Truworths, Identity and 4u2 to close shop in Tanzania over endless losses

Truworths, Identity and 4u2 to close shop in Tanzania over endless losses

Awe mkweli huyu jamaa anadai kuwa Dar kuna MALL 2 tu?
MLIMANI CITY
SHOPPERS PLAZA-Msasani
SHOPPERS PLAZA-Masaki
MAYFAIR PLAZA
SEACLIFF VILLAGE
QUALITY CENTRE
Bado nyingine ndogo ndogo...O'bay Shoping Centre,JM Mall,Tevi etc kingine kinachofanya WaTZ tusiwe na utaratibu wa ku-shop ni utitiri wa Boutique na Groceries stores zilizopo kila baada ya mita 10... Kampala,Lusaka,Nairobi,Kigali hakuna hilo pole zenu wa-Kenya...

Tanzania tunapiga hatua lakini bado hatujawa na shopping malls kubwa kihivyo. Pengine shopping habits zetu ni kikwazo na hata bei pia. Watu wengi sana wananunua vitu Kariakoo kwa imani (mara nyingi ni kweli) kuwa bei za bidhaa huko nafuu kuliko kwenye shopping malls. Na hapa tunarudi kwenye swali lile lile, rent ikiwa juu mwenye duka naye inabidi aingize hizo gharama kwenye bidhaa.

Kwa upande mwingine, hatuna mipango ya maana kabisa (hasa serikali kuu na local authority) kwenye upangaji wa biashara. tuna vikuka vidogo vidogo kila kona. Kwa nini wasifanye mipango itayowezesha biashara zikawa kwenye centers moja moja. Mfano, imarisha gerezani ili ijulikane ni eneo la spare parts, imarisha kitumbini ili iwe ni eneo la kanga, tenga eneo moja au hata mawili ili yatumike kama car-center.

Ukifuatilia mambo kwa karibua sana utagundua kuwa biashara zinapokuwa eneo moja, na kama mazingira ni mazuri (pubic transport, packing, na huduma zingine za kibinadamu) basi wateja wanakuwa wengi. Mteja angependa apate vitu au options nyingi akiwa sokoni na kwa kuweka biashara eneo moja unarahisisha hilo, pia utafanya watu wawe wabunifu ili wavutie wateja, i.e discount, quality, better packiging, better customer service. etc. Lakini huu mtindo wa kuwa na viduka vidogo vidogo scattered kila mahali ni tatizo.
 
Hizo reasons walizotitaja hususani rent ni kitu cha kuangalia sana.
Rent kwa tanzania ipo juu sana, hii inafanya garama ya uendeshaji iwe kubwa!

Vipi Rejo
hivi Hoja ya January kwa nini walipiga piga shaaa shaa wakati wangetulia haya yote wangeyajadili . Waliddhani hoja inawahusu Kina sisi wapangaji solo wa mbagala pekee kumbe hata makampuni makubwa.
 
Awe mkweli huyu jamaa anadai kuwa Dar kuna MALL 2 tu?
MLIMANI CITY
SHOPPERS PLAZA-Msasani
SHOPPERS PLAZA-Masaki
MAYFAIR PLAZA
SEACLIFF VILLAGE
QUALITY CENTRE
Bado nyingine ndogo ndogo...O'bay Shoping Centre,JM Mall,Tevi etc kingine kinachofanya WaTZ tusiwe na utaratibu wa ku-shop ni utitiri wa Boutique na Groceries stores zilizopo kila baada ya mita 10... Kampala,Lusaka,Nairobi,Kigali hakuna hilo pole zenu wa-Kenya...

Acha utani Bana ...kwa mtu yeyote ambaye amesafiri duniani hata hapo nairobi na kampala tu..utagundua hapa Tanzania Mall ziko mbili tu ..tena ndogo...Mlimani city na Quality center ....hayo mengine uliyoyataja sijui JM mall,Shoppers and the like are just shopping centers ...not mall in any available stAndards..

