TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Tumekurahisishia! Sasa nunua kifurushi chako pendwa cha BUFEE na ulipie kupitia akaunti yako ya T PESA.
Ni rahisi sana.
Piga *148*30#
Kisha ingiza 6 BUFEE PACK
Jitengenezee kifurushi kisha chagua lipa kupitia T PESA.

#RudiNyumbaniKumenoga
View attachment 2140707
 

Attachments

  • IMG_1635.jpg
    IMG_1635.jpg
    53.3 KB · Views: 50
Ttcl, je naweza kumtumia mtu mtandao mwingine salio langu la TTCL?

Ama naweza kumnunulia mtu wa mtandao mwingine kifurushi kutoka kwenye salio langu la laini ya ttcl?
 
Ttcl, je naweza kumtumia mtu mtandao mwingine salio langu la TTCL?

Ama naweza kumnunulia mtu wa mtandao mwingine kifurushi kutoka kwenye salio langu la laini ya ttcl?

Hiyo huduma kwa sasa haipo, ila tunaifanyia mchakato ili iwepo.
 
Hivi kwanini msg nyingi za Utapeli,zinatoka kwenye no za Ttcl?? Mnatumia vigezo vipi ninyi kuzirasimisha line zenu za Ttcl??
Binafsi huwa nahisi kuna mapungufu sehemu,jitahidini kudhibiti line zote ambazo hazijarasimishwa kwa usahihi ili iwe rahisi kuwafuatilia hawa matapeli
 
Kwenye upande wa dk na sms big up sana, kwa kuwa kwa Tsh 500 najipatia hadi dk 130 mitandao yote bila kikomo cha muda!
Shida ni kwenye internet bufee! Tsh 500 napata MB 387, tatizo ni kuwa nikiishawasha data tu, na zenyewe zinaanza ku accelerate hata kama nikiwa nimezima data!! Tena siku hizi mnapima kwenye muda, hata kama mtu amenunua bufee internet na hasilitumie, utashangaa baada ya masaa 12 mnamtumia sms ya umetumia 75℅ ya bando lako na hapo ndo basi tena!!
Shughulikieni hili wakuu kabla hatujarudi tigo, huko kumenoga zaidi!
 
Back
Top Bottom