TTCL fiber na Voda Supakasi ipi yafaa kwa matumizi ya home intaneti?

Huduma za TTCL ni za ajabu sana, fiber imekata Toka alhamisi mpaka leo ni siku ya 5 huduma sipati hapa nilipo... Nimefatilia sana ila naona Mambo ya ajabu tu... Watumishi wa hili shirika ndo wanaliua.. upuuzi kama huu unasababisha shirika watu waliogope.. nosense kabisa

Just assume nipo less than a km Toka makao makuu ya shirika la TTCL ya mkoa nliopo na huduma zinakuwa ovyo kiasi hiki, vipi walioko wilaya tofauti inapotokea kukosekana kwa huduma inakuwaje.. waache kufanya kazi kimazoea yaani kama vile shirika halijajiandaa kufanya kazi
 
Hamnaga kitu kama unlimited kwa pesa hizo! Tena hao Voda ndio matapeli kabisa.
Labda kwa Tanzania, nchi kama India JIO na Airtel Fiber wanakupa huduma ya uhakika tena at 50mbps kwa less than Tshs 40000 monthly
 
Hali ikoje hadi sasa mkuu? Speed inakuwa ileile mwezi mzima?

Vipi hoja ya huyu mwenzetu?

"Ulitakiwa kuomba ufafanuzi kuhusu hizo the so-called unlimited kwa sababu ingawaje huwa wanasema ni unlimited, mara nyingi kama sio zote zinakuwa sio unlimited wala nini! Ulitakiwa kufahamu wanatoa GB ngapi kwa sababu sio kwamba ni unlimited GBs!

Zamani hawa watu nilishagombana nao sana! Unalipa wanakuambia unlimited one months, unashangaa baada ya siku kadhaa bundle imekata au wamepunguza speed na kuwa ya jongoo!

Ikabidi niwapandie huko huko ndipo wakaniambia huwa wanafanya makadirio, kwa mfano wanakupa 30GB huku wakiamini zitakutosha mwezi mzima na ndo maana wanasema unlimited!!

Sasa kama matumizi yako ni makubwa tofauti na makadirio yao, ndipo hapo bado siku 15, umeshatumia 25GB... sasa utamaliza vipi siku zilizobaki, ndipo wenyewe wanakuwa wameweka cap kwamba zikabaki 5GB, automatically speed inapungua mno, to the point hata ku-download file kubwa inakuwa issue!"
 
Mkuu ungeeleza hivyo vigezo na masharti ungetusaidia sana
 
Leo nimefunga nyumbani Vodacom Supakasi..kiukweli ipo vizuri na inastream poa kabisa kwa wapenzi wa content za online..kama haupo karibu na access ya fiber basi supa kasi itakufaa..
Hongera. Vipi hakuna kiwango cha matumizi ya data? Labda ukifikisha 1 terabyte internet ina kata au slow down?
 
Mkuu ungeeleza hivyo vigezo na masharti ungetusaidia sana
To get Vodacom 5G internet service vigezo ni

-Certified copy of tin no
-certified copy of ID or Driving license
-Security deposit of 2 months payment

Then you get your internet service
 
Ttcl Adsl kuanzia Ubungo Mataa kuelekea Kimara, Mbezi Mwisho nk haipo, wanadai raia walishaharibu miundombinu.

Ttcl fiber kwenye maeneo hayo wanasema wanamsubiri mzabuni alete vifaa ndio wataanza kuwafungia waliofanya maombi tayari.

Wanachofanya kwa sasa ukienda unajaza form yao, kisha unasubiri mafundi wanaofanya survey ya kila Jmos na Jpili.

NB: Kama ttcl wameshindwa kucover fiber Dar tuu, kimkoa kidogo namna hii, sijui huko mikoani watakuja wafikiwe lini.

 
No need for antenna kama LTE ambayo yahtaj antenna

Hii utapew Nokia fastmile gateway device Kwa ajili ya kupata internet through FWA system mkuu
Maana yake nahama nayo popote pale?
Je kwa Mbeya Kyela itafanya kazi?
Kwa Dsm Saranga itafanya kazi? Kule kuna sehemu za miinuko sana?

Kama itafanya kazi tuongee tufanye biashara

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Maana yake nahama nayo popote pale?
Je kwa Mbeya Kyela itafanya kazi?
Kwa Dsm Saranga itafanya kazi? Kule kuna sehemu za miinuko sana?

Kama itafanya kazi tuongee tufanye biashara

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
5G coverage iko temboni, bonyokwa, Saranga, kimara,suka

Nmekutajia area zile ambazo umeonesha interested kama Saranga apo

Tuna coverage ya almost 50% Kwa dar es salaam so if interested we can work and do business
 
Kwamba fiber ya ttcl ipo morogoro road?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…