Try Again arejeshwa Simba, aunda Baraza jipya la Wadhamini lililopitishwa na Wanachama Bunju

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Klabu ya Simba SC imepitisha Baraza jipya la Wadhamini baada ya wanachama kulidhinisha katika Mkutano Mkuu wa Dharura uliofanyika leo, Agosti 2, 2026, Bunju jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa, Mwenyekiti wa Klabu hiyo alipendekeza jina la Salim Abdallah Muhene maarufu kama Try Again.

1785677251798.png

Wajumbe waliopitishwa katika Baraza jipya la Wadhamini ni Salim Abdallah Muhene, Dkt. Bill Kiwia, Alhaj Ismail Mohamed, Amos Makalla, Adam Mgoi, Hamad Abdallah na Hassan Hassan (Hassanoh).

Soma: Salim Abdallah 'Try Again' ajiuzulu uenyekiti bodi ya wakurugenzi Simba

Kwa mujibu wa Katiba ya klabu, mwanachama yeyote asiyeridhishwa na mapendekezo ya wajumbe anaweza kuwasilisha pingamizi lake kwa njia ya barua ili lifanyiwe tathmini kwa utaratibu uliowekwa.
 
Inamaana simba haina vijana hao kina makala bado wana mawazo ya ki ccm ccm hawataki ushindan wala mabadiliko wanaamini kwenye kutumia uongo,nguvu,vitisho
 
shabikia tu njombe mji inatosha mkuu
 
Pale Simba Kuna kakikundi cha wahuni Kanacho shirikiana na Yanga Kuivuruga Timu yetu.

Hii miaka 5 kilichoipa yanga Ubingwa ni Wahuni wa ndani ya Simba. Wanao ihujumu Timu.
 
Klabu ya Simba SC imepitisha Baraza jipya la Wadhamini baada ya wanachama kulidhinisha katika Mkutano Mkuu wa Dharura uliofanyika leo, Agosti 2, 2026, Bunju jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa, Mwenyekiti wa Klabu hiyo alipendekeza jina la Salim Abdallah Muhene maarufu kama Try Again.

Wajumbe waliopitishwa katika Baraza jipya la Wadhamini ni Salim Abdallah Muhene, Dkt. Bill Kiwia, Alhaj Ismail Mohamed, Amos Makalla, Adam Mgoi, Hamad Abdallah na Hassan Hassan (Hassanoh).

Soma: Salim Abdallah 'Try Again' ajiuzulu uenyekiti bodi ya wakurugenzi Simba

Kwa mujibu wa Katiba ya klabu, mwanachama yeyote asiyeridhishwa na mapendekezo ya wajumbe anaweza kuwasilisha pingamizi lake kwa njia ya barua ili lifanyiwe tathmini kwa utaratibu uliowekwa.
Hiki kikao ni batili. Kikao halali kinataka kesho chini ya Mwenyekiti wa Bodi Crecentius Magori.
 
Pale Simba Kuna kakikundi cha wahuni Kanacho shirikiana na Yanga Kuivuruga Timu yetu.

Hii miaka 5 kilichoipa yanga Ubingwa ni Wahuni wa ndani ya Simba. Wanao ihujumu Timu.
kwa hiyo Yanga ili ichukue ubingwa ni mpaka simba ihujumiane yenyewe kwa yenyewe? ukiona umezidiwa kaa chini,tafakari,jipange amka na nguvu mpya.
 
CCM ndani VIA makalla.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Back
Top Bottom