James Hadley Chase
JF-Expert Member
- Mar 25, 2020
- 1,984
- 3,695
Unajua ID anayotumia?Mhandisi Peter Ulanga
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unajua ID anayotumia?Mhandisi Peter Ulanga
Naunga mkono hojaCCM inaendelwa kuua nchi kupitia mashirika yake haya yanayofanya mambo pasipo tija yeyote...
Ukienda sasa pale makao makuu yao ukawaona utadhani wapo serious...
Wazee wa kalenda hawa🤣,We unasema Miezi 6?
Si wengine tuna miaka mitatu tangu ile siku ya kwanza wanazindua kampeni yao ya fiber mlangoni watu tulianza process na mpaka sasa hakuna responding.
Huko ofisini kwao tumeenda sana mpaka ikafika hatua tukaanza hadi kuwajua wafanyakazi wa pale kwa majina.
Ikafika muda unaingia tu ofisini unaskia "Aah Scars naona umekuja kufuatilia swala lako" na mimi najibu "ndio Edward si unajua bwana Omary siku ile alinisisitizia kuwa leo nikija nitamkuta Mateo ambaye anahusika na eneo langu"
Hii si kweli wote wanaolalamika sana wengi wao wapo karibu na hizo facility, ukitaka kuamini wewe soma comments tu, usipoona tatizo kwao hiyo itakua tatizo lingineInategemea na ulipo, isije ikawa upo km 5 toka ilipopita ikawa ni gharama sana kukufikia. Sisi tuliopo dodoma tunaenjoy tu
Nimeona mkuu, basi ni changamoto kwa kweliHii si kweli wote wanaolalamika sana wengi wao wapo karibu na hizo facility, ukitaka kuamini wewe soma comments tu, usipoona tatizo kwao hiyo itakua tatizo lingine
hayo ndo mashirika ya umma mkuu, sasa wewe fikiria complain zote hizi mtaani , mitandaoni lakini hakuna juhudi za kueleweka wanachukua, na washindani nao wanakuja kwa kasi, Na raisi alisema hawa kwa hali waliyofikia wabaki tu kwenye intaneti na hali yao yenyewe ndo hii. ukireflect mbali unakuja kuona mwendokasi, ndege na yawezekana hat ile treni tukaja kukwama vilevileNimeona mkuu, basi ni changamoto kwa kweli
Haya mashirika mengi ya umma yapo kisiasa zaidi.Mashirika yamejaa Wazee walio foji umri,
Wewe nawe una mawazo ya kiarabu arabu muda wote. Mbona kuna nchi nyingi kabisa mashirika ya umma yanafanya kazi vizuri kabisa? N usimamizi wa serikali iliyopo madaraka tu na hamna cha zaidi. Mtu kama Samia na CCM yake tunaweza kutegemea ufanisi kwenye usimamizi wakati wao wenyewe ni mafisadi na wavivu wa grade one? Ngonya nikuambia: Haya mashirika yote ya umma yakipata serikali iliyo makini yanafanya vizuri tu. Kwa nini wasipewe ajira zao kwa mkataba wenye makubaliano? Kwa mfano hili la usambazani na ufungaji wa fiber wanaambiwa muda wa ku-process maombi usizidi muda fulani na kama hawafanyi hivyo mkataba unavunjika na wafanyakazi wote wanaondolewa na kuajiriwa wapya kwa mkataba mpya. Hili litafanya kila mfanyakazi aone umuhimu wa kujiwajibika kwani asipofanya hivyo anajua ajira itaisha.Haya mashirika mengi ya umma yapo kisiasa zaidi.
Ni ujinga wa Mtanzania. Marekani mpaka inayofana na na Benki Juu, Federal Reserve, ni ya watu binafsi. Serikali wanawawekea sheria, sera na taratibu tu za kufata. Yaani ni facilitators tu.
