TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Wee ndio mtu wa marketing kiongozi...? Kwa hiyo hapo ndio Umemaliza kwa upande wa vifurushi mlivyonavyo...?
 
Jibu lako ni hilo hilo moja kwa kila tatizo kwenye hii thread?

“Pole kwa changamoto hiyo,tafadhali tufahamishe unapatikana maeneo gani ili tufuatilie na kutatua.
Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.”

Wewe ni robot?
 
Mkuu@TTCL custome care, naomba msaada ,simu yangu iliharibika nikaiweka ndani kwa muda wa mwezi na nusu, nimepata simu mpya naweka voucher imekataa, napiga customer care wananijibu kwamba nimevuka kiwango cha malipo ya simu. Anastahili kufanya je ili niwezie kutumia lakini yangu tena
NiPM namba yako tafadhali.
 
Wananzengo, niende moja kwa moja kwenye HOJA.

Nimekuwa nikijiuliza hivi hii kampuni ya TTCL ipo au ilishakufa maana hatuoni inafanya nini. Imeshindwa kabisa hata kuuza tu vocha, sasa bila kuuza vocha inapata wapi fedha za kujiendesha?

Kwanini hakuna hatua za kufumua hiyo kampuni mapema ili kuondoa hasara?
 
Hii kampuni kunabaadhi ya Mambo wanayotakiwa kuyaweka sawa ili wateja wavutike kuutumia. Jambo la kwanza ni kuhakikisha upatikanaji wa vocha zao maeneo mengi mtaani coz wengi wanaweza wasihamasike kutumia huu mtandao kwa kuwazia changamoto ya upatikanaji wa vocha maeneo wanayoishi. Japo najua zipo njia mbadala za kupata salio lakini mteja ni mtu ambaye hapendi usumbufu. Jambo la pili lazma wahakikishe salio la kupiga mitandao mingine liwe na dakika nying kwa gharama nafuu coz haiwezekani mtu anunue salio apewe dakika 35 za kupiga ttcl to ttc na dakika 5 kwenda mitandao mingine angali kwenye simu unawatu wasiozidi wawili wanaotumia mtandao wa ttcl Sasa sijui itakulazimu uongee nao tu ili kuzimaliza hizo dakika 35.
Naunga mkono hoja.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Aaaaaah nyie vijana mnapelekeshwa na wazee wanaotumia vitochi katika age ya smartphone so hata hawaoni umuhimu wa bundle kuwa kubwa.... Wanarahisisha maisha kipuuzi.
[emoji23][emoji23][emoji23]
Mbona mtamdao upo poa nowdays.
 
Obvious suala nitakalozungumzwa Pasi na shaka limezungumzwa na members hapo juu, Ila nitumie tu fursa hii kukazia maarifa, kiukweli TTCL ndio mtandao wangu kwa Mishe ya Internet na ninaenjoy vifurushi vyenu. Ila tatizo kubwa mpo tu katikati ya miji.

Napata shida sana nipokwenda nyumbani kusalimie huko Lindi vijijini.. Yaan ukianza kuiacha tu municipal ya Lindi basi mtandao unasepa mazima.

Nipo pale Nyangao - Lindi barabara kuu ya kuelekea Masasi District Ila mtandao hausomi kabisa.

Kwa nini wasiwe kama halotel ambao wanapatikana hadi remote area..?

Kuhusu suala la vocha za TTCL huwa siwazii, actually vocha zao ni adimu sana hata mijini Ila kwa kuwa kuna huduma ya T-Pesa hii ndo inanirahisishia sana, So naomba mlifanyie kazi hili.

Ni Mimi mteja wa TTCL kutoka NYANGAO-LINDI
Asante kwa ushauri wako.
Tunaufanyia kazi.
 
Back
Top Bottom