Inaonekana TTCL nikweli wamebadilsha utaratibu, kipindi cha nyuma mteja alikua anapata access ya settings za router yake.
Sababu ambazo nadhani zimechangia TTCL kunyima wateja username na pswd.
1. Kuna watu walikua wanabadilisha username na password ikitokea kuna tatizo kwa mteja inakua usubufu mkubwa kwa mafundi wa TTCL, unakuta wamepigiwa simu wanakuja wanakuta password zimebadilishwa na hazijulikani.
2. Wengine kwa utundu wamekua wakichezea settings zilizokua preconfigured na hivyo kupelekea kukosa huduma ya internet, na kupelekea usumbufu wa kuita mafundi mara kwa mara.
3. Kuzuia/kulinda miundombinu yao.
Solution
Nunua router nyingine ambayo utakua na uwezo wa kufanya chochote TTCL atabaki kuwa ISP/WAN kuanzia hapo kwenda mbele utakua na control ya network yako.
Analogia ya hii shida ni kama ifutavyo.
TTCL wamekukabidhi geti ila hawataki kukupa funguo za hilo geti, kwa hivyo huna udhibiti wa asilimia 100 na hilo geti,
Cha kufanya ni kuweka geti jingine jipya mbele ya geti la TTCL weka vitasa na funguo unazotaka hili geti jipya utakua na udhibiti nalo kadri utakavyopenda bila kugombana na TTCL na geti lao.