashambuliwi na urusi?
Na atufafanulie kuhusu majeshi ya NATO lini yalianza kuingia porini kupigana na mrusi, mana urusi hadi leo anasema NATO wakiingia yeye atashambulia kwa nuclear
 
Kwamba Trump ana uswahiba zaidi na Putin Kuliko maslahi ya taifa lake la Marekani?
Time will tell. NATO ilishapoteza Ukreni kitambo sana tangu walipoamua kuingia vitani na Putin. Hilo shika kabisa, usisahau.

Russia inamiliki 25% ya ardhi ya Ukreni. Hapo vipi?
 
Mayahudi hawaaminiki, yaliyomo katika vufua vyao ni tofauti sana na wanayoongea mdomoni, dini yetu ya kiislam imefahamisha hivyo kwa hawa jamaa. US walipokomea mtu akishashika madaraka kuna njia lazima apite
Vipi maisilamu ya kiarabu
 
Back
Top Bottom