Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump amekutana na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy katika jengo la Trump Tower huko New York mapema Ijumaa wiki hii na amemuahidi kumaliza haraka vita kati ya Urusi na Ukraine ikiwa atashinda kiti cha Urais wa Marekani.
“Tuna uhusiano mzuri sana na pia nina uhusiano mzuri sana kama unavyojua na Rais Putin, nadhani ikiwa tutashinda, nadhani tutaisuluhisha haraka sana.” Trump alisema kabla ya kukutana na Zelensky ambaye yupo Nchini Marekani kuhudhuria Mkutano wa Umoja wa Mataifa.
Soma pia: Yanayojiri kuelekea Uchaguzi Mkuu Marekani 2024: Nani kuibuka kidedea?
Baada ya wawili hao kukutana na kufanya mazungumzo Trump aliandika katika mtandao wake wa Truth Social kuwa “Ikiwa nitachaguliwa kuwa Rais, vita na Urusi na Ukraine vitaisha haraka. Ikiwa sivyo, vita hivyo havitakwisha kamwe, na vitaingia katika Vita vya Tatu vya Dunia,” amesema.
Awali Kiongozi huyo aliwaambia Waandishi wa Habari kuwa anaamini anaweza kuifanyia kazi ya kumaliza mgogoro wa Urusi na Ukraine lakini alipoulizwa iwapo Ukraine inapaswa kukabidhi ardhi kwa Urusi kumaliza vita, hakujibu moja kwa moja “wacha tupate amani, tunahitaji amani, tunahitaji kukomesha kifo na uharibifu.” alisema.