Tsh milioni 60 shwaaa zikapotea!

Tsh milioni 60 shwaaa zikapotea!

Story yako umetia chumvi japo lengo la kutia chumvi linajulikana

Nov. 2018 serikali ndio ilitangaza kununua korosho ( mpaka sasa miaka minne tu imepita) ila wewe umeshakaa miaka 7
Umeniwahi ndg,nami nilitaka nimuulize mtoa mada hili swali
 
Mbona chai ya moto sana!
Sukari imekolea sana hadi imepoteza ladha halisi ya chai [emoji16]
JamiiForums561838404.jpg
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nimecheka sana. Hii sio chai mzee ni true story kwenye utafutaji kuna kupoteza pia. Unapotafuta parefu na kupoteza ni parefu pia. High Risk, High Return na kupoteza ni hivyo hivyo.
Biashara ni kipaji sawa na hekima au upumbavu ndiyomaana elimu ya darasani haijawahi kuwa sahawia katika mipango, mbinu, utekelezaji, usimamizi na upataji wa faida.
 
Story yako umetia chumvi japo lengo la kutia chumvi linajulikana

Nov. 2018 serikali ndio ilitangaza kununua korosho ( mpaka sasa miaka minne tu imepita) ila wewe umeshakaa miaka 7
Kwa hiyo jamaa katupiga kamba ndeeeefu sana😆😂
 
Story yako umetia chumvi japo lengo la kutia chumvi linajulikana

Nov. 2018 serikali ndio ilitangaza kununua korosho ( mpaka sasa miaka minne tu imepita) ila wewe umeshakaa miaka 7
Hili ndio limenishtua
 
2017 hapo nikiwa bado nipo chuo na penzi limekolea kwa mpenzi wa Maisha yangu. Ananipa mtaji wa sh laki 1 na 50 nikanunua dagaa Nyasa wale ili niwe nauza Dar.

Kabla ya hiyo biashara nilishafanya biashara kama kuuza sabuni na yebo yebo nilikua napeleka Masasi na Mwanangu James Ila akaja nidhulumu nikapotezea.

Basi bwana kwenye Maisha yangu sikuwahi kuwaona dagaa nyasa hapo kabla so Mara ya kwanza nikawaona nilipoenda songea nikawapenda.. Hivyo nikamuomba mchumba anisaidie mtaji ili niwalete Dar niuze kweli nikachukua sampuli dumila 10 nikaja nao dar kisha nikaenda kwenye magenge makubwa yale kuwapelekea wengi walikataa ikabidi niwape bure kisha wauze kama watanunulika basi tufanye biashara hapo baadae bado walikataa[emoji16] Ila magenge manne yakakubali nikaacha na namba za simu basi hazikuzidi siku 3 nikapigiwa simu tukaongee.

Basi bila hiyana nikajivuta tukakubaliana niwe napeleka mzigo nawaachia wanauza ukiisha Nafuata pesa.. Aisee nakiri wazi Moja Kati ya biashara ambayo siwezi isahau ni ile ilikubali nikawa napata mshiko wa maana(kiuanafunzi) Maisha yakabadilika japo mwanafunzi kusafiri Mara kwa Mara nikichukua mzigo wa laki 2 faida laki 2 ikaja mpaka Kule nilipokua nanunua wakawa wananipa mzigo kwa Mali kauli kutoka na mzunguko mkubwa.kufipisha stori niliweza kumiliki 3M+ bank zilizotokana na biashara ile nikiwa mwanafunzi na pikipiki(bodaboda) pia geto Kali Lakini vilipotea ndani ya wiki Moja tu baada ya kutapeliwa kwa mtu niliyemuamini kupita kiasi.

Shukrani kwa brother wangu alinihifadhi kwake na kunifariji maana ningejitundika kwa mawazo ule mwaka 2018 nilipoteza kila kitu mwishowe hata shule ningepoteza. Nilikuja kuinuka tena 2019 mwishoni Ila nikaja kupigwa na kitu kizito kwa uchawi qmmake ile unapika chakula Asubuhi mchana kimechacha Maisha ni Vita.
 
Starehe mnazipenda ila mwisho wake MBAYA. Wengi wameteketea kwa kuendekeza UMALAYA.

Ishi vizuri, kula vizuri, fanya mazoezi na umrudie Muumba wako.

___________________________________________________________

Nikiwa na miaka 24 pindi tu baada ya kuhitimu elimu yangu ya chuo kikuu niliingia mtaani, akilini na moyoni nikiwa na hari ya kuanzisha kampuni yangu. Ndoto niliyokuwa nayo tokea naingia form 3 ambapo niliacha masomo ya sayansi na kufwata kile moyo ulichoniambia KUWA MFANYABIASHARA MKUBWA.

Basi bana mwaka wa kwanza ukaisha nipo kitaa, moja haisimami mbili haikaii. Mwaka uliofwata nikiwa mtaani, nikaaanda mpango wangu biashara (ambao kwa sasa nikiusoma naona makosa mengi sana) nikaongea na wadau wawili watatu kupata mtaji wa biashara. Mungu si athumani wala hadija nikafanikiw kupata mtaji wa shillings 60,000,000.

Nikaingia kwenye biashara ya ununuzi (ulanguaji al-maarufu KANG'OMBA) korosho huko Mtwara wilaya ya Masasi. Simu wa kwanza mambo yalienda vizuri hela ilirudi. Nikaamua kwenda Uganda kufanya utafiti biashara ya mchele kule sasa mambo ndipo yaliponiendea kidogo kombo maana nilianza kupoteza taratibu pesa.

Long story short, nilikuja kupoteza pesa Million 60 shwwaaaaaa zikapotea zoootee kwenye korosho pale mzee baba (sijui huko alipo ni kiongozi wa malaika au anapigwa kama ngoma) aliposema serikali inaubavu wa kununua korosho (nyooo walijuta kilichowakuta).

Nilikaa kitaa miaka 7 sina uelekeo zaidi ya kuwa chawa kwa mwanangu wa ukwelii. Ila nilichojifunza ukianguka chukua muda kunyanyuka angalia mazingira ulipodondokea ukiwa bado chini, yatathmini mazingira husika kisha ndio unyanyuke.

IMEKUWA MAUMIVU MAZITO ILA AKILI YA KUYASHINDA NILIJAALIWA NA MUNGU.
Boss 2018 Jiwe ndo alianza kununua korosho ukipiga hesabu ni miaka 4 imepita mpaka sasa.
 
Ukiwa muongo uwe na kumbukumbu...unasema ulikaa kitaa miaka 7 while issue ya Mzee baba nakorosho ni ya Nov 2018-2019 ht miaka mi4 haijatimia..
 
Kama kuna sehemu imekufunza au kukufurahisha basi hilo ndilo unatakiwa kuondoka nalo hapa. Kuhusu accuracy ya taarifa hilo mniachie mwenyewe maana nyie halitawasaidia kwa chochote.

Nilichokiandika nakijua na ninaelewa kwanini nimeandika hivyo.

Comment nyingi mnasema nadanganya, JE TULIKUWA WOTE?? Kama haukuwa na mimi MANGAKA kwenye kufaulisha KOROSHO za dili usiseme ni UONGO.

Soma kisha pita kule, kama kuna la kujifunza jifunze.
 
Nilitaka nisone tu comment. Acha nicomment na mimi…

WEWE NI MUONGO
 
Back
Top Bottom