Trump tena na wachina anasema sasa hivi wanafanya mapinduzi ya kiuchumi lazima washinde

Mi mi

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2024
Posts
6,406
Reaction score
12,736
Ni muendelezo wa Trump na kuwakalia kooni wachina toka awamu yake ya kwanza mpaka sasa kawaweka mdomoni kweli.

Trump anasema anachofanya sasa ni mapinduzi ya kiuchumi na hakika lazima washinde japo anakili maumivu watayapitia ila wanashinda.
China has been hit much harder than the USA, not even close. They, and many other nations, have treated us unsustainably badly. We have been the dumb and helpless “whipping post,” but not any longer. We are bringing back jobs and businesses like never before. Already, more than FIVE TRILLION DOLLARS OF INVESTMENT, and rising fast! THIS IS AN ECONOMIC REVOLUTION, AND WE WILL WIN. HANG TOUGH, it won’t be easy, but the end result will be historic. We will, MAKE AMERICA GREAT AGAIN!!!

Donald Trump Truth Social 04/05/25 08:34 AM

View: https://x.com/TrumpDailyPosts/status/1908499102473613666?t=4exeK0V2JrVHaZopdkNorQ&s=19

Mara ya mwisho kumsikia Xi Jinping akipiga domo kuhusu marekani lini ? Tumuulize ndugu yake na Xi Jinping
 
Kuna watu humu walikuwa wanaichukulia poa nguvu ya kiuchumi ya china hapa duniani wakidai Marekani ndo kila kitu.
Lakini jana baada ya kujibu mapigo kwa kuweka ushuru dhidi ya Marekani masoko ya hisa yaliporomoka kote ulimwenguni Marekani jana na leo tu masoko ya hisa yamepata hasara ya zaidi ya $6 trion na yanazidi kushuka hali yakuwa masoko ya hisa ndani ya china yako kawaida.
 
Yaliporomoka kwa ajili ya tarrifs zilizowekwa na China?
 
Kuna watu humu walikuwa wanaichukulia poa nguvu ya kiuchumi ya china hapa duniani wakidai Marekani ndo kila kitu.
Lakini jana baada ya kujibu mapigo kwa kuweka ushuru dhidi ya Marekani masoko ya hisa yaliporomoka kote ulimwenguni Marekani jana na leo tu masoko ya hisa yamepata hasara ya zaidi ya $6 trion na yanazidi kushuka hali yakuwa masoko ya hisa ndani ya china yako kawaida.
Wenzako huwa wanapiga mahesabu ya mbali sio kama viongozi wako wa shitholes country
 
Ila mwisho wa siku China lazima atapoteza kwani soko kubwa na la uhakika la Marekani kamwe hatabaki nalo kama ilivyokua na hatapata soko mbadala.
 
Kuna watu humu walikuwa wanaichukulia poa nguvu ya kiuchumi ya china hapa duniani wakidai Marekani ndo kila kitu.
Lakini jana baada ya kujibu mapigo kwa kuweka ushuru dhidi ya Marekani masoko ya hisa yaliporomoka kote ulimwenguni Marekani jana na leo tu masoko ya hisa yamepata hasara ya zaidi ya $6 trion na yanazidi kushuka hali yakuwa masoko ya hisa ndani ya china yako kawaida.
Wachina kwa hili wanaficha taarifa sahihi
 
Ila mwisho wa siku China lazima atapoteza kwani soko kubwa na la uhakika la Marekani kamwe hatabaki nalo kama ilivyokua na hatapata soko mbadala.
Hii kauli mnairudia mara kwa mara nawaona kama maroboti.... Siku China ikichukua hatua anazochukua Trump dhidi ya mataifa yote, wewe na mimi tutalia na kusaga meno.
 
Kuna watu humu walikuwa wanaichukulia poa nguvu ya kiuchumi ya china hapa duniani wakidai Marekani ndo kila kitu.
Lakini jana baada ya kujibu mapigo kwa kuweka ushuru dhidi ya Marekani masoko ya hisa yaliporomoka kote ulimwenguni Marekani jana na leo tu masoko ya hisa yamepata hasara ya zaidi ya $6 trion na yanazidi kushuka hali yakuwa masoko ya hisa ndani ya china yako kawaida.
Hahaha,,,,kumbe??? Duh. Ni vema kama hujui uchumi tulia. Masoko ya hisia yanaashiria ukubwa wa China😂😂😂😂😂😂wabongo KIBOKO😂😂😂😂😂
 
Watakao umia ni raia wa Marekani maana watalazimika kununua bidhaa kwa bei kubwa.
 
Haya ww unaye jua tuambie.
 
Ila mwisho wa siku China lazima atapoteza kwani soko kubwa na la uhakika la Marekani kamwe hatabaki nalo kama ilivyokua na hatapata soko mbadala.
China ni kiwanda cha dunia huku kwetu Africa kila kitu made in china soko la dunia kwa bidhaa mchina anakimbiza hilo liko wazi kiuhalisia sioni kama mchina anacha kupoteza maana bidhaa nyingi za marekani huku hatuzitumii labda twitter na facebook na watsapp ndioninatumika kila siku lakini mchina yeboyebo za kuvaa mguuni ,kiatu ,nguo,peni ,bodaboda etc etc
 
Hii kauli mnairudia mara kwa mara nawaona kama maroboti.... Siku China ikichukua hatua anazochukua Trump dhidi ya mataifa yote, wewe na mimi tutalia na kusaga meno.
Hiyo jeuri hana na ni yeye atakayeumia zaidi ya atakaokuwa anawalenga.
 
Watakao umia ni raia wa Marekani maana watalazimika kununua bidhaa kwa bei kubwa.
Wanarejea kuwekeza nchini mwao na muda sio mrefu nchi kama China inayotegemea zaidi soko la Marekani uchumi utaporomoka vibaya.
 
Kuna watu humu walikuwa wanaichukulia poa nguvu ya kiuchumi ya china hapa duniani wakidai Marekani ndo kila kitu.
Lakini jana baada ya kujibu mapigo kwa kuweka ushuru dhidi ya Marekani masoko ya hisa yaliporomoka kote ulimwenguni Marekani jana na leo tu masoko ya hisa yamepata hasara ya zaidi ya $6 trion na yanazidi kushuka hali yakuwa masoko ya hisa ndani ya china yako kawaida.
Bado issue ya rare minerals. Tusubiri tuone timbwiri hilo.
 
Back
Top Bottom