TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

nahitaji kuvuta ttcl kebo ili kupata huduma za internet katika ofisi yangu napataje hiyo huduma na ni kwa gharama gani
 
nahitaji kuvuta ttcl kebo ili kupata huduma za internet katika ofisi yangu napataje hiyo huduma na ni kwa gharama gani
Habari za mchana
Tuna huduma za aina mbili za cable, Copper na fiber, kuweza kuunganishwa na huduma hizi, inabidi kwanza tujue Ofisi yako ipo mkoa gani? eneo lipi? hii itatusaidia kujua kama hii huduma eneo ulilopo linapatikana, ili tuweze kukupa maelekezo sahihi ya kuweza kupata huduma hizi
 
nahitaji copper an how much is fiber mi nko mkoani tanga wilaya ya muheza actualy
 
nahitaji copper an how much is fiber mi nko mkoani tanga wilaya ya muheza actualy
Ndugu mteja, Fika duka la TTCL hapo Muheza kwa msaada zaidi kwani utapatiwa surveyor ambae atafika kwako kuangalia kama line yetu imefika au atakupa ushauli mbadala.
 
Ndugu mteja, Fika duka la TTCL hapo Muheza kwa msaada zaidi kwani utapatiwa surveyor ambae atafika kwako kuangalia kama line yetu imefika au atakupa ushauli mbadala.
Naomba kujua namna ya kutoa fedha kutoka kwenye Wakala Wallet (ile inayopokea commission), kwenda Wallet ya kuhudumia wateja.
 
Naomba kujua namna ya kutoa fedha kutoka kwenye Wakala Wallet (ile inayopokea commission), kwenda Wallet ya kuhudumia wateja.
*150*71# OK Kisha namba 7, kisha namba 2, kisha 1 mwisho 3, kiasi namba ya siri
 
Nasikitika sana kuona TTCL mpo nyuma ya wakati sana.

Watanzania wanashindwa kupokea hela kupitia Paypal na Skrill kwa muda mrefu sasa huku majirani zetu SafaricomKenya wakitoa huduma hiyo, na hii inawafanya watu watumie line za simu za Kenya na kufaidisha nchi nyingine. Je hamuoni kwamba hiyo kwenu ni fursa ya kuingiza kipato huku mkiinua uchumi wa nchi na wananchi?
 
Wamekalia kuuza MB ghali wao ndio wanaona ndio chanzo rahisi cha mapato
 
Twenzetu kwa Mkapa, tukashuhudie mechi Simba vs Yanga.
Pata tiketi yako mapema kupitia T-PESA
#SalamanaNafuu
#RudiNyumbaniKumenogaView attachment 1777203
Hivi nyie mko serious kweli? Mnaulizwa na kupewa maoni hata kujitutumua kujibu tu mmenyamaza. Mtaweza kweli ushindani na akina Tigo na Voda na wengine?
Pathetic kabisa. Utakuta hii account ni ya kaji sister do flani Kako hapo kupitia undugunization hakajui A wala B. Shwaini kabisa. you guys forget about taking over the market if you continue with this mentality.
 
Sawa mlituhimiza tununue, tiketi tukanunua!
Sasa game ndio hivyo tena imeyeyuka! Hela zetu mnaturudishia ama na zenyewe zimeyeyuka? Tunaomba jibu tafadhali, msikalie kimya hapa!
mkuu mbona tena umeni quote mimi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…