Watanzania wanaogopa ku shop kwenye shopping centers ..sembuse malls...tunapenda kushop kariakoo ...ili tu negotiate.....au vyakula tununue kwa mkopo dukani kwa mangi au mpemba.....tukienda mall tunaenda kushangaaa shangaaaaa.....
 
Hizo reasons walizotitaja hususani rent ni kitu cha kuangalia sana.
Rent kwa tanzania ipo juu sana, hii inafanya garama ya uendeshaji iwe kubwa!

Uko sahihi Rejao,
Lakini pia size ya middle class in Tanzania ni kitu cha kuangalia kwa mfanya biashara anayeilenga middle class. Wanaoweza kununua ndio haohao wenye uwezo kuruka kwenda shopping majuu. Pia UFISADI unaongezeka kisa mtu aweze kumudu maisha ya "watu wa middle class".

Middle class inayopata mapato halali ni ndogo mno.
 
Kwa mtu ambaye ulikuwa na tabia ya kushop truworths utagundua kuwa hawajaagiza nguo yoyote kwa kipindi kisichopungua miezi 18.
 
Tumezoea kufaa mitumba. Nguo ya Marks & Spencer, tunazipata nzuri na robo ya bei kwenye mitumba. Waache waende wakafanye biashara kwengine. Karume nitapata nikitakacho.
 
Pasco hapo umesema kweli, tuna vijiduka vyetu vya mtaani bei ni poa kabisa hakuna haja ya kwenda kwenye ma-mall watu wengi wa middle class huingia kwenye hivyo vijiduka vyetu.. Pia ukweli ni kwamba maisha hapa bongo yamepanda sana, sasa hivi ukiingia dukani au sokoni unachanganyikiwa na sijui miaka mitatu ijayo itakuwaje maana hakuna matazamio ya kurekebisha hali hii, leo asubuhi nimekwenda sokoni na mke wangu kwakweli tumechanganyikiwa sana maana nyanya 3 sh. 1,000/- , vitunguu nk usiseme hali ni mbaya, sasa sijui kwa hali hiyo kama wenzangu mnazo za ku-spend kwenye shopping bila utaratibu... haya ndio maisha bora kwa kila m-tz.
 
leo asubuhi nimekwenda sokoni na mke wangu kwakweli tumechanganyikiwa sana maana nyanya 3 sh. 1,000/- , vitunguu nk usiseme hali ni mbaya, sasa sijui kwa hali hiyo kama wenzangu mnazo za ku-spend kwenye shopping bila utaratibu... haya ndio maisha bora kwa kila m-tz.

Watanzania walichagua wenyewe hawakulazimishwa.Ukipenda boga shurti ulipende na ua lake.
 
Nimefuatilia mjadala kwa makini nakubaliana na pande zote. Kwanza labda nianza na wajibu wa serikali kwenye kodi za pango.

Serikali haitakiwi kupanga kodi ya pango kwa investors wa hizi mall na sector ya nyumba kwa ujumla lakini inatakiwa kuwa na sera dhabiti ya kudetermine kodi iweje, hapa serikali yenyewe inapoteza pesa nyingi sana ambazo ingeweza kupata kutokana na kodi za nyumba kama ingekuwa na sera ya kuregulate hizi kodi. Siku hizi vijana wengi wanapenda kukaa kwenye apartments kwenye prime areas badala ya wazee wetu waliotaka kujenga nyumba zao, hivyo basi serikali iandae sera madhubuti ya kuregulate hii sector ambayo mimi nasema ni sleeping giant na inaweza kufanya wonders kwenye uchumi wa nchi.

Kuhusu mtikisiko wa uchumi kutokana na Deacons kufunga, nafikiri retail mmoja impact yake ni ndogo lakini dalili za mvua ni mawingu tunapaswa kuchukua hatua in consideration real estate sector invyoshrink ulimwenguni na foreclasure, wakiuza yale majengo pale si kampuni zitahathirika hata serikali na taasisi zetu muhimu kama UDSM wataathirika kwa njia moja au nyingine

