TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Nyie jamaa sijawahi kuwaelewa kabisa sijui mnafeli wapi, hampigwi faini za ajabu kila siku kama wenzenu, nasikia nyie ndio internet provider kwa wengine (sijui kama ni kweli) lakini bado naona huduma zenu za vifurushi za kuunga unga sana.

Nyumbani bado hakujanoga.
 
Ongea, Peruzi na chati bila kikomo na Jiachie bando

# RudiNyumbaniKumenoga

151358944_10159393014102884_7471934062265208490_o.jpg
 
Wekeni
Jiachie bila kikomo kwa Buku tu.View attachment 1710115
Hebu wekeni T-Connect Plus ya mwezi inayoleta mantiki hata kama ni equivalent to weekly bundle manake ni ujinga kifurushi cha wiki kuwa Sh.10,000 kwa GB10 halafu kifurushi cha mwezi kuwa Sh 70,000 GB40 au eti GB15 kwa Sh 30,000. Matokeo yake, mnatusumbua wateja kwa sababu hakuna mwehu anayetumia pesa yake ya mfukoni atakayejiunga kifurushi cha GB 40 kwa Sh 70,000 wakati anajua akiwa ananunua in weekly basis atalipa Sh 40,000 badala ya 70K.

Mnaweza kuona sasa tatizo lipo wapi but mnatupotezea muda kujiunga bundle kila wiki! Na lingine msilojua, kuna uwezekano mkubwa mtu wiki akanunua GB 10 za TTCL, na next week akanunua ya mtandao mwingine na matokeo yake mnakuwa nyie ndo loser, kumbe kama mngeweka angalau equivalent monthly bundle, say 40GB kwa 40,000 hapo tayari mnakuwa na uhakika wa Sh 40,000 yenu wakati kwa sasa uhakika huo hamna!! Na mfano mzuri ni mimi mwenyewe.

Juzi 21/02 nimenunua GB10, leo mmenitumia message eti bundle yangu inaisha 23/02 saa 4 usiku! Bora muwe mmekosea lakini ikiisha kweli wakati ni weekly bundle, wala sitapoteza muda eti kuwapigia kuwaliza kulikoni, nawakimbia tu kama ambavyo nimekuwa nikifanya mara kwa mara! But what kama ingekuwa nimekuwa nimechukua monthly bundle equivalent to weekly bundle?

Hapo tayari mngekuwa na 40K yangu!!
 
Back
Top Bottom