TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Mkuu sina chuki
Lakini jaribu kujiuliza hizo dakika 100 zote za nini?
Why msiongeze MBs maana siku hizi hatabbaadhi wa watu wanawasiliana kwa kupigiana simu kupitia WhatsApp
Tatizo Baharia wa Buza unachuki mbona vifurish vipoi vyenye MB za kutosha,
 
Huo Mtandao Ni Jijini Tu
Huko Vijijini Shida
Wadau mimi niko tabora ndo mtandao wangu huku nzega mitandao mingine shida ila TTCL ni baba lao naona wote mnaopinga ni upotoshaji mkumnwa voucher zinapatikana na unaweza kununua kupitia mitandao mingine kama vida pesa

Aitel money na mingine hakuna mtandao kama ttcl unaweza nunua salio kupitia mitandao mingine pia unaweza nunua pitia bank zote.
 
Nyaku Mm sipondi mtandao wa Ttcl ila najaribu kutoa changamoto kwao tazama hata tigo days back walibadilisha vifurushi vyao nini kilitokea kwenye mitandao na pages za za kijamii, Wateja wengi waliponda, walilamika na wasio wasatrabu walitukana sana then kipi kilifanyika baada tu ya Two weeks Tigo walifanya mabadiliko makubwa kwenye vifurushi vyao.

Embu jiulize vip Kama wateja wangebaki na kukua kimya au kusifia nini kingetokea...?? Tigo ingepoteza wateja wengi hasa wapya.

Nikiri kabisa kabla ya kuijua ttcl nilikuwa natumia mtandao mwengine wa simu ila kilichonishawishi kuhama na kujiunga na Ttcl ni ushawishi wa huduma hasa vifurushi vyake niliusianisha na gharama zake na mtandao nilikuwepo wakati ule na mwisho nika decide kuhamia si hoja ya uzalendo iliyonipekeka Ttcl,
Ss basi kama ttcl inabadili vifurushi na nikae kimya kisa uzalendo hapo hatuisaidi kitu chochote lazima wambiwe
 
Seems umetumwa aisee na hauna uzalendo ndani yako ,TTCL Ni mtandao wa kitanzania na unaendeshwa na watanzania wenyewe badala uwe wa kwanza kuitetea wewe mtanzania mwenzetu ndio unakua wa kwanza kuichafua, tupende vya kwetu jamani

Sent using Jamii Forums mobile app
Hoja ya uzalendo ni dhaifu, Kuwa mzalendo akunifanyi ni kae kimya, nishinde hata kutoa maoni yangu kisa uzalendo

Pia kumbuka siku ya kwanza nakutana na mawakala wa usajili wa Ttcl hawakuniambia amia Ttcl kwakuwa ww ni mzalendo bali walinishawishi niamie Ttcl kwa kuwa wanahuduma bora, vifurushi vya bei nzuri na internet speed hipo vizuri.

Kwanini leo nionekane mbya nikihoji swala la vifurushi
 
Sio siri ngoja niende kwenya mada moja kwa moja.

Huu mtandao una matatizo mengi sana kama yafuatayo:

1. Huduma ya T PESA
Aisee huu mtandao kama utatuma hela siku ya Ijumaa usiku ghafla litokee tatizo wallah utakuja kuhudumiwa siku ya Jumatatu.

Hili tatuzo limenipata juzi hapa Ijumaa tarehe 7 yaani nilitamani kulia wallah.

2. Vifurushi
Hawa majamaa ukitaka uende nao sawa kwenye masuala ya MBs nakushauri tafuta kitambulisho cha chuo.

Aisee yaani GB 5 kwa Tsh 5000 mwezi mzima.

3. Vocha
Asikwambie mtu, TTCL hawana vocha aisee. Jana nimeenda pale Makao Makuu niliulizia vocha ya 500 hakuna wanasema zipo za 1,000.

Aisee ukienda kuulizia madukani yaani muuzaji anaweza akashangaa maana hiyo vocha ya TTCL ndiyo kwanza anaisikia kwako.

Kilichonipata jana
Nilijiapiza nikaonane na Afisa Masoko pale Makao Makuu pale Posta ili nimshauri kitu kimoja tu. Yaani nikafika mapokezi nikaonane na bwana Kindamba lakini nikazuiliwa.

Yule mama wa mapokezi aliongea sana mpaka wakati naondoka nimeinamishwa kichwa chini kwa masikitiko. Maana shida yangu nilitaka kuonana na Afisa Masoko au CEO wao.


Nilitaka niwambie kama vocha mtaani ni ngumu basi katika option ya kununua bando mteja achague alipe upitia T PESA au salio la kawaida.
 
Pole sana Baharia wa Buza,

Lakini ningependa kukuhakikishia kwamba, pamoja na mafanikio bado tunaendelea na jitihada za ziada kuhakikisha nchi nzima na kila mahali kunafikiwa na vocha za kukwangua. Pia ningependa kukutarifu kwamba unaweza kujipatia vocha zetu za TTCL kupitia njia mbalimbali za kielectonikia kama kupitia MAWAKALA WA NMB, KUNUNUA SALIO KUTOKA ACCOUNT YAKO YA NMB, MAWAKALA WA CRDB, KUNUNUA SALIO MOJA KWA MOJA KUTOKA ACCOUNT YAKO YA CRDB, KAGA CONNECT, MAWAKALA WA WASELCOM, KUPITIA ACCOUNT YAKO YA T-PESA AU WAKALA YEYOTE WA T-PESA Alie karibu nawe. Tafadhari endelea kufurahia huduma zetu za TTCL@TTCL Corporation

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu your very right, walivyo anza walituaminisha mtandao wao ni 4G na of course speed ya internate ilikuwa nzuri, nikashauri ofisini tujiunge nao na tukajiunga sasa hivi ni majanga ku download file dogo tu la MB chache can take even more than an hour leo wenzangu wameshauri tuachane nao nimewaomba tuwatizame mpaka mwisho wa wiki na kama wakiendelea hivi, ndio wamshatukosa Corporate customer wao
Hawa majamaa ni wahuni sana hawa yaani nimejiunga GB 10 ili nipakue vitu vangu chaajabu network ipo slow kama kinyonga.

Kesho asubuhi alfajiri na mapema naivunjavunja laini yao kwa meno yangu.
Uzi tayari.
TTCL

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku mbili tatu hizi 4G ya ttcl imegeuka kuwa 2G ya airtel. Very slow! Video ya dakika 5 youtube unaiangalia lisaa limojana nusu na bado huimalizi

Sent using Soviet T-72 Main Battle Tank
 
Siku mbili tatu hizi 4G ya ttcl imegeuka kuwa 2G ya airtel. Very slow! Video ya dakika 5 youtube unaiangalia lisaa limojana nusu na bado huimalizi

Sent using Soviet T-72 Main Battle Tank
Niliona iko slow nikahisi labda ni huku eneo niliopo nimerudi zangu tigo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom