Awe mkweli huyu jamaa anadai kuwa Dar kuna MALL 2 tu?
MLIMANI CITY
SHOPPERS PLAZA-Msasani
SHOPPERS PLAZA-Masaki
MAYFAIR PLAZA
SEACLIFF VILLAGE
QUALITY CENTRE
Bado nyingine ndogo ndogo...O'bay Shoping Centre,JM Mall,Tevi etc kingine kinachofanya WaTZ tusiwe na utaratibu wa ku-shop ni utitiri wa Boutique na Groceries stores zilizopo kila baada ya mita 10... Kampala,Lusaka,Nairobi,Kigali hakuna hilo pole zenu wa-Kenya...
Tanzania tunapiga hatua lakini bado hatujawa na shopping malls kubwa kihivyo. Pengine shopping habits zetu ni kikwazo na hata bei pia. Watu wengi sana wananunua vitu Kariakoo kwa imani (mara nyingi ni kweli) kuwa bei za bidhaa huko nafuu kuliko kwenye shopping malls. Na hapa tunarudi kwenye swali lile lile, rent ikiwa juu mwenye duka naye inabidi aingize hizo gharama kwenye bidhaa.
Kwa upande mwingine, hatuna mipango ya maana kabisa (hasa serikali kuu na local authority) kwenye upangaji wa biashara. tuna vikuka vidogo vidogo kila kona. Kwa nini wasifanye mipango itayowezesha biashara zikawa kwenye centers moja moja. Mfano, imarisha gerezani ili ijulikane ni eneo la spare parts, imarisha kitumbini ili iwe ni eneo la kanga, tenga eneo moja au hata mawili ili yatumike kama car-center.
Ukifuatilia mambo kwa karibua sana utagundua kuwa biashara zinapokuwa eneo moja, na kama mazingira ni mazuri (pubic transport, packing, na huduma zingine za kibinadamu) basi wateja wanakuwa wengi. Mteja angependa apate vitu au options nyingi akiwa sokoni na kwa kuweka biashara eneo moja unarahisisha hilo, pia utafanya watu wawe wabunifu ili wavutie wateja, i.e discount, quality, better packiging, better customer service. etc. Lakini huu mtindo wa kuwa na viduka vidogo vidogo scattered kila mahali ni tatizo.