TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Mkuu, maboresho ya intaneti zanazidi kuendelea ili muweze kupata spidi ya 4.5G.

Rudi Nyumbani Kumenoga


Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna kitu... Kwa sasa 4G inapatikana ukiwa katikati ya jiji.. ukiwa nje ya jiji labda buza mbagala, mkuranga hakuna kitu.. mtandao unasoma E..ikijitahidi sana ni H.... inakera sana..badilikeni..
 
Mkuu.

Mimi pia nimeshapoteza pesa, nilinunua vocha from Tigo Pesa to TTCL eeh, ilikua ya 10,000/ mpaka Leo huwa ni story tuu nikaona nitemane nao..
 
Mkuu.

Mimi pia nimeshapoteza pesa, nilinunua vocha from Tigo Pesa to TTCL eeh, ilikua ya 10,000/ mpaka Leo huwa ni story tuu nikaona nitemane nao..
Pole sana mkuu.
Nipe namba zako nikupatie msaada.
 
TTCL kifurushi cha internet GB 5 kwa Mwezi Sh 10000
Vodacom kifurushi cha internet GB 7 kwa mwezi Sh 10000
"Rudi nyumbani kumenoga "
 
Zingatia vitu vifuatavyo ili tuweze kutatua tatizo lako:

[emoji654][emoji654]Sehemu unayoishi.
Ni vyema kama utataja mji, wilaya na hata kijiji ulichopo ili tatizo litatuliwe.

[emoji654][emoji654]Kifaa uachotumia kwa ajili ya intaneti.
Mfano: Modem, Wi-Fi, simu janja au kinginecho.

[emoji654][emoji654]Mawasiliano yako, namba ya simu ni muhimu.

Unaweza kuja PM au kuwasiliana na TTCL Customer Care wetu WhatsApp kwa namba 0738 151 511.

Rudi Nyumbani Kumenoga.
 
Baada ya maboresho ya vifurushi ni changamoto ipi unayopata?
KUMBUKA

[emoji654][emoji654]Je, una ushauri wowote baada ya kuona mabadiliko ya vifurushi?

[emoji654][emoji654]Je, una tatizo la kushindwa kutuma SMS au calls?

Karibu nikuhudumie

Rudi Nyumbani Kumenoga
 
Rudisheni kifurushi cha toboa pack cha GB 10 Kwa 1000

Tulikuwa tunaenjoy sana
 
Duh kweli Tanzania tumekuwa kiuchumi ila vifurushi navyo mmepandisha bei kinoma, hizo bei sio rafiki kama hapo awali
 
Nilikuwa nikitoa 10,000/- napata GB 12 kwa mwezi na sasa 10,000/- napata GB 7 kwa mwezi.

Haya, kwa wiki nilikuwa nikitoa 2500 napata GB 3 sasa hivi kwa 3500 napata 2.5 GB.

Nimewahama kwa kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…