Lupweko
JF-Expert Member
- Mar 26, 2009
- 23,566
- 24,891
Kitendo cha Tshabalala kuongeza mkataba wa kuitumikia Simba SC bila kumshirikisha meneja wake, Henry Mzozo, hakuna namna nyingine ya kukielezea zaidi ya kusema ni udhalilishaji wa hali ya juu wa mchezaji kwa meneja huyo.
Mzozo katika siku za hivi karibuni amekuwa akizungumza katika vyombo vya habari kwa ujasiri mkubwa kwamba safari hii hakuna chaguo la 'mchezaji wake' kusalia Simba, na kwamba uamuzi walioufikia ni kuondoka kabisa Simba hata kama ikibidi kwenda Gwambina, kwa kile alichoeleza kuwa ilikuwa mchezaji huyo asisaini Simba hata kipindi cha miaka miwili iliyopita ila waliivumilia tu, lakini safari hii hawatasaini kabisa.
Kabla hata masaa 24 hayajapita, taarifa ya maandishi, picha na video ikatolewa katika mitandao rasmi ya kijamii ya klabu ya Simba zikimuonyesha na kumnukuu Tshabalala akikiri kusaini mkataba mpya na klabu hiyo, tena bila ya uwepo wa 'meneja wake' ambaye amekuwa akimpamba mchezaji huyo katika vyombo vya habari
Jambo hilo mimi binafsi nimelitafsiri kama ni dharau na udhalilishaji wa mchezaji kwa meneja wake, na hivyo kuwafanya baadhi ya watu waliokuwa wakifuatilia sakata hili, kufanya dhihaka na kejeli kwa meneja huyo pamoja na waliokuwa wakimuunga mkono, hasa baadhi ya wachambuzi wa soka la Tanzania
Tshabalala asiishie hapo, amuombe radhi meneja wake, na pia asimsahau moja kwa moja hasa kwa mgao walau kidogo wa dau alilotengewa na Simba