TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Ukijiunga na bando la bandika bandua unapewa GB 4 ambazo utazitumia kwa mchanganuo ufuatao
Kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa 1:59 usiku unapewa MB 500

Kuanzia saa 2 mpaka saa 11:59 unapewa GB 3.5

Ili bando linawafaa wale walioko bize mchana then usiku wanakua free coz kua nzia saa 2 kamili usiku mpaka saa 11 una enjoy GB.3.5 kwa buku


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ttcl Leo rasmi nimemwaga manyanga Nyumbani kumenichosha, Hii ni baada ya Ttcl kufuta vifurushi vyote vya 500 na 1000, na kupandisha bei ya 500 kwa kila Aina ya kifurushi chake.

Nimefanya tadhimini fupi na kugundua kuwa kutumia ttcl hakuna tofwauti na kutumia Tigo, Airtel nk.. Mf,
Tigo 3000=3Gb per week
Ttcl 3000=3Gb per week

Sasa nyumbani kumenoga kwa kipi...??? Netmbovu, customer care mbovu, vocha tabu then mnajiringanisha value na Tigo, voda, airtel n.k.

Mm ni mteja wa ttcl toka 2015 kipindi hicho kulikuwa kupiga ttcl to ttcl bure, Nimeona transition za ttcl karibu zote..
Mm nimoja ya watu waliwapigia kelele mjenge mnara wa kueleweka Dodoma nakumbuka mpaka mkasema nikusanye number nyingi za simu hili mtengeneze report na nilifanya hivyo nilikusanya about 20 phone number.

Leo nimejaribu kungalia msg za miahamala nilizofanya toka mwaka juzi duuh nikashtuka sana kwa kweli mumempoteza mteja potential..
Leo ttcl inafuta vifurushi vya bei ya wanyonge na kuweka vifurushi vya bei ya kwanzia alfu 5000=juu

Tadhimini nyingine fupi niliyofanya nimegundua kuwa yawezekana kabisa Ttcl hikawa inahujumiwa na mitandao mingine (private company) kwa maana kwamba wanatumia nguvu ya rushwa kufanya ttcl huwe mtandao mbovu wa ghari ya juu mpaka mteja aone akuna tofauti kati ya mtandao wa serkali na mashirika binafsi hivyo ushindani kati ttcl na mitando mingine unakuwa ziro.

Hembu tujiulize sote Ttcl ndio yenye mkongo wa taifa kwanini vifurushi vyake viwe bei juu sawasawa na company nyingine ambazo wamekodi mitambo kutoka ttcl. 🤔
 
Acha kupotosha wewe ......mbona vifurushi vipo vile vile .....

*148*30#
Mbona tunapata vizuri tuu.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kaka kila kampuni ya mawasiliano nchini na hata duniani wanahama na hawapo huko kwenye vocha za kukwangua wote wamehamia kwenye electronic vocha, ndio maana tumewawezesha wateja wetu muweze kununua kwa TPesa, mawakala wa CRDB, NMB, TPB , maxcom na Selcom, utaratibu wa vocha za kukwangua una madhara mengi kuliko faida.

Mabadiliko ya kuimarisha mashirika ya umma yanaendelea na ni kazi endelevu ikiwamo kuungwa mkono na wenye mali wewe ukiwa ni mmoja wao!!

Nimekopi huko facebook kwenye page yao
 
Mbao za Mawe njoo huku kuna kajamaa kaitwa alfatv wanaitetea kampuni yao ya TTCL wanasema ipo poa sana yaani imetulia.
Ina speed ya 15G kushinda kampuni yeypte hapa Afrika.
 
Acha kupotosha wewe ......mbona vifurushi vipo vile vile .....

*148*30#
Mbona tunapata vizuri tuu.....View attachment 1404240View attachment 1404241

Sent using Jamii Forums mobile app
Ww ndio umeona napotosha kwasababu mtandao huu umeaza kutumia juzi ujui tulipotoka na tulipo unachokiona hapo sicho kilichokuwepo kabla

Mm nalalamika kuhusu mabadiliko yasiyo na tija yasiyo shawishi mteja wazamani kuendelea kufurahia huduma mpya.

Hivyo vifurushi ulivyoscreen shot je ni vya ushindani? Je vinaweza kunishawishi niache kutumia tigo,\airtel yangu niamihe Ttcl? Embu jibu kama mzalendo
 
Akikujibu niTAG
 
Umesema hakuna kifurushi cha 500tsh ....sasa hiyo zamani na airtel au tigo ilikuwa bei gani sasa na hivi ....yaani still ttcl iko pouwa .....

Ukirudi na Fiber pia namtumia unlimited plus 50 mins talk time mitandao yote sasa wewe utaniconvice mimi vipi nihame ....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Benhorta ,Nimefanya tadhimini fupi na kugundua kuwa kutumia ttcl hakuna tofwauti na kutumia Tigo, Airtel nk.. Mf,
Tigo 3000=3Gb per week
Ttcl 3000=3Gb per week

Bado umedanganya pia .....
On a screenshot ya kifurushi cha week chagua wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Soma vizuri, Jibu hoja zangu straight usipinde pinde boss, Pia hiyo picha ya kifaa ulichoweka hapo sio hoja yangu, Si kila mtanzania anaweza kumiliki hicho,

Ninachozungumzia hapa ni normal cellural network, Usipindishe hoja za msingi.
 
Nikisubiri umalize alafu nije na screenshots zangu, Zitakazo onyesha tulipotoka na tulipo Pia na washindani wetu walipo tuone Ttcl wanakipi kipya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…