TTCL: Mpaka sasa tumefikisha Mkongo wa mawasiliano wa Taifa katika wilaya 121 kati ya 139 Tanzania Bara

TTCL: Mpaka sasa tumefikisha Mkongo wa mawasiliano wa Taifa katika wilaya 121 kati ya 139 Tanzania Bara

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722

​
Mkurugenzi Mtendaji wa TTCL, CPA Moremi Marwa, akizungumza leo Aprili 10, 2026, wakati wa uzinduzi wa minara 758 ya mawasiliano na uunganishaji wa mkongo katika wilaya 85, Marwa amebainisha kuwa hadi sasa mradi huo umeshafikia wilaya 121, ambayo ni sawa na asilimia 82 ya utekelezaji nchi nzima.

"Mheshimiwa, Shirika la Mawasiliano Tanzania linatekeleza mradi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ambao ulianza kutekelezwa kwa awamu mbalimbali kuanzia mwaka 2009.

Hadi sasa tumefikisha huduma ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwenye wilaya 121 kati ya wilaya 139 za Tanzania Bara ambapo ni kama asilimia 82.

Aidha, shirika linaendelea na mradi wa kufikisha huduma ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwenye wilaya 18 zilizobaki, na tunatarajia kwamba ifikapo mwezi Desemba mwaka huu, tutakuwa tumefika wilaya zote za Tanzania Bara"


 
Mkongo wa mawasiliano mikoa yote wakati hata vocha madukani hamna.

Nimeishi na line yenu ndio nikaamini hili shirika kweli linajiendesha kwa hasara.
 
Mkongo wa mawasiliano mikoa yote wakati hata vocha madukani hamna.

Nimeishi na line yenu ndio nikaamini hili shirika kweli linajiendesha kwa hasara.
zama za kununua vocha za kukwangua ZISHAISHA.
 
Hamna kitu,hasara haijawahi kuisha katika ilo shirika,mtabebwa mpaka lini?
 
Back
Top Bottom