Target market, jamaa hawakufanya research yao kiasi cha kutosha kujua wataudumia watu wa aina gani, nmiddle class anayepata kati ya 1.5 na 500,000.00 TZS sio rahisi kununua nguo pale. Nilikwenda siku moja na mabinti wangu wawili, top ya mtoto wa miaka 5 nikauziwa 98,000.00 then on the same day nikaikuta Sinza Kijiweni kwa 18,000.00 same designer. This is weared walikosea hesabu zao lazima wafunge wajipange upya
 
Awe mkweli huyu jamaa anadai kuwa Dar kuna MALL 2 tu?
MLIMANI CITY
SHOPPERS PLAZA-Msasani
SHOPPERS PLAZA-Masaki
MAYFAIR PLAZA
SEACLIFF VILLAGE
QUALITY CENTRE
Bado nyingine ndogo ndogo...O'bay Shoping Centre,JM Mall,Tevi etc kingine kinachofanya WaTZ tusiwe na utaratibu wa ku-shop ni utitiri wa Boutique na Groceries stores zilizopo kila baada ya mita 10... Kampala,Lusaka,Nairobi,Kigali hakuna hilo pole zenu wa-Kenya...

Kweli ni 2 tu zile nyingine ni ndogo mno kuitwa mall. Hapa Tanzania ukiwa na duka dogo watu wanachagua vitu wanaita supermarket. Supermarket inakwenda na mita squares za shopping tuwe wakweli. Suala la kuanguka kwa middle class ni la kuliangalia kwa makini ndio wanaosukuma maendeleo ya taifa.
 
Tulizonazo sio Malls bali ni VIJI shopping centres

sasa Tazama hii kitu ndani Ya Nairobi

Westgate Mall Nairobi


photo7big.jpg



Entrance
photo1big.jpg





photo3big.jpg





Rift Valley Academy Students Choir Performing in the mall
Rift%20Valley%20Academy%20Choir%20perfoming%20at%20Westgatebig.jpg





INSIDE%20THE%20MALLbig.jpg





photo4big.jpg





photo2big.jpg





Nakumatt Westgate
nakumattbig.jpg





Barclays Premier
barclaysbig.jpg





Safaricom
safcombig.jpg





Zain
zainbig.jpg





Dormans Coffee
dormansbig.jpg





United Colours of Benetton
benettonbig.jpg





Nike
nikebig.jpg





Adidas
adidasbig.jpg





Numetro Cinema Store
numetrobig.jpg





Onami - Grill & Sushi bar
onamibig.jpg

onami




Casinos
casinobig.jpg


Dah,acha waende tu huko bana sie watu wa mitumba bado.
 
Ukitaka kujua kama Tanzania is a hopeless country

Hakuna mtu aliyefanya analysis kuwa hawa jamaaa wakiondona how much loss Taifa litaingia

Hakuna mtu aliyejaribu kukaa na hawa jamaa waka address matatizo wanayokabiliana nayo

and of course no one cares
 
Ukitaka kujua kama Tanzania is a hopeless country

Hakuna mtu aliyefanya analysis kuwa hawa jamaaa wakiondona how much loss Taifa litaingia

Hakuna mtu aliyejaribu kukaa na hawa jamaa waka address matatizo wanayokabiliana nayo

and of course no one cares

Inasikitisha sana mkuu.
 
