KERO TTCL Fiber Kimara Temboni tumedhulumiwa pesa zetu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Godee jr umesikia hapo kituo cha mwisho ni Kisutu kawashtaki
 
Reactions: Lax
kwahiyo toka mlivolipa kifurushi mara ya kwanza hamkulipa tena sio? na mkifatilia mnapewa ahadi gani? na kwa huo wingi wenu mbona mlitakiwa muwe mshatatua tatizo mapema
Hatukulipa tena. Walitoa ahadi kuwa wangewasha mwezi wa 10, baadae wakasema wa 11. Wakaja wakasema January.
Cha kushangaza kila mwezi wanatuma Control number na na baadae wanakupigia simu kukumbusha kulipa. Ukiwaelezea huduma hakuna wanatuletea mafundi wao ambao ndio hao wanaotoa ahadi hewa
 
hapo sasa changamoto, ila kama mkiungana na mkalalamika kwa pamoja watu wote hao, tafuta hata watu 5 unaolewana nao kiasi wape namba hiyo kila apige simu kwa wakati wake akilalamikia hilo jambo na akitoa hiyo historia, mkiwa 10 itapendeza zaidi --- kumbuka kutupa mrejesho
 
Sawa mkuu
 
TTCL ni moja ya shirika la Umma linalikufa kwa kuzidiwa wateja baada ya UDART. Nimeomba toka mwaka jana mpaka leo sijafungiwa
 
Niliwazia kitaa wakati wanapita pita hapa na pale.

Fasta nikawaita wamefunga kwangu so far Iko vizuri sema Ina katakata sana
 
Niliwazia kitaa wakati wanapita pita hapa na pale.

Fasta nikawaita wamefunga kwangu so far Iko vizuri sema Ina katakata sana
ni shared hii, nadhani ndio sababu ya kukata kata, ninachotaka kufahamu ni moja 70,000 na nyingine 55,000 nilitamani nijue tofauti ya hizi bei mbili.
 
ni shared hii, nadhani ndio sababu ya kukata kata, ninachotaka kufahamu ni moja 70,000 na nyingine 55,000 nilitamani nijue tofauti ya hizi bei mbili.

View: https://www.instagram.com/p/DUlBvY0jc-l/


cha 70,000/- wanakupa na simu ya mezani ya ttcl, unapata dakika 300, 20GB kwenye laini moja ya ttcl , na router kifurushi unlimited cha 20mbps

cha 55,000/- unapata kifurushi cha router tu, unlimeted speed 20mbps
 
Line zimejaa, hawanag Hesabu hawa watu, ni kukosa tu akili
 
Watanzania sijui tupoje!
Wewe unataka wateja, umewapata wamelipa gharama za awali kisha huwapi huduma kwa mwaka mzima.
Kisha unawatupia wao lawama hawafuatilii!!!!
Miezi you're hiyo wangekuwa wanalipa 70K kila mwezi kwa watu 50 unageingiza kiasi gani?
70,000x50x12= 42,000,000
Hii haitoshi gharama za ulinzi, usafi au maji hapo ofisi kuu ya TTCL?
Wenzenu wanapambana kushikikia wateja nyie mnataka wake kuwabembeleza kuuulizia huduma. Mnataka pesa yao waliyo tafuta kwa jasho iwatese wakati wanaitumia?
 
Wanatia hasira sana hawa watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…