TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Tunapenda kuomba radhi wateja wetu kwa usumbufu uliojitokeza kutokana na kukatika katika mara kwa mara kwa huduma zetu za mawasiliano na T PESA siku ya tarehe 06/04/2021.

Hali hii imetokana na zoezi la kuboresha mtandao wa TTCL upande wa huduma ya T PESA ambalo tulikuwa tunalifanya jana na ambalo tumelikamilisha kwa ufanisi.

Lengo la maboresho haya ni kuendelea kukupa we we mteja wetu huduma za viwango vya juu unavyostahili.

Wazee mpo nyuma sana sijui kinawakwamisha kitu gani na nyinyi ndio mkonge wa taifa nyinyi wa kushindwa na simba net au raha au Aptus au Tigo au Airtel kweli kwenye huduama zenu sijui mnashindana na nani Kwa kweli
 
Hebu nyie ttcl onyeshen ukomavu na muwe na ubunifu

Kuna kifurushi cha data cha 1.2gb mnatoa kwa siku 5 hebu hicho kifurushi cha siku 5 kipeleken siku 7 muone kama watu hawajaja kwenu

Halotel wanawapiga bao kwenye data hasa sh 1000 kwa gb 1 kwa wiki

Hebu njoen na kitu tofaut kitakachowaleta watu kwenu na ongezen ubunifu zaid na sio kama hiv mnavoenda
 
1 GB kwa 2, 000/= in 7days maana yake nini? Kwamba mko ndani ya agizo la mkuu wa nchi au nje ya agizo hilo?
 
Hivi nyie watu mna wafanyakazi wengi sana au?
Maana sijui tatizo lenu nini?
Adi mnazingua kiasi hicho?
 
Back
Top Bottom