Tsh
JF-Expert Member
- Aug 26, 2021
- 17,022
- 36,936
Mkuu, Kwanza Usifananishe USA na Tanganyika.Kwani mpaka wanakuja kuagiza hizo bidhaa kwenye nchi zingine hizo bidhaa za ndani hazikuwepo au walikuwa hawazioni?
Viwanda vya nchini Marekani vina jiendesha kwa gharama kubwa sana hivyo kufanya bidhaa zao kuwa juu pia, ndio maana raia wa Marekani wanakimbilia kununua bidhaa za nchi nyingine.
Ni sawa na sisi hapa sukari ya kiwango cha juu kutoka Brazil ina uzwa kwa 1800 wakati sukari isiyo kuwa na ubora kutoka mtibwa inauzwa 3500 hicho ndo kitakacho wakuta wamarekani.
Tukirudi kwenye hii point yako,
U.S. private FDI inaenda $127 b hapo hapo Total FDI ni $ 189 b. Hapo tunaongelea zaidi ya 60% ya FDI. Hapo ukumbuke USA kama nchi haiinvest moja kwa moja ila imeweka policy za private sector kufanya hili. Meaning ikiweka kodi 100% lazima policy itabadilika na hawa watu wake watarudi kuwekeza nyumbani au kwenye nchi mbadala.
We sema China TI inaenda kwenye 8T, ukiweka % kulinganisha na Fdi Ina maana hapo ni chini ya 2% kwamba, Mmarekani anaweza kuondoka China na China mambo yakaenda. Swali la kujiuliza ni, China anapozalisha bidhaa anategemea auze wapi?
Hapa ndipo ilipo silaha ya USA.
Soko la China linategemea USA, EU, Japan na Korea kusini kwa approx 38% to 40%, hawa ni wale wa kufuata kile anachosema USA moja kwa moja, Asean countries mchina ana 15% ambapo huku nako somehow USA ana sauti kiasi fulani, ikipotea hata 5% China imepoteza 45% ya Soko. Tunakuja Africa, USA anahitaji only ushawishi wa 5% kukamilisha 50% ya kupotea kwa soko la China.
Silaha ya mchina ipo kwenye mbadala wake, ili hichi kitu kiwezekane USA lazima awe na mbadala wa hiyo 50% jambo ambalo si jepesi au ni gumu kuwezekana sababu ya sera zake za uzalishaji kupelekea labour kuwa juu, inamaana hapa lazima atafute nchi mbadala wa China ambayo raia wake watakubali kutumikishwa kwa gharama nafuu halafu hapo hapo afanye huo uwekezaji wa kiwango cha mbadala wa China,(USA HAPA HATOBOI KIRAHISI) ila kama inawezekana basi unamuona mhindi ila sasa mhindi itachukua muda gani? Mchina hapa ameshika mpini.
Sasa ukiangalia kwa makini, USA na CHINA ni wapinzani wawili ambao mmoja ana mboga na mwingine ana ugali, ni either win-win au Loose-Loose. Nachokiona kiuchumi, mchina na USA wanakamilisha ule msemo wa bora adui umjuaye. Hawa ni maadui wanaofahamiana hivyo panapohitajika sana wanakaa wanakubaliana win-win au Loose-Loose, maadui wa aina hii si wa kuwategemea sana waingie vita kubwa ila ikitokea inakuwa vita hatari mno.
Shortcut nzuri kwa China na BRICS ni kuondoa ushawishi wa EU na nchi nyingine kwa marekani, ila sasa hapa kuna mengi mno, tukiyajadili hatutamaliza.
NB: WALE PRO CHINA NA PRO USA RUKSA KUNISHAMBULIA.