Habari wakuu,
Nadhani imefikia pahala Simba haina budi kutafuta suluhisho za beki hizi kongwe zitokazo pembeni.
Hii kutokana na kuchoka kimwili mpaka kiakili haswa linapokuja suala la maamuzi ya haraka na ukabaji kwa ufasaha kama walivyokuwa awali.
Tshabalala anashindwa win wipira mingi sana akikaba, na pia amekuwa mwepesi wa kupoteza mipira jambo ambalo linacost team kwa kiasi kikubwa sana.
Kapombe kwa sasa hana uwezo wa kufanya marking kabisa. Amekuwa uchochoro kwa washambuliaji na pia pale anapokuwa na mipira haswa huwaza zaidi kutoa krosi zaidi ya hapo hana mbinu nyingine mbadala. Pia amekuwa mzito kupandisha mashambulizi kwenye upinzani.
Me naona ni muda muafaka sasa kuwapumzisha maveterani hawa kwa upande wetu, kwani tayari wamekwisha choka na wanashindwa kuendana na kasi ya club katika kutafuta matokeo.
Zaidi ya hayo, tunawaheshimu na tunathamini mchango wao.