Huu mtandao ni utopolo wa hali ya juu.
1.Picha linaanza simu ina bando ila kuperuzi haiwezekani ama usubiri usiku sanaaaa
2.Kupiga simu customer care muda wowote wakipokea katambikie mizumu ya kwenu
3.*148*30# ukachagua INTERNET then ukaenda kwny T-connect plus unakutana na vifurushi vya siku
-Tsh500=300mb
-Tsh1000=750mb
-Tsh2000=2gb
Yani vifurushi vya siku vina gharama kubwa kuliko mitandao mengine yote niliowai kutumia afu bila kusahau kuwa net yao ni pasua kichwa ukitoka mitaa ya posta tu hupati kitu
4.Ukitumia T-Pesa huwe tayari na ela ya akiba mana uwezekano wa muamala kutokukamilika ni mkubwa afu ukiwapigia simu ata wiki nzima hawapokei
5.Makato ya T-Pesa kuenda sambamba na mitandao pendwa mingine huu nao ni uzwauzwa wa kiwango cha PhD.
6.Taarifa za TCRA zinasema wateja kama laki 6 wanatumia huu mtandao maajabu ni kuwa wanashindwa kuudumia wateja laki 6,je wataweza wateja 10M+ km voda na tigo
7.Mtandao ambao ukitoka Dar kwenda mikoani simu yako inageuka kuwa Calculator mana hakuna mtandao tena hapo
8.Mtandao ambao nikiweka jero napata dakika 10 tu usawa wenyewe huu wa magu
9.Mwisho nilikuwa mteja mtiifu wa huu mtandao kipindi unaanza ila nilishatupilia mbali line yao mana ni zaid ya utopolo aseee
Sent using
Jamii Forums mobile app