TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Heri ya sikukuu ya Pasaka Piga *148*30# au*150*71# au *148*30*35# ufurahie vifurushi vya DATA, SMS, UNI na BANDO TAM TAM vilivyoboreshwa kama ilivyokuwa awali.....
T - pesa ni changamoto unajikuta unatoa hela ukiweka namba ya siri inaandika time out ukipiga huduma kwa wateja unaambiwa muamala hujaenda unaambiwa toa tena napo inakua vile vile mwisho wasiku unaamua kuhailisha ndo unaona text zinakuja nyingi za miamala uliyo fanya unajikuta umetoa pesa zaidi ya mara tano ukiwapigia huduma kwa wateja wanajibu hovyo tu.

Au unatoa pesa message ya uthibitisho inakuja lakin kwa wakala haijaja kwahyo anashindwa kukupa pesa mpaka usubilie kwakwel INAUMIZA sana yaani ukitoa pesa Ttcl mpaka ije itoke ni zaidi ya dakika 45
 
Mbona kwenye menu ya *150*71# huduma ya tam tam plus hamjarudisha?
 
Kasulu Kigoma network ya laini zenu inasumbua sijui kwa nini, boresheni huduma ya speed ya iternet angalau isome 4G
 
T - pesa ni changamoto unajikuta unatoa hela ukiweka namba ya siri inaandika time out ukipiga huduma kwa wateja unaambiwa muamala hujaenda unaambiwa toa tena napo inakua vile vile mwisho wasiku unaamua kuhailisha ndo unaona....
Aisee leo nmenunua Luku mara tatu inakataa..... Eeh bhana eeh baada ya nusu saa zinakuja token tatu tofauti.

Hawa jamaa hawapo kibiashara kabisa.... Customer care yenyewe wanapokea baada ya lisaa
 
Bando tam lililokuwa linanunuliwa kupitia Tpesa (sh.1000: 1.2 gb na dk. 10 mitandao yote kwa siku 5) iko wapi?
 
TTCL Customer Care asante Sana kwa bando la #Bandik Bandua....speed kali Sana usiku hamuweki gavana...mwendo wa kudownload kwa speed kama mwanzo!
 
TTCL mpo vzr sana ila jaribuni kusambaza huduma zenu kama vile vocha na minara mikoa yote na kuiboresha kama ilivyo kwa Dar es Saalam ili internet zenu na mawasiliano yasambae vzr zaid ktk mikoa yote TZ na kuteka soko vzr zaidi, tumewachoka Vodacom kwani wamekuwa viburi sana.
 
Inasumbua mkuu, "bando tam" lililokuwa linanunuliwa na Tpesa (sh. 1000 gb 1.2gb na dk 10 mitandao yote kwa siku 5 wamelifuta...hahaha kampuni ya umma inafanya kazi kwa kuwaiga kampuni binafsi! Aibu!
Mbona limesharudishwa mkuu
 
mbona mumeanza kuwa wezi. nilijiunga na kifurushi wiki iliopita, hela imekatwa na nikapata msg kuwa nimeunganishwa wakati si kweli. nimepiga simu customer care wakasema kuna tatizo nitarudishiwa kifurushi changu nadni ya masaa 24. cha ajabu wili ya 2 sasa na nilishakata tamaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…