INAUZWA Tshirt printer inauzwa - Heat press machine heavy duty

No powder dtf hiyo sijaijua kaka.. dtf hatari sana ila tatizo spares na white
DTF Technology mpya hiyo.
No powder DTF ni technology mpya McCloud technology kampuni ya kimarekani wamezindua week iliyopita.

Wenyewe wamekuja na special pre-treated DTF ink.

Changamoto kubwa ya DTF ni ink clogging hasa ile White ink. Inahitajika kutumika mara kwa mara au na kile kifaa cha kusafishia ambacho sasa itasababisha head isidumu.

Pia unaweza tumia Epson l1800 au 800 serious na Epson nyingine nyingi.

Ila hizo nilizotangulia kuzi mention kidogo speed sio nzuri sana, naweza recommend kutumia Epson xp15000 ambayo ipo vizuri.

Changamoto nyingine ni icc profile za hizi printer maana what you see on screen inaweza toka tofauti.

Ila hao FUNSUN WAPO VIZURI KWENYE MACHINE ZAO.

Kiujumla ni technology mpya hii.
 
Nimekupata mkuu, na kama nikiwa na heatpress, laptop na printer hizi za epson zinazouzwa 200k to 1m haitafaa?? I mean badala ya kwenda kwa watu wenye mashine kama hizo.
 
Nimekupata mkuu, na kama nikiwa na heatpress, laptop na printer hizi za epson zinazouzwa 200k to 1m haitafaa?? I mean badala ya kwenda kwa watu wenye mashine kama hizo.

Zinafaa. Wengi ndio wanatumia epson ulizotaja. Hii mashine kubwa ni style ya kisasa ambayo inapendezesha dark tshirts zaidi.

Hii mashine kubwa ni modern technology ndio maana tunaitumia pia.. ila hata epson tunatumia sana miaka na miaka
 
inkjet ya kawaida moja unaweka kwa ajili ya sublimation( sublimation ink) nyingine kawaida kwaajili ya transfer paper (dye ink)
sijakuelewa mkuu sublimatiion ink/ dye ink ni wino wa kawaida kama wino hizi zingine za printa za kawaida au zikoje zenyewe?
 
sijakuelewa mkuu sublimatiion ink/ dye ink ni wino wa kawaida kama wino hizi zingine za printa za kawaida au zikoje zenyewe?
-Kwa inkjet kuna sublimation, dye na pigment ink. Ingawa siku hizi hadi wa solvent tunatumia lakini kuna issue chache za kudeal nazo unapo tumia solvent ink.

-Kwa large format kuna sublimation na solvent ink.

So sublimation ink ni wino unaojitegemea ambao ni special kwaajili ya kutransfer image to items kama t-shirt, vikombe, chupa, picha za frame n.k.
 
asante sana kunielezea kwa mapana mmaana nilikuwa sifahamu mm natengeneza batik na wino wa batik dye ink sasa imenichanganya kidogo asante kunifafanulia
 
asante sana kunielezea kwa mapana mmaana nilikuwa sifahamu mm natengeneza batik na wino wa batik dye ink sasa imenichanganya kidogo asante kunifafanulia
Tupo pamoja.
Hii sublimation ndio inatumika hata kwenye viwanda vya textile.
Unaprint artwork kwenye sublimation paper kwa kutumia sublimation printer then una transfer kwa heatpress au electric iron/pasi.
 
ukiwa na printer za kawaida kama za hp, laserjet au epson huwezi kutumia kwenye sublimation paper?
 
Lazima printer uibadilishe itumie sublimation ink au toner then unatumia pamoja na hizo sublimation paper
ok na je printa zake zinapatikana hapa au mpk uagize nje na zinaitwaje?
 
ok na je printa zake zinapatikana hapa au mpk uagize nje na zinaitwaje?
Epson hizi hizi ikiwa mpya hujaweka wino, nunua ule wa sublimation ndio utumie kisha itakuwa tayari kwa matumizi. Hapo itakubidi ununue sublimation transfer paper ambazo zipo za dark na light.

Kisha unaweza print. Unapo print lazima image uprint in mirrored mode.

Then uta transfer image kwa heatpress sehemu unayotaka uiweke kama ni t-shirt, au mugs nk
 
Kama ni used imetumika na wino mwingine inatakiwa ink tank system (head hadi nozzle zile) zisafishwe then ujaze wino wa sublimation.

Ukienda kwa wanao repair watasafisha. Kama haujui peleka huko.
 
Mimi nauza heat press pamoja na vifaa vyote vya kuprintia mug, kofia na sahani za size ndogo na kubwa pamoja na Epson L3111 vyote kwa Tshs laki saba (700,000/=). Nina hitaji muhimu sana nataka pesa.

Pamoja na hivyo, nakupatia baking paper maalum kwa ajili ya kufanyia transfer kwenye material unayoprint.

Nahitaji pesa by kesho.
 
Mkuu kuna transfer paper za sh 130,000 Hadi 160,000 ,Sasa mhusika faida atapata vipi?, Maana t-shirt wanaprint kwa bei isiyozidi 5000,na karatasi zimo 100,bado wino,

Transfer paper Mimi najua ni sh 15,000 elfu zimo 100,au Ni fake
 
Mkuu Namba na herufi zinauzwa wapi na kwa bei gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…