KERO TTCL ni sikio la kufa! Haiwezekani kwa zaidi ya miezi sita nimeomba huduma ya fiber nyumbani wananizungusha tu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Uaomba fiber mtaani kwako imepita? TTCL wamewaaminisha watanzania popote unapata finer lakini kiuhalisia kuna maeneo hayana miundombinu ya fiber, so inabidi wakuungie mtu mmoja na hapo ndio ugumu unaanzia.
 
Kama huduma ya fiber haijapita mtaani uungwana ni kumjulisha muombaji ili musisumbuane.
 
Sina hamu na hawa jamaa TTCL, Mimi nilitoa gharama zote za nguzo kama 4 hivi na hapo nikampa kitu tech wao na huko ofisini wakanila karibia million yote nifanyiwe haraka, nikaja kupata mwisho wa siku sasa changamoto za huduma zikaanza haipiti wiki Net down nianze kuwapigia na hapo pesa kidogo lazima umpe atakwambia shida tumeitatua kuna sehemu wire basi muhimu kila wiki kuna issue utasema wanafanya kusudi. Nikaamua kuachana nao na kusahau gharama nilizoingia na toka wakati huo sitaki hata kuwasikia.
 
Inategemea na ulipo, isije ikawa upo km 5 toka ilipopita ikawa ni gharama sana kukufikia. Sisi tuliopo dodoma tunaenjoy tu
Kwa upande wangu cable ya fiber imepita na kugusa juu ya bati la nyumba yangu. Lakini nina zaidi ya mwaka mmoja toka nimeomba sijapata huduma.
 
Upo wapi? Na je miundombinu ya fiber ipo karibu nawe? Ujue vitu vingine tutailaumu TTCL bure tu,

Unakuta mtu yupo madongo kuinama A miundombinu ipo Madongo kuinama C na ili kumfikia inahitaji km kama 6 za waya na mteja ni mmoja, sasa kweli Shirika litaweza kumfikishia kila mtu ilhali bado na mhusika unaweza kuta yupo peke yake


Ndio maana wanasogeza taratibu ili iwafikie kwa ujumla
 
Mkitaka kujua hili tatizo ni kubwa kiasi gani, tembelea page zao za instagram, tafuta post zinazoitangaza fiber mlangoni kwako. Nimechukua chache mjionee. Wengine wameamua hadi kuwatag wahusika mbalimbali wenye dhamana akiwamo waziri so there is no way viongozi hawana taarifa juu ya uzembe huu.







 
Hivi si anatakiwa aje mpimaji ili kuona miundo mbinu imekaaje then ndio wafanye maamuzi na wakujulishe juu ya maamuzi yao? Sasa hata mpimaji haji hadi miaka inapita watajuaje juu ya miundo mbinu ya eneo lako? Na walalamikaji wengine wanadai nguzo zipo mbele ya nyumba zao na baadhi ya majirani wanapatiwa huduma. Unasemaje juu ya hilo?
 
Hii huduma inaombwa online kwa website yao. Mfano mimi awali ya yote niliwaambia sehemu nilipo na wakasema wapo wamefika na pia wanasema ukiona mtaa wako haupo wakati wa kujaza kwenye website basi hawajafika. Lakini nimejaza na hadi nyumba number niliikuta ile leo ni karibia mwaka hawajaja.

Halafu uungwana mwingine mteja anapopiga simu na kuuliza ni vema kusema kuwa huko hatujafika tarajia siku fulani, wanapokuwa wanasema tutakutafuta wanalenga nini?

Kama ndio utetezi mmeambiana mje kusema hapa, fikirieni upya.
 
Ndugu zao na DAWASA, wavivu sana wa kufikiri. Ni karibia mwaka sasa huduma ya maji hatujapata tangu tufanye maombi ya kuunganishiwa. Hovyo kabisa.
Mkuu hao penyeza rupia ndio maana rushwa haishi kwa sababu kama hizi. Hizo taasisi za umma nao waanze kulipwa mishahara kutokana na faida wanayozalisha
 
Haitakaa seriall iendeshe biashara.watebdaji hawana uchungu. Private sector is the best solution
 
Rewards zisipokuwa tied na performance ndio mashirika yanakuwa hivi.

Tigo Fiber nimeunganishwa ndani ya siku 1.... sijasaini hata paper moja, nimelipa pesa; kesho fiber ndani ya nyumba. Nimeletewa mkataba baada ya mwezi.

Kama upo eneo lina Tigo Fiber, nenda huko, achana na hao TTCL. Kwanza huduma yao yenyewe ni kimeo.
 
Inasikitisha sana
 
Hakuna shirika la umaa linalotoa huduma inavyostahiki.

Serikali inajisumbuwa na kutia chooni pesa za walipa kodi kuendelea kuyalea haya mashirika ya umma, hayana faidia yoyote.
you meant faida? sure.
 
Nchi ya kitu kidogo hii.
Hivi mlienda na shati la mikono mirefu huko au mlienda mikono mitupu.

Walishaambiwa wale urefu wa kamba zao.
 
Mimi nimejaza form zaidi ya mara 10, nikaenda mpaka ofisini kuuliza kulikoni nikajibiwa vifaa hakuna lakini vikija nitapigiwa simu, kimya, nikajaza tena hola, nikaandika email nikajibiwa nikaunganishwa na masavea kwenye email nikawasiliana nao wakaishia mitini.
Nikaenda voda siku 3 nikapewa huduma japo ni gharama lakini afadhali.
Kama unataka fiber kwa sasa halotel ni wa moto🔥 sana na bei chee mno.
TTCL ni 🚮
 
Shirika la kiduwanzi sana hili

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…