TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Nipo Dodoma...TTCL haina usikivu kabisa kabisa...ukimpigia mtu simu kuelewana ni ngumu ngumu sana...ofisini wenzangu wengi Walinunua line zenu kwaajili ya vifurushi vizuri vya sauti.
Lakini sasa ukipiga huelewani na unaempigia kabisa..lazima upige ukate kwanza urudie urudie lakini usikivu wa sauti kwa kampuni yenu ni shida kubwa kubwa kubwa.
Wengi ofisini kwetu wameziondoa line kila mtu alalamikia usikivu..
Mtu umenunua dkk 750 halafu husikilizani na Unayeongea naye mpaka unalazimika kununua kifurushi cha mtandao mwingine upige ndio mnasikilizana vizuri tuu.

Internet sio reliable kabisa..kuna siku na muda inakata kabisa...hakuna Internet.ikirudi haitabiriki mara ipande mara ishuke kabisa.
Mkiboresha hasa usikivu mtafika mbali sana.
Seen
 
Kuna wakati sipatikani nikiwa dodoma mjini lakini ishara ya mnara kwenye simu inasoma ipo full.

Pia internet kwa kutumia modem...niki conect nikatumia internet mara ninapodis-conect..nakuwa siwezi tena ku conect kwa mara nyingine ili nitumie internet hadi siku inayofuata. Nakereka sana na hili dodoma.
 
kuna wakati sipatikani nikiwa dodoma mjini lakini ishara ya mnara kwenye simu inasoma ipo full
pia internet kwa kutumia modem...niki conect nikatumia internet mara ninapodis-conect..nakuwa siwezi tena ku conect kwa mara nyingine ili nitumie internet hadi siku inayofuata. Nakereka sana na hili dodoma
Seen
 
Huduma ndi nzuri kiasi.

Changamoto kwa upande wangu ni 1. Nikipiga simu kwa mtu mfano namba 0768........ Tukaongea naye vizuri tu, kasheshe ni kipiga namba hiyohiyo kwa kutumia call list utakuta imeondolewa 0 kwa hiyo utaikuta 768...... Sasa kama hujaangalia vizuri utakuta unapiga vivyo hivyo. Unakutana na namba unayopiga haipo. Kumbe sifuri imeondolewa.

2 sms kwenda mitandao mingine zina sumbua hasa sms ndefu

3 internet ipo chini sana kwa eneo la Tunduma
 
Mimi natumia modem yenu, internet ni nzuri hapa maeneo ya Kariakoo na Muhimbili ila speed yake sio kivile kama nilivyotarajia....

Pia naomba kufahamu kujua jinsi ya kucheki salio la MBs
 
Mimi nina laini yangu ambayo hapo awali nilikuwa nikijiunga kifurushi cha chuo bila shida yeyote,Tatizo lilianza nilipoibadirisha laini yangu kuwa spesho namba siipati tena huduma hiyo,tafadhali nisaidieni
 
Baada ya matangazo meengi ya kujinasibu sana kuhusu nyumbani kumenoga nikanunua simcard ya TTCL....Duh kumbe nimeingia mkenge.....kwanza coverage yake siyo kiviile kama nilivyofikiria...yaani hata ukisagiri Dar - Dom inapatikana kwa tabu sana....sasa hivi hapa nillipo ni Dom Town pamoja na kuweka 25GB za internet hopeless kabisa....nimeweka ya Voda 80 MB ya kukopa Tsh 500 ....net imefunguka vizuri....na hii ni mara nyingi maeneo mbalimbali....sasa najiuliza TTCL mnakwama wapi mbona huduma zenu za kusua sua sana?...MwaKA jana Aprili niliomba uwakala ...kila siku nikienda napigwa kalenda na maelekezo napewa tofauti tofauti....nika nyoosha mikono.....au likiwa shirika la umma basi ndiyo lazima liachwe nyuma kila kitu?
 
Mimi nina laini yangu ambayo hapo awali nilikuwa nikijiunga kifurushi cha chuo bila shida yeyote,Tatizo lilianza nilipoibadirisha laini yangu kuwa spesho namba siipati tena huduma hiyo,tafadhali nisaidieni
Kitambulisho cha chuo bado unacho?
 
Kamilisha majukumu yako ya wiki kwa bando la bei nafuu kutoka TTCL.

Endelea kufurahia huduma zetu.
Piga *148*30# kisha chagua OFA MAALUM.

# RudiNyumbaniKumenogaView attachment 1502823
103435166_10158688696737884_452055640939712890_o.jpg
 
Nilinunua simu ya mezani wireless huku kigamboni, sasa siwezi kuitumia, very poor signal, imekuwa pambo sebuleni.
 
Back
Top Bottom