TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Kwa nini namba zenu zinatumika Sana na matapeli wanaotuma jumbe za tuma pesa kwenye namba hii?
Huyo Tapeli ni mmoja tu, ametumia kitambulisho kimoja kwa line zaidi ya Mia moja. Maana siku moja nilifuatilia nikakuta namba zake zingine TTCL wameziblock tayari hazitumiki. Zilikuwa namba kama 15 hivi zilizo kuwa blocked.

Tatizo la TTCL ni urasimu. Ukipeleka shida kama hiyo ya kupokea sms za kitapeli mchakato wao wa ndani wa kuiblock hiyo namba unapita kwa watu kama wanne au watano ndipo mtu wa mwisho anapewa order ya kuizima hiyo line.

Laiti kama ingekuwa ukienda na sms tu ya kitapeli halafu Customer Service Officer aka confirm ni ujumbe wa kitapeli akafanya Uamuzi hapo hapo ingekuwa hizi sms tumezipunguza sana
 
Nunua tiketi yako kwa T PESA leo ushuhudie tamasha la TTCLNandy Festival
Wapi: Uwanja wa Jamhuri Dodoma
Tarehe: 26 Juni 2021
Utapata burudani ya kufa mtu kutoka kwa wasanii mbalimbali kama vile
👉Nandy
👉Mabantu
👉Mr. Blue
👉Marioo
👉Professor Jay
👉Rosa Ree
👉Shilole
👉Meja Kunta
👉Wini
👉Tanasha Dona
👉Linah
👉Moni Centrazone
👉Ben Pol
👉G Nako
👉Joh Makini
#RudiNyumbaniKumenoga
#Watakaatu
#TPESA

 
Ttcl mpo? Mnadai nyumbani kumenoga turudi lakini tukirudi mambo nitofauti kabisa.Sehemu nyingi huduma zenu ni duni kabisa.mtandao haupatikani,hebu nenda arusha,hapo olasiti tu ni mjini kabisa lakini hamna kitu.Hili ni shirika la uma fanyeni kitu tuwaunge mkono ni shirika letu hili,mnakwama wapi?
 
Huwa nasikitika sana nikiiona TTCL inafanya mambo kama simba mzee. Enzi hizo posta na simu ilikuwa kampuni kubwa sana ikimiliki miundo mbinu ya posta na mawasiliano ya simu. Nilitegemea TTCL awe na ndio namba 1 kwa huduma ya mtandao ulio na kasi zaidi kuliko kampuni yoyote na pia POSTA awe ndio BANK kubwa nchini inayotumia Sci, techn na Innov wakati wengine wangekuwa wanafuata kwa mbali . Lakini TTCL ndio wamekuwa mkia katika technologia na innovation ktk mtandao. Nifahamisheni mtazinduka lini?
 
Mbona hujasema hasa TTCL inakuwa Mkia kwenye eneo lipi mkuu?
 
Kwenye spidi ya internet, aina ya vifurushi na muda vinapotolewa, T-pesa upatikanaji, coverage ya mtandao na mengine mengi soma kwa wenzangu. Nilidhani mgekwenda hadi vijijini mwisho, ikiwezekana hata mtu akiwa porini , mbungani mtusaidie tusipoteze network.
 
Hivi huu mlaini wenu unaopanda E tu ndio nn daaaah,najuta kuwafaham
 
TTCL acheni usanii nitahama huu mtandao soon. jumamosi iliopita nilichuna vibaya vocha za ttcl. nilipiga simu customer service nikaambiwa nitume serial no kisha within 24hrs tatizo litakuwa solved. sasa inaenda wiki kila nikijaribu kupiga simu kuulizia naambiwa kuna changamoto, sijui nitatumiwa msg. tatizo kama hili lishawahi kunikuta huko nyuma na sikupata voucher yangu lakini nikapuizia. This time msiposolve hii issue nahama
 
Mimi leo nimechuna vibaya nimeambiwa 24 hrs ndio nasikikizia
 
Ila bundle za Internet ni majanga kusema ukweli huku Tsh 1,000/= unapata 1Gb dk 100 na sms 100 ila nyie unapata MB400 badilisheni kwanza muendane na soko
 
Kwa kweli ttcl mnahitaji kuboresha bundle zenu, kwa sasa zipo ghali sana.
 
Tangu lini kampuni za serikali zikafanya biashara na kufanikiwa? tegemea machungu zaidi na hasara kubwa
 
Hivi kweli ttcl mnalengo la kukuza hii kampuni ya umma au kuidhoofisha

Hivi kitu Kama vocha TU had mtu aende benki akalipie ndio apate vocha

Mmekosa ubunifu kiasi gani jamn hili nalo linahtaji rocket science ?

Wakat dunia inaenda kasi nyinyi mnarud nyuma ubunifu wenu n zeroooooo mmejaa vilaza

Nilikuwa nataka nijenge nchi yangu kwa kuichangia kupitia taasisi zake lakn inaonekana hamna Nia ya kuijenga nchi kabisa

.....NAISIKITIKIA NCHI YANGU......

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…