TTCL kero hii itaisha lini?

TTCL kero hii itaisha lini?

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,703
Reaction score
1,724
TTCL (Shiriki la mawasiliano la Tanzania) leo ni mara ya nne nakatwa pesa kila niingizapo vocha kwenye simu.
Mie huweka vocha tatu za shs 1,000/= ili nijiunge na kifurushi, cha ajabu naweka vocha ya kwanza haikatwi ya pili inakatwa ya tatu haikatwi.
Mara ya tatu usiku nilijaribu kununua bando kupitia T-pesa ikashindikana, ikanibidi kuongeza salió kwanza kupitia T-pesa napo nikakatwa.
Mara zote nawapigia na wananirekebishia. Sasa ntaendelea kuwapigia mpaka lini kila niongezapo vocha???
 
Mimi internet imekatwa leo ingawa nimeshalipia ,hawa jamaa ni kwikwi ,very unreliable haya ndio mashirika bora tumuuzie muhindi tu
 
Mimi internet imekatwa leo ingawa nimeshalipia ,hawa jamaa ni kwikwi ,very unreliable haya ndio mashirika bora tumuuzie muhindi tu
Ukweli sasa ni tatizo tena kubwa sana.
Jana, nimetafuta wakala ili niweke pesa kwenye cm na kununua kifurushi cha king'amuzi cha Startimes, nimezurura Tabora mjini wengi hawana huduma ya T-pesa na baadhi hawaifahamu.
Nikaelekezwa na mfanyakazi mmoja mstaafu wa TTCL nikafanikiwa. Mida ya saa tisa mchana nikatuma pesa Startimes ya kifurushi, mpaka saa hii hakuna kitu.
Mapema leo nikawapigia T-Pesa na nikawaeleza kukatishwa tamaa na huduma MBOVU wanayonipatia.
Nikiingiza vocha ya pili kati ya tatu, nakatwa. Nalipia king'amuzi kupitia T-Pesa napo shida.
Inakera.
 
Back
Top Bottom