. Hapa kwetu inabidi tubadilike, kwenye biashara iwe biashara,
Bora wazee kuliko baadhi ya vijana ni kero kubwa..Mashirika yamejaa Wazee walio foji umri,
Aisee! Pole sana. Nimeomba kwa njia ya mtandao ijumaa nilipigiwa simu kutoka kwao kwamba kuanzia leo wanaweza wakafika home kwaajili ya survey. Nitaleta mrejeshoBaada ya hapo nikaja kuambiwa kuwa eneo langu kifaa cha kuunganishia fiber kimejaa hivyo engineer wao yupo kwenye process ya kutengeneza kingine.
Hiyo ilikuwa ni Septemba mwaka jana.
Mpaka leo hicho kifaa bado engineer anakitengeneza.
Nikaona bora nichukue Router ya Airtel ambayo mpaka sasa naweza kusema ndio option bora kwasababu inakupa extra benefit ya kuweza kuitumia popote lakini advantage nyingine ni kuwa na uhakika wa kupata huduma hata pale umeme unapokuwa umekatika kwasababu ina battery yenye reserve ya ku store charge kwa masaa zaidi ya 8.
unaombaje huduma kwa hao muflisi ambao hawajielewi kabisa, tafuta watu wengine hao umbwa unapoteza muda tu kwanza hata wakishafunga huduma zao utakuja kuniambia baadae.Habari za muda huu Wanajamvi,
Hii Kampuni ya TTCL ni sikio la kufa na wala halisikii dawa tena, haifanyi vizuri kwenye mawasiliano ya simu kawaida wala kwenye Internet. Mimi nipo Dar es Salaam na nimeomba huduma ya kufungiwa internet nyumbani (fiber) na sasa yapata miezi sita ila sijafungiwa wala hakuna kitu cha maana kinachoeleweka kutoka kwao.
Ukihitaji Internet wanasema inabidi uombe kupitia website yao na ukifanya hivyo kwa kweli ni kwa haraka tu maombi yako yanapokelewa na kuambiwa yanafanyiwa kazi. Unataarifiwa mara moja kwa ujumbe mfupi (sms) na hapo hapo kwenye website yaani unaweza kusema kweli hawa jamaa ni top-notch na nitapata huduma fasta kabisa.
Ila hapo sasa ndio mchezo unapoanza, utazungushwa hadi ujute mwenyewe. Nimepiga simu zaidi ya mara 5 kwenye namba yao ya huduma kwa wateja wanapokea na jibu lao mara zote linakuwa "Ni kweli umeomba fiber, ombi lako tunaliona na tunalifanyia kazi. Mafundi wetu wa eneo lako watakupigia simu ili waje kukuunganishia". Baada ya hapo nimekuwa nikuliza kwamba hao mafundi watakuja lini atleast mnipe muda kabisa nijue au nifanye taratibu nyingine, hapo utajibiwa "Tafadhali kuwa mvumilivu, mafundi wetu watakutafuta"
Hata hivyo, baadhi ya watu wanasema TTCL hawaji kufunga internet hadi wapate shinikizo kutoka kwa Wakubwa zao. Yaani utafungiwa Internet ukiwa unawajua hao wakubwa ambapo hili ni jambo la ajabu kabisa kwa Taasisi ya Serikali kama ile inayoendeshwa kwa kodi za Wananchi.
TTCL kwa sasa sitaki tena huduma yenu hii, nitafunga internet ya watu wengine na kwa mtindo huu hamtakuja kuwa shirika la maana na hata nashangaa lile gawio mnatoa kwa Serikali huwa mnatoa wapi. Hii Kampuni inakufa hata Wakurugenzi wabadilishe kwa namna gani.
Pia soma;
1. Kuchelewa kupatikana kwa huduma ya internet ( fiber) TTCL
2. Huduma ya TTCL ya kutoa Internet nyumbani ni mbovu sana
Mwaka jana waliniambia vifaa vya kufanyia installation vimeisha hivyo nisubiri.Aisee! Pole sana. Nimeomba kwa njia ya mtandao ijumaa nilipigiwa simu kutoka kwao kwamba kuanzia leo wanaweza wakafika home kwaajili ya survey. Nitaleta mrejesho