TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

TTCL Arusha hebu, fungeni mtambo wa 4G au 5G kama upo, ili wenye line za TTCL tutumie kwa raha, maana line za TTCL ni za kuongea internet ni shida, halafu lingine mtandao wenu unachangamoto kutoshika vizuri hasa ukiwa ofisini maeneo Mianzini, Ngarenaro, Kaloleni, Sanawari, Sekei nk.
 
Tatizo langu la Kwanza ni text message haziendi ninapozituma. Tatizo la pili ni kwamba nikipiga simu kwa mara ya kwanza inaenda. Ninapo redial inakataa na kunipamaelezo kwamba namba ninayopiga sio sahihi!
Naomba majibu.

Tatizo nini?
 
Laiti kama mngekuwa mnatumia mtandao wenu basi mngezijua kero pasipo hata kutuuliza wadau, maana ni nyingi tena za wazi wazi...

Kiufupi Kampuni yote iko hovyo hakuna cha uafadhali...
Si uzitaje
 
1. Kuangalia salio la vifurushi, hebu fanyeni mtu aone vyote kwa pamoja na sio data kivyake, voice kivyake..
2. Huduma kwa wateja hawapokei simu!
3. Hakuna notification ukiishiwa salio au usipokuwa na credit kwenye simu
 
Hii kitu ilinitokea siku hiyo hiyo nikatupa Laini yao.


Kwanza Vocha hazipatikani... Nikaamua kuhamisha Salio toka MPesa kwenda TPesa ili ninunue Kifurushi.... Nikajiunga sikupata kifurushi na Salio wamekata.


Nikaamua kutupa Laini Chooni kabisa.
 
Kuna sehemu bado mnasua sua mtandao uko E..sehemu za mijini tu ndo mko vizuri
 
Hii kitu ilinitokea siku hiyo hiyo nikatupa Laini yao.


Kwanza Vocha hazipatikani... Nikaamua kuhamisha Salio toka MPesa kwenda TPesa ili ninunue Kifurushi.... Nikajiunga sikupata kifurushi na Salio wamekata.


Nikaamua kutupa Laini Chooni kabisa.
Pole sana
 
TTCl zingatieni Haya mnayo ambiwa hapa
 
Cha kwanza internet unavyowasha data iko vizuri Ila baada ya dakika kadhaa inaanza kuwa weak.
Cha pili kifurushi cha jiachie wekeni option ya voice tu na ya SMS tu kila kimoja kijitegemee.
Kwenye miradi maalumu ya kiserikali jitahidi mpunguze gharama maeneo hayo.
Kikubwa nawapongeza maana mtandao wenu unashika mpaka katikati kabisa ya mbuga ya selous
 
Nipo DAR, Kawe Beach upeponi, sms zenu ni kero, mna support less than 160 characters
 
Mnazingua sana kwenye huduma kwa wateja hasa mtu akitaka kuongea na mtoa huduma .Dadeki rekebishen
 
kwanza mimi nawapongeza , huwa hamuwaibii wateja vifurushi , pili kiukweli vifurushi vyenu vina bei nzuri saaaana. ila tatizo lipo unapoisha muda wa kazi, ( yaani kuanzia saa 10 jioni ) internet inakuwa slow'' saaana pili hebu jaribuni kuongeza matangazo na mwisho nyinyi wenyewe mujaribu kutumia TTCL network. mimi sioni sababu ya kuwa na network slow wakati mnaambiwa '' leteni bajeti ya mwaka 2020/2021'' ( mapungufu ya mtandao si ndo mnaingiza huko , eeeh, jamani !! ila hilo la matangazo hasa namna ya kupata vocha na T pesa mutilie mkazo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…