Ttcl Leo rasmi nimemwaga manyanga Nyumbani kumenichosha, Hii ni baada ya Ttcl kufuta vifurushi vyote vya 500 na 1000, na kupandisha bei ya 500 kwa kila Aina ya kifurushi chake.
Nimefanya tadhimini fupi na kugundua kuwa kutumia ttcl hakuna tofwauti na kutumia Tigo, Airtel nk.. Mf,
Tigo 3000=3Gb per week
Ttcl 3000=3Gb per week
Sasa nyumbani kumenoga kwa kipi...??? Netmbovu, customer care mbovu, vocha tabu then mnajiringanisha value na Tigo, voda, airtel n.k...
Mm ni mteja wa ttcl toka 2015 kipindi hicho kulikuwa kupiga ttcl to ttcl bure, Nimeona transition za ttcl karibu zote..
Mm nimoja ya watu waliwapigia kelele mjenge mnara wa kueleweka Dodoma nakumbuka mpaka mkasema nikusanye number nyingi za simu hili mtengeneze report na nilifanya hivyo nilikusanya about 20 phone number...
Leo nimejaribu kungalia msg za miahamala nilizofanya toka mwaka juzi duuh nikashtuka sana kwa kweli mumempoteza mteja potential..
Leo ttcl inafuta vifurushi vya bei ya wanyonge na kuweka vifurushi vya bei ya kwanzia alfu 5000=juu,
Tadhimini nyingine fupi niliyofanya nimegundua kuwa yawezekana kabisa Ttcl hikawa inahujumiwa na mitandao mingine (private company) kwa maana kwamba wanatumia nguvu ya rushwa kufanya ttcl huwe mtandao mbovu wa ghari ya juu mpaka mteja aone akuna tofauti kati ya mtandao wa serkali na mashirika binafsi hivyo ushindani kati ttcl na mitando mingine unakuwa ziro. Hembu tujiulize sote Ttcl ndio yenye mkongo wa taifa kwanini vifurushi vyake viwe bei juu sawasawa na company nyingine ambazo wamekodi mitambo kutoka ttcl. [emoji848]