TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Ni HERI MARA 1000 usumbufu wa TTCL kuliko WIZI wa VODACOM. nilichokuja kugundua ni kwamba TTCL kuna maeneo inasumbua ila kama eneo nilipomimi

YAANI mpaka nikiona mtu anaiponda TTCL naona kama ametumwa na VODACOM hapa jamii forum. ila Muda wa kazi ukipita , yaani kuanzia saa 11 jioni huwa internet inakuwa slow sana. ila kusema kweli mnyonge mnyongeni ila kwa VIFURUSHI vinavyojali kipato cha mtanzania, hapana kwa kweli, TTCL bei rahisi sana , yaani mimi Tsh. 3000 natumia wiki zima, kuna siku jioni nilipoona mtandao uko slow, nikaweka kifurushi cha VODA cha Tsh.1000, yaani hazikupita dakika 25.
 
Na wewe mkuu yaani unahatarisha maisha yako kipindi cha corona kwenda kuulizia TTCL makao makuu vocha ya 500,hivi siku hizi bado kuna watu mnakwangua vocha? unakwangua na ukijukuta umekwangua namba ya vocha ,mwishowe unabaki huna vocha.
 
Hakuna nmtandao wa hovyo Tanzania kama Ttcl. Bando langu la 5000 ntawaachia na laini nimeivunja.
 
Kampuni mlioingia nayo mktaba(BWW COMPANY LIMITED)kwa ajili ya kusisimamia freelancer ni wababishaji au mtaji hawana. Walichowafanyia vijana wale wanaosajili laini hakivumiliki, si kwa pesa zile walizowatumia jana usiku.

Kwa mwezi mzima mtu anatumiwa elfu hamsini kwa laini 100 wakati kabla ya hapo hiyo ilikuwa pesa ya fomu kwa kila mteja mpya aliyeweka vocha kuanzia 500 wanakulipa 500 kwa laini 100 una elfu hamsini nje na commission ikilinganisha na mitandao kama Tigo, Voda, Airtel wao wanalipa 1000 au 800 kwa kila mteja mteja na bonus juu na vifaa wanavyotumia vya kusajilia laini za TTCL wengi wamenunua kwa pesa zao mfukoni.

Mbaya zaidi imewalipa kwa MPesa badala TTCL na mkataba wao mpaka mwaka 2021 ndio unaisha na huu mwezi NNE ndio mwezi wao wa kwanza tayari wameonyesha udhaifu kuwa mtaji hawana wanategemea pesa za TTCL zinazoletwa na wale vijana kwa kila mteja mpya wanayemsajili.

Anayehusika awasaidie hawa vijana wapate haki yao
 
TTCL inaongozwa kutoka Chato, no creativity, no professionalism.

Unapelekaje tangazo la biashara TBC tv station ambayo haina watazamaji kabisa?
Kwa namna hiyo unadhani utakuwa?

Kwenye huu ulimwengu wa soko la ushindani, TTCL mnashindana na Nani?
 
Mkuu pole sana kwa yaliyokukuta. Pambana utatoboa. Kinachouma zaidi ni kuchomw na jua, kula kwa shida, maneno ya kukatisha tamaa kutoka kwa wateja n.k. Hapo bado baby wako hajakupiga kizinga na kodi ya nyumba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…