TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Vocha zenyewe mitaani HAMNA,

Izo bando tunaweka vipi?
 
Tatizo huduma zenu zipo mijini tu yan huku vjijin wala hakuna network mnatiwa gepu kubwa na hawa halotel waliokuja juzi juzi,Halotel network yao inapatikana hadi huku chaka hebu tanueni wigo wa mtandao wenu,hiwezekan kilomita 600 kutoka Dar network hakuna,hili ni shirika la taifa la mawasiliano hebu lipeni hadhi basi.All in all hongereni na hilo bando lenu jipya.
 
Hata baadhi ya sehemu za mjini ukishakuwa mbali na Barabara, mfano huku uswahilin kutoka Barabara kubwa kama Kawawa na Morogoro road ukizid kuingia uswahilin network yao mbovu. Pia maeneo ya Kigogo Luhanga kutoka Barabara kubwa pia network yao hovyo sana. Kwahiyo nadhan itakuwa vizur zaid kama mtaimarisha network yenu pia mijin.
 
😀😀😀ila we jamaa unachekesha sana kama huwezi kujibu ni vyena kukaa kimya. Wameulizwa coverage ipoje wamepiga kimya kazi tu kutoa pole
Ndugu mteja, kipindi naanza kutumia mtandao wa TTCL network ilikuwa haipatikani hapa Buza.
Nikawasiliana na uongozi wao, asubuhi nakuta nimeumiwa ujumbe wakiniuliza kuhusu tatizo baada ya kuwaeleza wakasema upo sehemu gani?
Nikawaambia Buza, wananiambia subiri baada ya dakika 5.
Baada ya dakika 5 wananitafuta wakaniambia angalia network kama ipo sawa.
Kudadeki kitu kilikuwa kinasoma H+ ikipungua sana mwisho ni 3G.

Hivyo basi TTCL Customer Care wakikuuliZa unapatikana wapi?
Ujue wanataka wajue tatizo linalokukabili na kulifuatilia ili walitatue.

TTCL anafanya ROAMING kwenye minara ya Tigo
 
😀😀😀 thank you for your amazing stoy but no thanks.
 
Juzi juzi tu nimeitupa line baada ya kukaa nayo siku 3.
1. Network slow sana.
2. Huwezi itumia line kwenye kitochi. Inafanya kazi kwenye smartphone tu.
 

TTCL tatizo ni kubwa kuliko wengi tunavyoliona na watu wengi walishashauri kuwa wafanye "Shut down" kwanza ya uongozi pale juu kabisa halafu isukwe team ya kiushindani kibiashara na waweke pembeni siasa zao za " RUDI NYUMBANI KUMENOGA" hapo ndipo TTCL itanoga na watakuwa na bei ya chini kwa sababu tayari miundo mbinu mingi wanayo na wataweza kufikia watu wengi kwa wakati mmoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…