TTCL Fiber ukimuunga mtu atumie Wi-Fi yako moja kwa moja anakuwa na access ya router yako

TTCL Fiber ukimuunga mtu atumie Wi-Fi yako moja kwa moja anakuwa na access ya router yako

sema wewe ndio ujui kubadiri password ya router ya ttcl , ulitakiwa kuja kuuliza nmna ya kubadiri password ya router ya TTCL na sio ulichokuja kusema
Mkuu tupe huo muongozo wa kubadilisha password ya router ya TTCL itakua msaada mkubwa sana kwa wadau humu ndani maana ni tatizo hakuna anayejua na hata ukiwafata wanataka uwape customer namba ya router wakufanyie wenyewe kwa kweli utakua umesaidia sana kwa hilo.shukrani
 
Mkuu tupe huo muongozo wa kubadilisha password ya router ya TTCL itakua msaada mkubwa sana kwa wadau humu ndani maana ni tatizo hakuna anayejua na hata ukiwafata wanataka uwape customer namba ya router wakufanyie wenyewe kwa kweli utakua umesaidia sana kwa hilo.shukrani
Jaribu superuser kote user Na password.
 
Tatizo kubwa lilopo awakupi uwezo wa kufanya chochote kama mteja wao ata kubadilisha password lazima uwatafute wao
Apo ndo Kipengele yaani wana amini unaweza Lipia Huduma yao kila mwez ila hawakuamin kuchange Password zako😂😂
 
Yes ila mpaka uwe na access sasa ya kuingia kwenye setting ili uwaunge kwa Mac address Access awakup jamaa
TTCL washamba tu. Jaribu user user au admin admin..kama hawakubadili itakubali.
 
Inaonekana TTCL nikweli wamebadilsha utaratibu, kipindi cha nyuma mteja alikua anapata access ya settings za router yake.

Sababu ambazo nadhani zimechangia TTCL kunyima wateja username na pswd.

1. Kuna watu walikua wanabadilisha username na password ikitokea kuna tatizo kwa mteja inakua usubufu mkubwa kwa mafundi wa TTCL, unakuta wamepigiwa simu wanakuja wanakuta password zimebadilishwa na hazijulikani.

2. Wengine kwa utundu wamekua wakichezea settings zilizokua preconfigured na hivyo kupelekea kukosa huduma ya internet, na kupelekea usumbufu wa kuita mafundi mara kwa mara.

3. Kuzuia/kulinda miundombinu yao.

Solution

Nunua router nyingine ambayo utakua na uwezo wa kufanya chochote TTCL atabaki kuwa ISP/WAN kuanzia hapo kwenda mbele utakua na control ya network yako.

Analogia ya hii shida ni kama ifutavyo.

TTCL wamekukabidhi geti ila hawataki kukupa funguo za hilo geti, kwa hivyo huna udhibiti wa asilimia 100 na hilo geti,

Cha kufanya ni kuweka geti jingine jipya mbele ya geti la TTCL weka vitasa na funguo unazotaka hili geti jipya utakua na udhibiti nalo kadri utakavyopenda bila kugombana na TTCL na geti lao.
 
Chief-Mkwawa Kuna mikoa naona uhitaji wa wateja wa wi-fi, ila huduma mbovu hivi hawa hawakubali franchising?.

Yaani una ingia nao ubia wa kusambaza vifaa na huduma, Kisha mna katiana percentage?.
Kiranga una fahamu kuhusu hili?.

Iwe voda, ttcl.
Wanakubali, Tanga hapa kuna Fiber ya Bahoza, source ya Fiber ni Tigo, ukifuata utaratibu unaweza kuwa Mvno wa kampuni nyengine, sema si uwekezaji wa kitoto.
 
Wanakubali, Tanga hapa kuna Fiber ya Bahoza, source ya Fiber ni Tigo, ukifuata utaratibu unaweza kuwa Mvno wa kampuni nyengine, sema si uwekezaji wa kitoto.
Ohh ina pendeza, maana naona Kuna maeneo huduma ina hitajika Sana.
ila hao watoa huduma wako bize maofisini.

mfano minimum yaweza kuwa ngapi?
 
TTCL Fiber mlangoni kinachoboa ni kwamba ukimuunga mtu atumie Wi-Fi yako basi yeye moja kwa moja anakua na access ya router yako anaweza unganisha mwengine kwa ku-share QR Code au ku-access Password kabsaa hii kitu ina boa sanaa.

Na hawa jamaa hawakupi access ya router labda hubadili Password hawakupi Ukitaka ku change Password hadi uwa tafute wao ndo waje wa change na unaweza wasubir miezi ndo waje wa change.

Hili linakera sanaa aisee kwanin hawati access hata ya kuchange Password basi waweke security ya mtu kuto share password na QR Code ukisha mjoin.
Kuna fewtures ya wewe kutengeneza Guest WIFI - ambayo utakaempa password yake atakuwa anapata internet tu na atakuwa na acess ya router yako
 
Back
Top Bottom