Obvious suala nitakalozungumzwa Pasi na shaka limezungumzwa na members hapo juu, Ila nitumie tu fursa hii kukazia maarifa, kiukweli TTCL ndio mtandao wangu kwa Mishe ya Internet na ninaenjoy vifurushi vyenu. Ila tatizo kubwa mpo tu katikati ya miji.
Napata shida sana nipokwenda nyumbani kusalimie huko Lindi vijijini.. Yaan ukianza kuiacha tu municipal ya Lindi basi mtandao unasepa mazima.
Nipo pale Nyangao - Lindi barabara kuu ya kuelekea Masasi District Ila mtandao hausomi kabisa.
Kwa nini wasiwe kama halotel ambao wanapatikana hadi remote area..?
Kuhusu suala la vocha za TTCL huwa siwazii, actually vocha zao ni adimu sana hata mijini Ila kwa kuwa kuna huduma ya T-Pesa hii ndo inanirahisishia sana, So naomba mlifanyie kazi hili.
Ni Mimi mteja wa TTCL kutoka NYANGAO-LINDI