TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Wazee mpo nyuma sana sijui kinawakwamisha kitu gani na nyinyi ndio mkonge wa taifa nyinyi wa kushindwa na simba net au raha au Aptus au Tigo au Airtel kweli kwenye huduama zenu sijui mnashindana na nani Kwa kweli
 
Hebu nyie ttcl onyeshen ukomavu na muwe na ubunifu

Kuna kifurushi cha data cha 1.2gb mnatoa kwa siku 5 hebu hicho kifurushi cha siku 5 kipeleken siku 7 muone kama watu hawajaja kwenu

Halotel wanawapiga bao kwenye data hasa sh 1000 kwa gb 1 kwa wiki

Hebu njoen na kitu tofaut kitakachowaleta watu kwenu na ongezen ubunifu zaid na sio kama hiv mnavoenda
 
Mlitoa taarifa ilivyopotea? Yaani mnaudhi sasa.
 
1 GB kwa 2, 000/= in 7days maana yake nini? Kwamba mko ndani ya agizo la mkuu wa nchi au nje ya agizo hilo?
 
Hivi nyie watu mna wafanyakazi wengi sana au?
Maana sijui tatizo lenu nini?
Adi mnazingua kiasi hicho?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…