Nyie ni mtandao wa mjini tu, uku vijijini na ukubwa wenu wote mnatumia minara ya TiGo!! Speed ya internet konokono ana speed. Jichunguzeni mnakwama wapi?
Mkuu baba, shirika hili limekaa kipigaji.
Nadhani ni kijiwe cha mafisadi ambao Magufuli na sekeseke lake la kutumbua kashindwa kuwabaini hawa kwa sababu ya pazia la gawio!
Ushauri ulioutoa hapa, umekuwa ni zaidi ya ushauri bali ni mwangwi sasa unaovuma tokea kila kona ya nchi hii.
Siyo kwamba raia hawapendi kutumia huduma hii, bali uongozi na wafanyakazi wa shirika hili ndiyo hawapendi raia watumie huduma zao.
Kama faida yao inatokana na kuuza masafa kama nilivyomsikia siku1 Kindamba akieleza, basi sasa kuna haja gani kuendelea na hii biashara sumbufu ya mitandao ya simu kwa huduma za hovyo?
Wameshindwaje kuboresha minara yao, gharama za vifurushi vya data na voice nk nk ili kushindana na soko la mashirika mengine binafsi?
Ina maana hao staff wa Ttcl hawatumii mitandao ya simu zingine wakaona na kujifunza ubora wa huduma za wenzao?
Kwa utitiri huu wa mitandao ya simu nchini, mtu akiona internet haisomi ipo mkusuasua na vifurushi ghali basi muda huo huo hufyatua line hiyo na kuweka line nyngine.
Tuseme na hili nalo hawalijui?
Lakini niseme tu kwamba, ipo siku ukuritimba wao huu utakomeshwa kidhalilishaji ama kufirisika kabisa,kwani mara ngapi tumeona wakipumulia mashine?
Maana sasa wamekosa ubunifu wa kiushindani.
Yuko wapi Mchechu wa Nhc aliyejinasibu kubadilisha shirika kwamba anajenga na kuuza nyumba kwa bei nafuu, ukiangalia kiuhalisia ni za bei ya kutupwa ambapo mtu wa kipato cha chini hawezi kununua, alifurushwa kwenye mkutano wa hadhara!
Sasa na huyu bado kaziba nta za masega masikioni mwake, hapokei maoni ya wadau wala ushauri wowote wa kuboresha kutokana na soko linavyokwenda, ipo siku yake!