Tatizo kubwa Tanzania ni kuwa hatuko serious kabisa

Kama huamini tazama standards za mijadala ya JF ndio utajua ukomo wa akili zetu

na hii inatokana na elimu tuliyopewa na makuzi tuliyokuwa nayo toka utotoni

Standards, accountability na entrepreneurship kwetu sisi ni mwiko

Hii ni kuanzia juu kwa wanasiasa mpaka chini

Kuna mtu aliznzisha thread Mary Nagu aondoke na mimi namuunga mkono
 
Jamani, inabidi ukweli hata kama unauma kwa sababu: [1] middle class ya Tanzania ni ndogo sana. Watumishi wangapi wa serikali wanaweza kuserve kiasi cha shilingi laki tano kwa mwezi? utawahesabu kwenye viganja vyako. wengi tunaishi kwa kubabaishi/kubangaiza na kutegemea posho hata kwa wabunge wetu. [2] Wenye pesa dar es salaam ni wahindi na waarabu. Hawa wenzetu wana mavazi yao maalum na ni nadra kuwaona huko kwenye malls zilizotajwa. Kodi za majengo n amasharti yake ni kama Waziri Tibaijuka alivyonena mjengoni, kwamba sekta ya ujenzi ni ndogo sana ikilinganishwa na mahitaji katika soko. Dawa yake ni kuwa na sera za makusudi za kujenga middle class kama mataifa ya Asia yalivyofanya miaka ya sitini hadi themanini. kupeleka shutuma kwa Gavana na Mabenki ni visingizio bila sera za kukuza middle class
 
Mkuu Tusker Baridi, hawa jamaa wameshindwa tuu kufanya biashara kwa sababu bei zao sio attractive kwa level ya middle class ya Tanzania japo nakubali ni kweli reantal fee ya nyumba ni kubwa, ukweli ni kuwa hao waiowatarget kama middle class kwa bei zao, wan ao aford sio middle class bali ni high class ambao wana access kupata kila kitu huko vinakotoka.

Mimi nina six kids, (3 girls na 3 boys) last December ile nyingine, nilitoka na family for X-mass shopping, nikaanzia W-Store pale mjini, nilipata vitu vya maana vya only small ones. Takaingia duka la pili lile la jeans za Levi Straus, ndio hili la hawa jamaa, kabinti kakapenda jeans, kuuliza bei naambiwa TZS 138,000, binti anang'ang'ania kuwa etiu ni fashion ya sasa iliyotoka na mama yao akasupport, Kaka yake na dada yake ambao ni ma teenager, wakashauri "Dada kama ....anaitaka jeans hiyo, nipe 50,000 tuu nikamnunulie mahali!. Kusema ukweli tulitoka bila kununua chochote humo ndani!.

Maadam wale wawili wadogo wameshapata nguo, wale wawili wakubwa wakaomba wapewe pesa wao na waende na wadogo za "mahali" wakawanunulie nguo. Niliwapa, japo concern ya mama yao, wasije wakatinga Kariokoo kutuzolea mchina, my boy akasema no, mchina tunamjua, wee leta pesa tunakuja na nguo za ukweli!. Kilichofua walirudi na nguo za ukweli za level ile ile ya maduka makubwa!. Ndipo wakasema kuna viduka tuu mitaa vinaleta nguo za ukweli na bei ni poa!. Kama ni hivyo, nani aende Mlimani city akachinjwe?. Acha wajiondokee tuu nao walikuwa wanatukamua sana!.

Umelenga kwenye tatizo lakini umeliangalia kimakosa nadhani kwa vile ulifaidika. Ukweli ni kwamba kufanya biashara halali Tanzania ni kitu kigumu sana, hizi multinational mara nyingi zinafuata sheria zote za nchi ili kutoharibu brandname yao ikitokea scandal.
Hapo "mahali" waliponunua hizo nguo utakuta yafuatayo.
a) Hawalipi kodi
b) Hawawalipi wafanyakazi mishahara inayotakiwa kisheria
c) Wana bidhaa feki (knockoffs) hata kama ni feki ambayo sio rahisi kugundua.

Kwa hiyo hizo ni artificially low prices, hazilingani na gharama halisi ya kufanya biashara TZ.
 
watanzania tuna matatizo mengi sana na mfumo wetu wa kufanya biashara siyo mzuri hillo halina ubishi. Wenzetu wa Kenya wanapenda kufanya mambo yao kwa staili ya kimagharibi zaidi kitu ambacho watanzania wengi hakijaingia sana, kuwa na malls kubwa siyo dalili ya maendeleo , watanzania tutafaidika kwenye hili jambo biashara ya malls ,brick and mortar ni mambo ya kizamani hata US zilikozaliwa malls zinafungwa kwa sababu ya competition kutoka internet outlets. Kwa nchi yetu ambayo ni asilimia 14 tu ya watu wana umeme ni upumbavu kutumia nishati kubwa kwenye malls kuuza t-shirts zinazoworth $10 or less,
 
Back
Top Bottom