TOKA MAKTAB:
04 December 2024
Benguela, Angola
Makamu wa Rais wa Tanzania Dr. Philip Isdori Mpango kumuwakilisha rais Samia Hassan, uzinduzi Lobito Corridor Angola
View attachment 3247293
Dr. Philip Isidori Mpango amewasili Benguela nchini Angola kumuwakilisha rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Dr. Samia Suluhu Hassan katika uzinduzi wa mradi wa Lobito Corridor ambao marais Joe Biden wa Marekani, rais wa Angola waheshimiwa João Manuel Gonçalves Lourenço , Rais Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DR Congo, Rais Hakainde Hichilemawa Zambia wote watakuwepo katika hafla hiyo inayofuatiliwa na ni gumzo ulimwenguni kote kuhusu uwekezaji mkubwa wa Marekani kuipiku China katika eneo hili la bara la Afrika.
Leo tarehe 04 December 2024 Rais Biden atakwenda Lobito, Angola kwa Mkutano wa Kilele kuhusu uwekezaji wa miundombinu katika eneo hilo la ukanda / ushoroba wa Lobito Corridor na viongozi kutoka Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Tanzania na Zambia.
View: https://m.youtube.com/watch?v=SS1DCxUVW1g
Mradi wa reli ya Lobito corridor utakavyokatiza, utakaofaidika na mapesa matrilioni ya shilingi za kitanzania ambazo zimetangazwa na kuhakikishiwa wakati wa a ziara ya rais Joe Biden nchi ya Angola, na pia mbali ya rais wa Angola pia watakuwepo viongozi wa DR Congo, Tanzania na Zambia wakati wa uzinduzi wa mradi huo leo .
View attachment 3247294
Mradi reli wa Lobito Corridor