TTCL fiber na Voda Supakasi ipi yafaa kwa matumizi ya home intaneti?

TTCL fiber na Voda Supakasi ipi yafaa kwa matumizi ya home intaneti?

Wakuu habari zenu.

Natumai mu wazima.

Kutokana na mabando kuwa juu, niliamua kwenda maduka ya TTCL na Voda shop kuangalia home internet.

TTCL walinipa hii details.
View attachment 2097538

Kulingana na matumizi yangu nilipenda hicho cha 55k.

Lakini sijajua wakoje kihuduma plus kununua DSL modem.

Nikaamua kucheki Voda Supa kasi

View attachment 2097542

Voda wana laki 115000 lakini nimeenda Voda Shop Ubungo plaza wananiambia wana Laini ya Supakasi Unlimited 50k kwa mwezi.

Watalaamu naomba ushauri ni ipi reliable isiyo na speed ya kusua sua ili nichukue nihustle kutafuta hela.

Mabando ya 3k kila siku yanaumiza alafu unatumia kibahili sio.

Naombeni msaada sana.

Shukrani in advance.
Ukitazama quality ya matangazo hayo mawili utapata majibu
  1. Tangazo la TTCL linaonekana lipo hoi bin taabani, je tutegemee huduma bora hapo!?
  2. Tangazo la Vodacom linajitanabaisha kuwa watoa huduma wako smart
 
Inategemea na fundi aliyefanya configuration ya router wengi wanaweka band moja tu.
Ikishakuwa wifi 5 kuendelea inakuwa na band zote 2.4ghz na 5Ghz.

2.4ghz ina range kubwa ndio maana hao mafundi wanaweka kama default sababu wifi isipofika mbali utalalamika.

5ghz ina speed ila range yake ndogo, most of time hii watu hutumia kufanya Configuration za Gaming, streaming etc ndani ya Nyumba,
 
Tofauti ya TTCL Fiber na Vodacom supakasi ni thahiri mbili tu, mengine ni minor

  1. TTCL Fiber ni fixed delivery so huwezi kutumia nje ya ofisi au nyumbani wakati Supakasi Vodacom ni mobile, wireless, unaweza kusafiri nayo nk
  2. TTCL ni cheap TZS. 55k/month wakati Vodacom supakasi ni TZS. 115(4G)/month
 
IMG_0024.png

Supakasi hao
 
IMG_1951.png

Hivi hii changamoto ni kwangu tu au hadi huko kwenu.
Namaliza mwezi sasa Supakasi kupata 10Mbps ni ndoto.
 
Mfano Fiber ya TTCL ni 1TB kwenye Terms zao wameandika, ina maana uki abuse na kutumia zaidi ya 1TB kisheria wanaruhusiwa kupunguza speed.

Sijajua term za Voda zipoje.

Huku voda bwana chief mkwawa hatujawai kuona usumbufu sisi kwa mwezi nafikir tu natumia zaidi ya 3TB na hatukuwahi kukwama tuna upload na kudownload movie na bado nina download mafaili ya simu na kuna wadau jirani hapa tumewapa password hao sijui matumizi yao yakoje ila kasi tunapata ni ile ile
 
Wakuu mnaotumia supakasi ikitokea katikati apo hujalipia kama miezi miwili kunakua na shida?
 
Back
Top Bottom