Trump: Nchi za BRICS zenye mpango wa kuikwepa Dola ya Marekani zitakumbana na ushuru wa asilimia 100, Wanaweza kwenda kutafuta “mjinga” mwingine

Mkuu, Kwanza Usifananishe USA na Tanganyika.

Tukirudi kwenye hii point yako,

U.S. private FDI inaenda $127 b hapo hapo Total FDI ni $ 189 b. Hapo tunaongelea zaidi ya 60% ya FDI. Hapo ukumbuke USA kama nchi haiinvest moja kwa moja ila imeweka policy za private sector kufanya hili. Meaning ikiweka kodi 100% lazima policy itabadilika na hawa watu wake watarudi kuwekeza nyumbani au kwenye nchi mbadala.

We sema China TI inaenda kwenye 8T, ukiweka % kulinganisha na Fdi Ina maana hapo ni chini ya 2% kwamba, Mmarekani anaweza kuondoka China na China mambo yakaenda. Swali la kujiuliza ni, China anapozalisha bidhaa anategemea auze wapi?

Hapa ndipo ilipo silaha ya USA.
Soko la China linategemea USA, EU, Japan na Korea kusini kwa approx 38% to 40%, hawa ni wale wa kufuata kile anachosema USA moja kwa moja, Asean countries mchina ana 15% ambapo huku nako somehow USA ana sauti kiasi fulani, ikipotea hata 5% China imepoteza 45% ya Soko. Tunakuja Africa, USA anahitaji only ushawishi wa 5% kukamilisha 50% ya kupotea kwa soko la China.

Silaha ya mchina ipo kwenye mbadala wake, ili hichi kitu kiwezekane USA lazima awe na mbadala wa hiyo 50% jambo ambalo si jepesi au ni gumu kuwezekana sababu ya sera zake za uzalishaji kupelekea labour kuwa juu, inamaana hapa lazima atafute nchi mbadala wa China ambayo raia wake watakubali kutumikishwa kwa gharama nafuu halafu hapo hapo afanye huo uwekezaji wa kiwango cha mbadala wa China,(USA HAPA HATOBOI KIRAHISI) ila kama inawezekana basi unamuona mhindi ila sasa mhindi itachukua muda gani? Mchina hapa ameshika mpini.

Sasa ukiangalia kwa makini, USA na CHINA ni wapinzani wawili ambao mmoja ana mboga na mwingine ana ugali, ni either win-win au Loose-Loose. Nachokiona kiuchumi, mchina na USA wanakamilisha ule msemo wa bora adui umjuaye. Hawa ni maadui wanaofahamiana hivyo panapohitajika sana wanakaa wanakubaliana win-win au Loose-Loose, maadui wa aina hii si wa kuwategemea sana waingie vita kubwa ila ikitokea inakuwa vita hatari mno.

Shortcut nzuri kwa China na BRICS ni kuondoa ushawishi wa EU na nchi nyingine kwa marekani, ila sasa hapa kuna mengi mno, tukiyajadili hatutamaliza.

NB: WALE PRO CHINA NA PRO USA RUKSA KUNISHAMBULIA.
 
Trump sio mara ya kwanza kuwa na mawazo ya kijinga kama haya.

Alijaribu upuuzi wake dhidi ya China katika awamu yake ya kwanza wataalam wa uchumi walimuonya akajifanya kichwa ngumu ila matokeo ya maamuzi yake aliyaona.

Ujinga wa Trump mihemko yake humfanya kuwa wakwanza kuchukua maamuzi huku anaye dili naye anatulia anafuatia kujibu hatua za maamuzi yake.

Huyu Trump China akijibu mapigo yeye mwenyewe atarudi mezani kuweka mambo sawa kama alivyofanya awamu ya kwanza na uzuri mpambe wake Elon ana maslahi makubwa huko China
 
sucker kwenye uborawao
 
Nimejibu kirefu kwenye post namba 201 mkuu, unaweza nikosoa.
Hapa unazungumzia U.S.A ama China ?
 
Weka hapa hayo matokeo usiongee bila data

Kampuni nyingi zilirudisha viwanda Marekani na kutengeneza ajira nyingi, mifano ya kampuni ni Apple, HP, Dell, Adidas, n.k.

Na cha ajabu hakukuwa na mfumuko wa bei kama kwenye awamu ya Biden
 
Ndio mkuu, Ndo maana nikasema USA na CHINA ni maadui wanaofahamiana, tusitegemee vita kubwa vya haraka kwa kiwango cha kumshusha Mchina kutoka USA au kumshusha USA huku mchina akihusika moja kwa moja.

BRICS ni hatua za awali sana za kumshusha USA, sidhani kama USA anaweza ishambulia BRICS kwa hatua kubwa kubwa ni sawa na kupiga majasusi wachache walioingia nchini kwako kwa kutumia Nuke, uharibu kila kitu.

USA itaenda mdogo mdogo kama BRICS wafanyavyo huku ikimtazama Mchina kwa makini maana movement ya mchina ndo ina madhara kiuchumi kwa USA. Mchina akipiga sana USA atapiga sana, akipiga kidogo, USA atapiga kidogo. Kete zinatembea.
 
