TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

TTCL boresheni mtandao wekeni mawakala kila kona ya nchi kama mitandao mingine. tunashindwa kuwasapoti kwakua mtandao wenu mawakala wachache
 
Nashangaa sana na kujiuliza line za TTCL zitapatikana lini? Mpaka maofisin kwenu hakuna. Wako mawakala anakwambia akusajilie kwa 10000 line moja. Jaman Tanzania ni nini hiki #Waziri nape, #Mkurugenzi mkuu Kampuni??
 
Nina kumbukumbu mbaya sana na huduma za TTCL. Huduma mbovu sijawahi kuona yaani ilibidi nicheke badala ya kusikitika. Okay ilikuwa mwaka mmoja uliopita. Siku hizi wamebadilika? Maana nataka wanieletee home internet.
Karibu sana nyumbani mkuu, haujachelewa.
 
Songea huduma ya Ttcl fiber vipi inapatikana?! Na nikitaka kufungiwa inagharimu kiasi gani?
 
Shirika bora la mawasiliano kupata kutokea duniani.
Hongereni @TTCL Corporation nyie ni G.O.AT achana na hawa kima sijui Vodacoma, airtel, zantigo na halotel
 
Kwanini laini zenu hazipatikani? Wiki mbili nilienda ofisini kwenu wakaniambia niende baada ya wiki laini zitakuwa zipo. Nimeenda leo laini hakuna. Nahitaji laini ya TTCL
 
Kwanini laini zenu hazipatikani? Nilienda wiki 2 zilizopita kwenye ofisini yenu nikaambiwa laini hazipo, nimeenda tena leo laini hazipo.
Nahitaji laini
Walisema mwezi huu January 2023 mzigo wa laini mpya ungeingia rasmi sokoni.
Kuwa na subira
 
Sasa nani anatumia huo mtandao huko mtaani mpaka wauzaji wapate wakumuuzia vocha
 
Hamko siriaz na mtandao wenu
 
Hivi mnajua kwamba line za simu za TTCL zimeadimika kabisa mtaani hazipatikani?
Je ni hujuma mnajihujumu wenyewe?
Je mnahujumiwa?
Je mmekata tamaa kwa sababu wateja wanakwepa underperformance ya customer care hafifu mliyonayo?
 
Hivi mnajua kwamba line za simu za TTCL zimeadimika kabisa mtaani hazipatikani?
Je ni hujuma mnajihujumu wenyewe?
Je mnahujumiwa?
Je mmekata tamaa kwa sababu wateja wanakwepa underperformance ya customer care hafifu mliyonayo?
wakikujibu niite mbwa
 
Hivi mnajua kwamba line za simu za TTCL zimeadimika kabisa mtaani hazipatikani?
Je ni hujuma mnajihujumu wenyewe?
Je mnahujumiwa?
Je mmekata tamaa kwa sababu wateja wanakwepa underperformance ya customer care hafifu mliyonayo?

Mkuu kama uko DSM na unahitaji line ya TTCL pita maeneo ya chuo cha usafirishaji (NIT).

Jana katika safari zangu nimeziona pale.
Achana na kuwauliza huku hao wacheleweshaji.
Nimeomba huduma ya fiber mlangoni kwako tangu mwezi wa 7 2022 hadi leo January sijaona simu yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…