Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,743
- 25,564
SeenNipo Dodoma...TTCL haina usikivu kabisa kabisa...ukimpigia mtu simu kuelewana ni ngumu ngumu sana...ofisini wenzangu wengi Walinunua line zenu kwaajili ya vifurushi vizuri vya sauti.
Lakini sasa ukipiga huelewani na unaempigia kabisa..lazima upige ukate kwanza urudie urudie lakini usikivu wa sauti kwa kampuni yenu ni shida kubwa kubwa kubwa.
Wengi ofisini kwetu wameziondoa line kila mtu alalamikia usikivu..
Mtu umenunua dkk 750 halafu husikilizani na Unayeongea naye mpaka unalazimika kununua kifurushi cha mtandao mwingine upige ndio mnasikilizana vizuri tuu.
Internet sio reliable kabisa..kuna siku na muda inakata kabisa...hakuna Internet.ikirudi haitabiriki mara ipande mara ishuke kabisa.
Mkiboresha hasa usikivu mtafika mbali sana.