Weka hapa hayo matokeo.

Kampuni nyingi zilirudisha viwanda Marekani na kutengeneza ajira nyingi,mifano ya kampuni ni Apple, HP, Dell, Adidas, n.k.
Apple ya wapi unayo tolea mfano wewe ? Unajiandikia tu chochote

 
Kampuni ya Apple walihamishia viwanda vyao Marekani 2019, waliofaidika ni wamarekani walioajiriwa, Wamarekani kuongeza vipato, US kuongezaukusanyaji wa kodi husika, n.k.

 
Unaelewa kweli maana ya kuamisha viwanda ?

Maana Apple mpaka leo bado wapo China.

Article yenyewe hiyo umeisoma na kuilewa kweli au umebandika tu hapa tu ?!
 
Unaelewa kweli maana ya kuamisha viwanda ?

Maana Apple mpaka leo bado wapo China.

Article yenyewe hiyo umeisoma na kuilewa kweli au umebandika tu hapa tu ?!
Walirudi China Baada ya Biden kuingia madarakani, Awamu ya Biden ilijikita zaidi kwenye kubadili jinsia
 
Huna akili.

Napoteza muda hapa.
Huna facts ulichobakiza ni matusi tu

Awamu ya Biden kipaumbele kilikuwa ni kubadili jinsia si mambo ya uchumi ndio maana kumekuwa na mfumuko mkubwa sana wa bei Marekani

Siku ya Pasaka pale white house Biden aliizindia na kusherekea Transgender Day of Visibility
 
Duuh yale yale ya kuweka akiba ya US dollar kwa kununua US treasury bond

Akyamama mmarekani alishatushika dunia nzimq, anatuendesha kama mazuzu
Samahani mkuu,siyo kweli mmarekani kashika dunia nzima na wengine wote ni mazuzu anatuendesha atakavyo.
 
Kwani huo ushuru anao sema atapandisha si aliupandisha mwaka 2018 lakini mpaka anaondoka madarakani uchumi wa china ulikuwa hauja athirika chochote.
Wameweka maelfu ya vikwazo dhidi ya Urusi lakini bado wakashindwa kuusabaratisha uchumi wa Urusi.
 
Aiseeeee....
Nimekuelewa vizuri sana....
Yaani...kuna jamii fulani kule Ulaya na US ......
Wanaamini Wachina ni "ALIENS" waliokubaliana kuleta maendeleo..........
 
Aiseeeee....
Nimekuelewa vizuri sana....
Yaani...kuna jamii fulani kule Ulaya na US ......
Wanaamini Wachina ni "ALIENS" waliokubaliana kuleta maendeleo..........
Wewe umenielewa,lakini Kuna jamaa amenitusi,mfumo Bora wa uchumi kusanya alafu rudisha kiasi flani kwa jamii, pia Nina wasiwasi na sera za ccm pia wanakamua Kodi harafu majanga yakitokea hawapo tayari kuchangia mwisho wa siku watu hawana furaha na sababu hawana mbadala wanaendelea na maisha,sera nzuri ni ku shield maisha ya wahanga wanapokumbwa na uncertainty.
Huwezi vuna Kodi yote kwenda kuhudumia deni ambalo hata wahusika hawajui litaisha lini.
Na pia maamuzi makubwa lazima wananchi wahusishwe na sio Ile saccos pale Dodoma,katika swala la nishati safi,bibi anajatibu kutafuta dollar 42.0 billion dollars,lakini kama wananchi wataambiwa faida na matokeo ya mradi huenda wakawa tayari,mbona miradi mingine wananchi wameelewa mfani SGR na Stigler,hakuna namna nchi ikaendeshwa kwa kuviziana kama Hamas na Israel
Pia Kuna huyu mtoto tunae mlea ukubwani I mean Zanzibar,Kuna percentage ya mgao imeongezwa toka asilimia 3.5% mpaka kumi ya Pato la Kodi toka bara hii pia inahitaji uwazi,Kuna athari gani KIUCHUMI na kuna jitihada gani zinatumika kuziba hiyo deficit.Mf Watoa huduma wengi katika taasisi za serikali wanakufa sababu ya stress za kutolipwa kwa wakati,je hii asilimia kumi haijachangia kiasi flani,tuwe wawazi isiwe kama uchumi wa hao "ALIENS"
 
Kwani huo ushuru anao sema atapandisha si aliupandisha mwaka 2018 lakini mpaka anaondoka madarakani uchumi wa china ulikuwa hauja athirika chochote.
Wameweka maelfu ya vikwazo dhidi ya Urusi lakini bado wakashindwa kuusabaratisha uchumi wa Urusi.
Ok boss
 
Sidhani kama hili linahitaji ubishani, Uchumi wa China kufika hapo ulipo ni nguvu ya US na Ulaya. Bila US China asingefika hapo.

China anauza sana US, muda huohuo kampuni nyingi saaana za Ulaya zimewekeza China. Kati ya mataifa ambayo sio rahisi kupambana na US ni China.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…