TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Mkuu, ebu fanya kama ndio unaanza kulinadi hili shirika la TTCL, maana wengine tinajua lilisha jifia na likazikwa. Naomba uorodheshe baadhi ya huduma zenu internet pamoja na vifurushi vya kupiga simu, na usisahau huduma za kifedha.
 
mimi nipo dar mlipoanza mlinishawishi na kweli internet yenu ilikua the best saizi ni takataka kabisa na line nilitupa mimi kwa mwezi nilikua natumia elfu 40 internet na nilikua na enjoy nikashawishi hadi washkaji ila saizi wananiona kituko hebu fanyeni kama mwanzo mlifanyaje internet ikawa na speed vile badae mkaminya ikawa ina load nikatupa line nikaludi mtandao wa zamani voda
 
TTCL nilikiwa nawatetea sana wako vzr kumbe utopolo mtupu kuna siku niko nabet live inplay kila nikiplace bet mtandao unalet useng.e na hapo miGB kibao ninayo hafu nilikuwa nakula kabisa tokea hapo line yake nimeifungia kwnye droo wajinga sana nyie.
 
TTCL hamna mipando endelevu na huduma zenu mmewalenga zaidi watu waishio kwenye miji tena si miji yote. Nimewahi kutumia Moderm ya TTCL ila usumbufu nilioupata wala sijui nilikoitupa. Ni aibu kuwa shirika la simu la Taifa!
Nilishawahi kuleta uzi humu nikilalamikia huduma mbovu za TTCL hata sijui nianzie wapi lakini mifano michache niliweka laini ya TTCL kwenye WiFI Access link yenye 25GB nikiwa town kabisa DSM- maeneo ya Victoria lakini sikuziona hizo 25GB nikaitupa line nikaendelea kutumia Voda au Airtel.

Mfano wa pili hapa Dodoma ,PSPF PLAZA karibu na DUWASA wamelazimisha wafanyakazi wote tuwe na laini za TTCL ,wengi tumeweka 25GB hivi ninavyozungumza kila mtu analalamika internet haieleweki yaani huwezi kufungua video clips,instagram nk kabisa,iko very slow hivyo tukiwa hapa tunaswitch to mitandao mingine.

SIJUI MNAKWAMA WAPI NYIE VIUMBE
 
Ruaha - Stand ya mbuzi hapa mtandao wenu unazingua, ukiingia ndani unazima ukitoka nje unakubali.. Unanifanya nikose kuangalia muvi online
 
Back
Top Bottom